Tetesi: Chanzo cha afisa biashara aliyechana Quran tukufu ni kurogwa; aliwatesa wafanyabiashara katika ukaguzi wa leseni

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,466
2,000
Katika kufuatilia chimbuko la kisa cha Afisa biashara aliyeonekana akichana kitabu cha Qur'an!

Moja mwananchi ambaye hakutaka jina lake litajwe; Amesema Aliwahi kufungiwa biashara yake changa na afisa huyo walipo mkamata na mgambo wa halmashauri kwa kudaiwa kutokuwa na leseni;
Pamoja na kujitetea kuwa biashara yake ilikuwa changa na alikuwa tayali kashaanza mchakato wa kukata leseni lakini Afisa huyo pamoja na wenzake ( walimfungia biashara yake na kuondoka naye kimabavu kiasi cha kulipishwa faini ambayo hata hakupewa risiti!

Mnyetishaji huyo alizidi kusema, matendo ya afisa huyo yameumiza wafanya biashara wengi kwa kutisha na kukamata wafanya biashara!

Mnyetishaji huyo anasema Kitendo cha kuchana Quran ilikuwa ni mwanzo tu wa pigo katika kuelekea kutembea uchi!

Na iwe fundisho kwa maafisa wengine wanaotumia nafasi zao kunyanyasa wengine!

Waziri Jafo mnamo tarehe 7 feb 2020 alitoa tamko la kumsimamishwa kazi mtumishi huyo na kumwagiza mkurugenzi wa kilosa kumchukulia hatua ya nidham! Kwa maana hii mkurugenzi usisahau kupitia namna alivyokuwa akitekeleza majukumu yake kama mtumishi wa serikali ili kubaini kama kuna mazingira ya Rushwa yalifanyika hadi kupelekea mtumishi huyo kuchanganyikiwa!
quran.jpg


Updates

Huyo jamaa bundi kazidi kumuandama tena na leo; magufuli kamfukuzia mbali!
Yaaan anapigwa kama mpira wa kona!

Kiufupi ndugu zake wajiandae kwa lolote kuanzia sasa! Vinginevyo Mkono wa Mungu uingilie kati
 

Jembekillo

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
4,245
2,000
Hayo maeneo aliyochania hiyo quran me napajua ni opposite na stendi ya mabasi ya kilosa kuna bar inaitwa Shinyanga then pembeni kuna kijiwe cha bodaboda.

Hao bodaboda huwa wanaanza kuwatania walevi wa hiyo bar kwa kuwaambia kuwa hawawezi kufanya jambo fulani hata akilewa vipi. Sasa mlevi akiona hivyo anatafuta namna ya kudhihirisha atafanya nini ili aonekane jasiri.

Huyo afisa biashara ni mlevi mbwa alikuja kulewa hapo bar, baada ya kulewa ndo akakutana na bodaboda wakaanza kumwita mlokole gani wewe unalewa hovyo, akajibu dini yake ndo bora kuliko dini yoyote hata hao waislam si lolote kwake.

Bodaboda mmoja akampa juzuu amma akamwambia ichane hii kama unaweza. Huyo mlevi akaichukua akaanza kuichana huku wanamrekodi video. Ndio mwanzo wa hiyo issue.

So yawezekana ni kweli karogwa ndo maana anafanya vitu nje ya self control au pombe ndio imempelekea kupata ujasiri wa kuchana maneno ya Allah (s.w)
Mengine nawaachia wahusika!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,466
2,000
Kimsingi uchawi ni lazima utafte chanzo cha kukuingia ili ukuangamize! Pombe na hao boda ni mbinu tu ya kumaliza mchezo!

Kwani hujawahi ona mtu anarogwa anateleza kidogo lakini kishindo cha kuangua utazani katoka ghorofani tena anaangukia utosi? Jiulize huwa inawezekanaje
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,304
2,000
Hata Mimi niliwaza hivyo. Huyu Jamaa NI mwendawazimu. Katika Hali ya kawaida MTU ambae kichwani zinamtosha hawezi kufanya upuuzi kama huo tena mbele ya camera
Yule mwehu

Kachanganyikiwa 100%

Sio akili timamu ile
 

Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,375
2,000
Hizo nguvu za kuchizisha watu (kama ni kweli) si bora wangezielekeza kwenye kuvutia wateja kwenye biashara zao.

Watachizisha wangapi? Dhulma nchi hii imewekwa na inalindwa na mfumo!
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,466
2,000
Hizo nguvu za kuchizisha watu (kama ni kweli) si bora wangezielekeza kwenye kuvutia wateja kwenye biashara zao.

Watachizisha wangapi? Dhulma nchi hii imewekwa na inalindwa na mfumo!
Unafikili mnapojaa kwa mangi huwa hakuna dawa? Wee wa wapi! Kichwa cha kondoo huwa kipo chini hapo tayali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom