Chanzo cha kuchokana, kununiana katika mahusiano/ndoa na jinsi ya kukabiliana na tatizo hili

kwenye kuitwa baba fulani inatokana sana na watoto kwenye familia yenye watoto wadogo inabidi kuitana kama wanavyofanya watoto ili watoto wajue kuwa yule ni baba, unapomwita jina lake mfano Peter au darling unawachanganya sana watoto kiasi kwamba kesho akiulizwa baba yako nani atajibu 'darling'

ile inafanyika kwa sababu ya watoto ila huko chumbani mkiwa peke yenu au kwenye chakula cha usiku mnaweza kuitana majina yote ya mapenzi

kuna katoto kamoja baba yake alikuja na wageni basi kikamkimbilia na kumuita jina lake mfano Peter Jipanguse dingi yale nae akajibu rrrrrrrrraaaaa rrrrrrrrrraaaaaaaa wale wageni hoi kwa kicheko nasikia hako katoto kanamwita baba yake kwa jina lake la kwanza na nahisi ni kutokana na mama yake anavyomwita mumewe

so kwa familia yenye watoto kuitwa baba fulani au mama fulani nadhani imekaa fresh tu ila mkiwa 6 x 6 inakuwa haijatulia
 
kwa nn ukiona mtu amekuudhi usimweleze mpaka uanze kununa utakuta mtu umechelewa kurudi or anything then mtu anakuchunia hii ipo sana kwenye ndoa hapa TZ

Kununa kuna maana yake.. mtu anayenuna mara nyingi ( siyo zote) hawezi kupigishana kelele kama kaudhiwa.Ananuna kama namna ya kufikisha ujumbe kuwa all is not well. Pia kufuatana na culture za baadhi ya jamii kunyima unyumba bana ya waliooana inaashiria zaidi ya adhabu - disengagement following a major problem na siyo kutofautiana kidogo tu mtu anakimbilia kumnyima mwenziwe!
 
hivi wew umemkera mkeo na ukajua hasa kuwa kakasirika .................hata dakika tano nyingi unataka unyumba! serously unategemea afurahie hilo tendo?

kina baba mnawapa wanawake muda mgumu ..........akiwakatalia mtasema kanuna akiwakubalia itakuwa sawa na kuwa raped tu since akili yake bado iko kwenye hamaki na mwili wake upo off

Kwani wanawake hawawaudhi/wakera waume zao?? Wao haombi unyumba?
 
na wewe unajua kabisa ukichelewa utaamuudhi sasa y uchelewe bila tarifa na ukija husemi lolote...mie nakununia kabisa na kama umeniudhi kikubwa mwili wangu nao uhusahau mpaka tuweke mambo sawa.
mie nashauri kuwe na mawasiliano mazuri kwenye ndoa kama ukiona mtu kachelewa unamuuliza kwa upole mtu ukifika m/mke anaanza kuwaka na wewe ukiwaka ananuna utakuta usiku unyumba unanyimwa wakati ni haki ya ndoa na mwanaume akinyimwa unyumba ni dharau kubwa sana na ni moja ya vitu ambavyo kisheria vinaweza kusikilizwa na kukubalika kuvunja ndoa na mahakama
 
eee pamekucha!!!!

kuitana baba nanii au mama nanii inahusu???, kuitana majina yetu au majina mbadala inapendeza.

kuhusu kununa mnataka tufanye nini?? lijitu jingine kila siku linakosea na kuomba msamaha, kujirekebisha hakuna, inatia hasira
 
hawa wanaume wakiwa na hasira/wakinuna wanaishia baa badala ya kukaa na kusolve matatizo family
 
inategemeana huenda ikawa suluhisho au kuongeza tatizo wanaume wengine hawatoi huduma mpka unune je ufanyeje sasa?.
 
mie nashauri kuwe na mawasiliano mazuri kwenye ndoa kama ukiona mtu kachelewa unamuuliza kwa upole mtu ukifika m/mke anaanza kuwaka na wewe ukiwaka ananuna utakuta usiku unyumba unanyimwa wakati ni haki ya ndoa na mwanaume akinyimwa unyumba ni dharau kubwa sana na ni moja ya vitu ambavyo kisheria vinaweza kusikilizwa na kukubalika kuvunja ndoa na mahakama

Hakuna kitu kibaya kama hicho; naongea from xperience nakwambai ni Neema ya mungu ilituponya kwani the moment mwenzio anakufanyia hivyo inaleta messsage mabya sana kwako na unachukia toka moyoni; kibaya zaidi waweza kufanya lolote baada ya hapo kwani saa zote mtu unakuwa na hasira na kwa wenye roho nyepesi hushindwa kujizuia; Ilitugharimu sana sisi kupona na janga na nawaa couples humu ndani msinyimane eti ikiwa ni silaha ya kurekebishana; MMEKWISHA!
 
inategemeana huenda ikawa suluhisho au kuongeza tatizo wanaume wengine hawatoi huduma mpka unune je ufanyeje sasa?.
hapana kununa si kitu kizuri na hii wanawake wengi kama sio wote wanaitumia sana but no inaongeza kuchukiana tu ktk mapenzi unajua m/ume anapenda sasa kuelezwa live (ukweli) kisha yaishe kwa nature yetu sasa utakuta mmegombana mchana mtu anaweka kisasi hadi usiku au wiki nzima kwa kweli binafsi sipendi hicho kitu

nimekumbuka wimbo wa Marlaw na Chid Benz unaitwa "Bado Umenuna" jaribuni kuusikiliza
 
hawa wanaume wakiwa na hasira/wakinuna wanaishia baa badala ya kukaa na kusolve matatizo family
utaanzia wapi kusolve wakati mtu amekununia hakuongeleshi chumbani mzungu wa nne au anakupa mgongo hapo unategemea nn kama sio kukuzidishia hasira tu na matokeo yake mtu unaona bora ukae baa na kupiga story na walevi wenzio ukifika home ni kulala tu
 
hapana kununa si kitu kizuri na hii wanawake wengi kama sio wote wanaitumia sana but no inaongeza kuchukiana tu ktk mapenzi unajua m/ume anapenda sasa kuelezwa live (ukweli) kisha yaishe kwa nature yetu sasa utakuta mmegombana mchana mtu anaweka kisasi hadi usiku au wiki nzima kwa kweli binafsi sipendi hicho kitu

nimekumbuka wimbo wa Marlaw na Chid Benz unaitwa "Bado Umenuna" jaribuni kuusikiliza

lakini muda mwengine hua ni chachu ya mapenzi pia
 
kwa nn ukiona mtu amekuudhi usimweleze mpaka uanze kununa utakuta mtu umechelewa kurudi or anything then mtu anakuchunia hii ipo sana kwenye ndoa hapa TZ

Mtu akikuudhi, inakuwa ngumu sana kumsemesha, hapa unasubiri labda yeye aanze mazungumzo, labda nimechelewa nilikuwa sehemu fulani, lakini unakuta mtu anauchuna hasemi alipokuwa na wewe unakuwa umeshajikoki kwamba yeye ndiye aanze kujielezea, sasa na yeye unakuta ameuchuna anataka uanze kumuuliza, ulikuwa wapi? Hapo ndo huwa pagumu kwani unajidai hutaki kujua mambo yake huku unataka, roho inaungua lakini unaona ukimuuliza atazoea kuwa anakwenda anakotaka, analudi saa anayoijua yeye, hasemi alipokuwa kwa kujua wewe utamuuliza na wewe ndo hivyo hutaki kumuuliza, kwa hiyo mnakuwa m-menuniana kwa sababu eti hakuna anayetaka kuanza mazungumzo.
 
hapana kununa si kitu kizuri na hii wanawake wengi kama sio wote wanaitumia sana but no inaongeza kuchukiana tu ktk mapenzi unajua m/ume anapenda sasa kuelezwa live (ukweli) kisha yaishe kwa nature yetu sasa utakuta mmegombana mchana mtu anaweka kisasi hadi usiku au wiki nzima kwa kweli binafsi sipendi hicho kitu

nimekumbuka wimbo wa Marlaw na Chid Benz unaitwa "Bado Umenuna" jaribuni kuusikiliza

Kuna wanaume mabingwa wa kununa usiombe!
Mwanaume anayenuna na kuzira anaboa kuliko maelezo!
 
Mtu akikuudhi, inakuwa ngumu sana kumsemesha, hapa unasubiri labda yeye aanze mazungumzo, labda nimechelewa nilikuwa sehemu fulani, lakini unakuta mtu anauchuna hasemi alipokuwa na wewe unakuwa umeshajikoki kwamba yeye ndiye aanze kujielezea, sasa na yeye unakuta ameuchuna anataka uanze kumuuliza, ulikuwa wapi? Hapo ndo huwa pagumu kwani unajidai hutaki kujua mambo yake huku unataka, roho inaungua lakini unaona ukimuuliza atazoea kuwa anakwenda anakotaka, analudi saa anayoijua yeye, hasemi alipokuwa kwa kujua wewe utamuuliza na wewe ndo hivyo hutaki kumuuliza, kwa hiyo mnakuwa m-menuniana kwa sababu eti hakuna anayetaka kuanza mazungumzo.

Vunja Ukimya.......zungumza na mwenzio............swallow your pride and egos! .......................kwa hisani ya Watanzania wenzio!
 
Wanawake wamezidi bana sasa ukinuna ndio nini kama si kujipa ugonjwa usio na tiba..
 
Back
Top Bottom