Chantal Kazadi kama Patrice Lumumba.

Kulwanotes

Member
Nov 3, 2021
22
55
Stori za muziki.

Kwenye album ya Titanic yake JB Mpiana ya mwaka 1997 na Band yake ya Wenge BCBG Les Anges Adorables; kuna wimbo uitwao Baracuda. Katika wimbo huu namba tatu kwenye album hiyo, dakika ya 3:20, JB Mpiana anataja maneno haya 'Afrika sukisa Chantal Kazadi'.

Unaweza usikiliza hapa [Procès Mambika-Boomplay Music]. Nilikuja yasikia tena maneno haya katika wimbo wa Koffi Olomide[siukumbuki ni wimbo gani]. Binafsi napenda sana kufuatilia historia katika muziki. Nilikuwa nikiifahamu—kwa kuisoma na kusikiliza nyimbo zake—band ya Afrika Sukisa ikiwa chini ha Dr Nico Kasanda. Swali kwangu lilikuwa ni nani hasa huyu Chantal Kazadi? Kutokana na vyanzo mbalimbali, nilivutiwa sana na historia ya kimuziki ya huyu bwana, lakini kilichonivutia zaidi ni kifo chake cha kusikitisha sana kutokana na ukatili wa hali ya juu uliotumika kumaliza maisha yake.

Ni nani huyu?

Miaka ya 1950, Muziki wa Kongo ulikuwa ukichukua sura na uelekeo mpya kabisa. Band za kisasa zilikuwa zikiibuka. Moja ya Band iliyokuwa ikivuma miaka hiyo ni Africa Jazz iliyokuwa chini ya Joseph Kabaselle.

OK-Jazz_in_Brussels,_1961-1.jpg

Band hii ilikuwa na wanamuziki wengi nyota kama Tabu Ley Rochereau. Akiwa kijana mdogo kabisa, Nico Kadanda pia alikuwa mpiga guitar wa band hii. Miaka ya 1960 mwanzoni band ya African Jazz ilifanya maonyesho makubwa kama kutumbuiza kwa Rais keita wa Mali na uwanja wa taifa hilo na maeneo mengine, lakini wanamuziki hawakuridhika na malipo waliyoyapata. Misusuko ya Band ilianzia hapa na hatimaye band hii kutawanyika kwa wanamuziki wengi kujitoa. Tabu Ley alijitoa na kina Dr Nico kasanda na kuanzisha band yao. Africa Fiesta. Ukisilizia nyimbo zao kama Ndaya Paradis,
Ukiiacha uzuri wa Sauti ya Ley, unasikia kitu chenye upekee. Guitar. Africa Fiesta ilikuwa na wapiga gitaa mahiri sana. Akiibeba sifa hiyo ni Nico Kasanda. Alipachikwa jina la Doctor, si kwa utabibu, bali ufundi wa kucharaza gita. Mimi binafsi licha kuwa sikuwepo duniani wakati huo, lakini nimesikiliza nyimbo kadhaa alizocheza magitaa, kwa kweli ni mmoja ya wapiga gita adimu ambao dunia ilishawahi kuwapata.

Screenshot_20211116-062747.png

Kama ilivyo kawaida ya Band zote duniani, migongano huwa haikosekani na hatimaye band hizi kuvunjika na Sababu huwa ni zile zile tatu; maslahi, wanawake au umaarufu. Kwa hapa ilikuwa ni maslahi. Mwaka 1965, mmoja ya wanaband waasisi wa Africa Fiesta, Robert Izeidi alikwena Ufaransa kutafuta deals za band yake. Aliporudi alikuta malalamiko ya Dr Nico kuwa, yeye Izeidi amekwenda nje ya nchi na kusaini mkataba na kampuni ya Muziki ya Kenya ya Associated Sound Limited, ASL nyimbo za band kama nyimbo zake binafsi. Dr Nico akitumia cheo chake cha Chef d'orchester (Afisa utumishi wa band) alitanganza kumfukuza Izeidi. Izeidi akijitetea kuwa yeye hausiki na lolote juu ya suala hilo la ASL na wao kama band wana mkataba na kampuni ya Congo Fonior kuuza kazi zao nje ya nchi. Izeidi aliamua kuangusha mbuyu; kwa hoja kuwa Africa Fiesta ina viongozi watatu, yeye, Dr Nico na Tabu na wana kura ya maamuzi, basi wanapiga kura na kumuondoa kundini Dr Nico. Na ikawa hivyo. Tabu Ley alibaki Afrisa Fiesta International na Dr Nico akaanzisha Band yake ya Africa Fiesta Sukisa mwaka 1966.

Eternel-Docteur-Nico--Merveilles-du-pass---1967--afrocharts-5f09fe7c8d8617d9cd7e38f-500x500.png

Katika kuisuka Band alisaka vipaji na hatimaye kuwanasa vijana wadogo wa miaka wawili, Valentine Sangana na Etienne Kazadi. Etienne Kazadi alikuwa mtanashati, aliyewavuruga warembo wa nyakati hizo (naweza sema mama zetu). Na hata jina lake la utani lilikuwa na maudhui ya kike, Chantal.

Changamoto kubwa ni kuzipata nyimbo zake mitandaoni. Binafsi nyingi nimezisikiliza TBC na Radio Congo.

moja ni hii hapa unaweza isikia sauti yake.

nyimbo nyingine unaweza isikia hii hapa, inaitwa Mbandaka (mji uliopo huko mto Kongo).

Katika dunia ya leo kwa wafuatiliaji wa muziki wa Dansi, unaweza mfananisha na Fally Ipupa alivyokuwa Quartier Latin kwa Koffi miaka ya 2000 mwanzoni. Katika sababu zile zile—maslahi—uliibuka mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki wa band ya Afrisa Sukisa na Boss wao, Dr Nico. Madai ya wanamuziki ilikuwa ni kuwa Dr Nico (yeye hakuwa muimbaji bali mpiga gita tu) kuwa anawalipa fedha kidogo na pia hata nyimbo wanazotunga wao, zote zimesajiliwa katika majina ya Dr Nico. Kwa mujibu wa Ethnomusicologist, Masoud Masoud wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) amethibitisha madai haya kuwa ni kweli.

Wanamuziki hawa walianza jitoa, na Chantal Kazadi naye alifukuzwa hasa kwa kudai uwazi wa mapato ya nyimbo zao akiwa na miaka 20. Katika kuondoka kwake huko, licha ya Dr Nico, kumsema vibaya kwenye mahojiano, yeye Chantal alikuwa akimshukuru kwa kumsajiri kwenye band yake, iliyompa jina na umaarufu na kumfunza muziki. Chantal Alienda anzisha band yake. [ Kwa mujibu wa jarida la The Monitor iliitwa Africa Soul].

Kifo Chake.

Mwaka 1971 Kazadi alitoka kwenye hotel yake katika mji wa Kananga ulioko Kasai, na kwenda barabarani kutafuta lift ya usafiri ili awahi kwenye onyesho lake—enzi hizo maisha ya wanamuziki hayakuwa professional, kama leo, au miaka ya 1990 (kwa huko Kongo).

Wakiwa njia, polisi wa doria walikamata gari hilo kwa madai kuwa kulikuwa na tukio la wizi na mauji ya mfanyabiashara wa madini na watuhumiwa ndio waliokuwa kwenye gari hilo. Polisi walichukua na kwenda nao 'chemba'. Kazadi aliteswa na kukatwa katwa mwili wake na kuwekwa kwenye mfuko, kisha kutupwa kwenye mto Lulua.

Dhana mbalimbali juu ya kifo chake.

i. Vyombo vya muziki.

Hii ni dhana iliyoenea sana kuwa Kazadi alishiriki kweli tukio hili la ujambazi, kwa lengo la kupata fedha ili apate vyombo vya muziki.

Dhana hii ilipingwa (na hata kwangu haina mantiki) kwa sababu kuu mbili, moja ni kuwa Chantal Kazadi toka wakati akiwa kwa Dr Nico, matajiri wengi walikuwa wakitaka kumfadhili ili aanzishe band yake, hivyo hakuwa na sababu ya kushiriki uhalifu ili apate vyombo wakati tayari alikuwa na fursa ya kuvipata 'bure'. Kimuziki huyu bwana alikuwa na mafanikio makubwa akiwa na Umri mdogo sana, kwani 1968 akiwa na miaka 17 tu, alipewa tunzo iliyoheshimika zaidi wakati huo, Tunzo za Wizara ya Sanaa ya nchini humo—kwa wakongo ni kama Grammy by then. Pili, walioineza dhana hii walikuwa ni 'Team Dr Nico', so ni dhana iliyosukumwa na chuki.

Hebu tujiulize, jinsi Harmonize alivyokuwa akihit akiwa WCB, na Maboss wengi walivyokuwa wakimtaka. Haingeleta mantiki yeye kushiriki ujambazi ili apate fedha za kuanzisha studio yake.

ii. Kuwa na watu wasio sahihi, sehemu isiyo sahihi na katika wakati usio sahihi.

Wapo wanaoamini—hasa wafanyakazi wa hoteli aliyokuwepo Kazadi kabla hajaondoka kwenda kwenye tamasha lake—kuwa, Kazadi alikumbwa tu na tukio hili na kujumuishwa kwenye ujambazi lakini yeye hakushiriki. Mji wa kananga [kwa mujibu wa wakongo ni mji wenye uhalifu mwingi sana unaochochewa na biashara za magendo ya madini—unaweza fananisha na Mererani hapa kwetu(si kwa uhalifu lakini😀).

Nature ya mauji yake, yalijaa ukatili, kiashirio kuwa wauaji walisukumwa na chuki dhidi ya muhanga wao na walimjua fika ni nani, ishara kuwa mauji haya yalisukumwa na chuki nyuma yake.

iii. Dr Nico yuko nyuma yake.

Alipokamatwa Chantal Kazadi, alijitetea kuwa yeye si jambazi na alikuwa akienda kufana tamasha na hata kujitetea kuwa ni mwanamuziki kwenye band ya Dr Nico. Askari mmoja alitumwa kwenda kwa Dr Nico ili kuthibitisha madai hayo, Taarifa iliyorudi ni kuwa Dr Nico hana muimbaji kama huyo na wala hamjui.

Dhana hii ina mashaka sehemu mbili; taarifa iliyorejeshwa na Polisi yule yawezekana ikawa imechakachuliwa na pili yawezekana Dr Nico alijibiwa kwa hasira pengine bila kujua Kazadi yuko kwenye mazingira gani.

iv. Wivu wa mapenzi.

Dhana yenye nguvu na inayo aminiwa na wengi ni ya wivu wa Mapenzi. Kazadi alikuwa ni kipenzi hasa cha wanawake. Yadaiwa [kwa mujibu wa mjomba wake Kazadi] kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa Jenerali Leopold Massiala. Alipokamatwa Kazadi, ilikuwa ni fursa adimu kwake.

Kwa mujibu wa wataalamu wa uchunguzi wa mauji, aina ya mauji huamua nini msukumo wa muuaji na hivyo kuamua muuaji ni nani. Kazadi alikamatwa kwa tuhuma za ujambazi, lakini aliuliwa kwa kukatwa katwa mwili, na kutupwa mtoni. Ishara kubwa kuwa muaji alisukumwa na chuki dhidi ya Kazadi. Mapenzi ni moja ya jambo ambalo hupelekea mauji ya kikatili. Lakini mimi binafsi nashindwa kushawishiwa na dhana hii kwa hoja ya nature ya mauji. Kwa sababu, waliokamtwa wote waliuawa katika mtindo mmoja.

Unaweza soma kwa kina kisa hiki kwenye kitabu cha Gilbert Aonga Ebolu L’Histoire de Chantal Kazadi (The Story of Chantal Kazadi) kipo Amazon (Amazon product ASIN 2754307052). Nimejaribu kutafuta toleo la Kiingereza sijapata, ila unaweza soma mapitio yake hapa (bookshelf )

Kwetu wadau, naomba neno lenu.

Cc: Safari_ni_Safari luambo makiadi mfianchi Mkereketwa_Huyu papag Mtu baki
 
Stori za muziki.

Kwenye album ya Titanic yake JB Mpiana ya mwaka 1997 na Band yake ya Wenge BCBG Les Anges Adorables; kuna wimbo uitwao Baracuda. Katika wimbo huu namba tatu kwenye album hiyo, dakika ya 3:20, JB Mpiana anataja maneno haya 'Afrika sukisa Chantal Kazadi'.

Unaweza usikiliza hapa [Procès Mambika-Boomplay Music]. Nilikuja yasikia tena maneno haya katika wimbo wa Koffi Olomide[siukumbuki ni wimbo gani]. Binafsi napenda sana kufuatilia historia katika muziki. Nilikuwa nikiifahamu—kwa kuisoma na kusikiliza nyimbo zake—band ya Afrika Sukisa ikiwa chini ha Dr Nico Kasanda. Swali kwangu lilikuwa ni nani hasa huyu Chantal Kazadi? Kutokana na vyanzo mbalimbali, nilivutiwa sana na historia ya kimuziki ya huyu bwana, lakini kilichonivutia zaidi ni kifo chake cha kusikitisha sana kutokana na ukatili wa hali ya juu uliotumika kumaliza maisha yake.

Ni nani huyu?

Miaka ya 1950, Muziki wa Kongo ulikuwa ukichukua sura na uelekeo mpya kabisa. Band za kisasa zilikuwa zikiibuka. Moja ya Band iliyokuwa ikivuma miaka hiyo ni Africa Jazz iliyokuwa chini ya Joseph Kabaselle.

View attachment 2012485
Band hii ilikuwa na wanamuziki wengi nyota kama Tabu Ley Rochereau. Akiwa kijana mdogo kabisa, Nico Kadanda pia alikuwa mpiga guitar wa band hii. Miaka ya 1960 mwanzoni band ya African Jazz ilifanya maonyesho makubwa kama kutumbuiza kwa Rais keita wa Mali na uwanja wa taifa hilo na maeneo mengine, lakini wanamuziki hawakuridhika na malipo waliyoyapata. Misusuko ya Band ilianzia hapa na hatimaye band hii kutawanyika kwa wanamuziki wengi kujitoa. Tabu Ley alijitoa na kina Dr Nico kasanda na kuanzisha band yao. Africa Fiesta. Ukisilizia nyimbo zao kama Ndaya Paradis,
Ukiiacha uzuri wa Sauti ya Ley, unasikia kitu chenye upekee. Guitar. Africa Fiesta ilikuwa na wapiga gitaa mahiri sana. Akiibeba sifa hiyo ni Nico Kasanda. Alipachikwa jina la Doctor, si kwa utabibu, bali ufundi wa kucharaza gita. Mimi binafsi licha kuwa sikuwepo duniani wakati huo, lakini nimesikiliza nyimbo kadhaa alizocheza magitaa, kwa kweli ni mmoja ya wapiga gita adimu ambao dunia ilishawahi kuwapata.

View attachment 2012486
Kama ilivyo kawaida ya Band zote duniani, migongano huwa haikosekani na hatimaye band hizi kuvunjika na Sababu huwa ni zile zile tatu; maslahi, wanawake au umaarufu. Kwa hapa ilikuwa ni maslahi. Mwaka 1965, mmoja ya wanaband waasisi wa Africa Fiesta, Robert Izeidi alikwena Ufaransa kutafuta deals za band yake. Aliporudi alikuta malalamiko ya Dr Nico kuwa, yeye Izeidi amekwenda nje ya nchi na kusaini mkataba na kampuni ya Muziki ya Kenya ya Associated Sound Limited, ASL nyimbo za band kama nyimbo zake binafsi. Dr Nico akitumia cheo chake cha Chef d'orchester (Afisa utumishi wa band) alitanganza kumfukuza Izeidi. Izeidi akijitetea kuwa yeye hausiki na lolote juu ya suala hilo la ASL na wao kama band wana mkataba na kampuni ya Congo Fonior kuuza kazi zao nje ya nchi. Izeidi aliamua kuangusha mbuyu; kwa hoja kuwa Africa Fiesta ina viongozi watatu, yeye, Dr Nico na Tabu na wana kura ya maamuzi, basi wanapiga kura na kumuondoa kundini Dr Nico. Na ikawa hivyo. Tabu Ley alibaki Afrisa Fiesta International na Dr Nico akaanzisha Band yake ya Africa Fiesta Sukisa mwaka 1966.

View attachment 2012494

Katika kuisuka Band alisaka vipaji na hatimaye kuwanasa vijana wadogo wa miaka wawili, Valentine Sangana na Etienne Kazadi. Etienne Kazadi alikuwa mtanashati, aliyewavuruga warembo wa nyakati hizo (naweza sema mama zetu). Na hata jina lake la utani lilikuwa na maudhui ya kike, Chantal.

Changamoto kubwa ni kuzipata nyimbo zake mitandaoni. Binafsi nyingi nimezisikiliza TBC na Radio Congo.

moja ni hii hapa unaweza isikia sauti yake.

nyimbo nyingine unaweza isikia hii hapa, inaitwa Mbandaka (mji uliopo huko mto Kongo).

Katika dunia ya leo kwa wafuatiliaji wa muziki wa Dansi, unaweza mfananisha na Fally Ipupa alivyokuwa Quartier Latin kwa Koffi miaka ya 2000 mwanzoni. Katika sababu zile zile—maslahi—uliibuka mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki wa band ya Afrisa Sukisa na Boss wao, Dr Nico. Madai ya wanamuziki ilikuwa ni kuwa Dr Nico (yeye hakuwa muimbaji bali mpiga gita tu) kuwa anawalipa fedha kidogo na pia hata nyimbo wanazotunga wao, zote zimesajiliwa katika majina ya Dr Nico. Kwa mujibu wa Ethnomusicologist, Masoud Masoud wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) amethibitisha madai haya kuwa ni kweli.

Wanamuziki hawa walianza jitoa, na Chantal Kazadi naye alifukuzwa hasa kwa kudai uwazi wa mapato ya nyimbo zao akiwa na miaka 20. Katika kuondoka kwake huko, licha ya Dr Nico, kumsema vibaya kwenye mahojiano, yeye Chantal alikuwa akimshukuru kwa kumsajiri kwenye band yake, iliyompa jina na umaarufu na kumfunza muziki. Chantal Alienda anzisha band yake. [ Kwa mujibu wa jarida la The Monitor iliitwa Africa Soul].

Kifo Chake.

Mwaka 1971 Kazadi alitoka kwenye hotel yake katika mji wa Kananga ulioko Kasai, na kwenda barabarani kutafuta lift ya usafiri ili awahi kwenye onyesho lake—enzi hizo maisha ya wanamuziki hayakuwa professional, kama leo, au miaka ya 1990 (kwa huko Kongo).

Wakiwa njia, polisi wa doria walikamata gari hilo kwa madai kuwa kulikuwa na tukio la wizi na mauji ya mfanyabiashara wa madini na watuhumiwa ndio waliokuwa kwenye gari hilo. Polisi walichukua na kwenda nao 'chemba'. Kazadi aliteswa na kukatwa katwa mwili wake na kuwekwa kwenye mfuko, kisha kutupwa kwenye mto Lulua.

Dhana mbalimbali juu ya kifo chake.

i. Vyombo vya muziki.

Hii ni dhana iliyoenea sana kuwa Kazadi alishiriki kweli tukio hili la ujambazi, kwa lengo la kupata fedha ili apate vyombo vya muziki.

Dhana hii ilipingwa (na hata kwangu haina mantiki) kwa sababu kuu mbili, moja ni kuwa Chantal Kazadi toka wakati akiwa kwa Dr Nico, matajiri wengi walikuwa wakitaka kumfadhili ili aanzishe band yake, hivyo hakuwa na sababu ya kushiriki uhalifu ili apate vyombo wakati tayari alikuwa na fursa ya kuvipata 'bure'. Kimuziki huyu bwana alikuwa na mafanikio makubwa akiwa na Umri mdogo sana, kwani 1968 akiwa na miaka 17 tu, alipewa tunzo iliyoheshimika zaidi wakati huo, Tunzo za Wizara ya Sanaa ya nchini humo—kwa wakongo ni kama Grammy by then. Pili, walioineza dhana hii walikuwa ni 'Team Dr Nico', so ni dhana iliyosukumwa na chuki.

Hebu tujiulize, jinsi Harmonize alivyokuwa akihit akiwa WCB, na Maboss wengi walivyokuwa wakimtaka. Haingeleta mantiki yeye kushiriki ujambazi ili apate fedha za kuanzisha studio yake.

ii. Kuwa na watu wasio sahihi, sehemu isiyo sahihi na katika wakati usio sahihi.

Wapo wanaoamini—hasa wafanyakazi wa hoteli aliyokuwepo Kazadi kabla hajaondoka kwenda kwenye tamasha lake—kuwa, Kazadi alikumbwa tu na tukio hili na kujumuishwa kwenye ujambazi lakini yeye hakushiriki. Mji wa kananga [kwa mujibu wa wakongo ni mji wenye uhalifu mwingi sana unaochochewa na biashara za magendo ya madini—unaweza fananisha na Mererani hapa kwetu(si kwa uhalifu lakini).

Nature ya mauji yake, yalijaa ukatili, kiashirio kuwa wauaji walisukumwa na chuki dhidi ya muhanga wao na walimjua fika ni nani, ishara kuwa mauji haya yalisukumwa na chuki nyuma yake.

iii. Dr Nico yuko nyuma yake.

Alipokamatwa Chantal Kazadi, alijitetea kuwa yeye si jambazi na alikuwa akienda kufana tamasha na hata kujitetea kuwa ni mwanamuziki kwenye band ya Dr Nico. Askari mmoja alitumwa kwenda kwa Dr Nico ili kuthibitisha madai hayo, Taarifa iliyorudi ni kuwa Dr Nico hana muimbaji kama huyo na wala hamjui.

Dhana hii ina mashaka sehemu mbili; taarifa iliyorejeshwa na Polisi yule yawezekana ikawa imechakachuliwa na pili yawezekana Dr Nico alijibiwa kwa hasira pengine bila kujua Kazadi yuko kwenye mazingira gani.

iv. Wivu wa mapenzi.

Dhana yenye nguvu na inayo aminiwa na wengi ni ya wivu wa Mapenzi. Kazadi alikuwa ni kipenzi hasa cha wanawake. Yadaiwa [kwa mujibu wa mjomba wake Kazadi] kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa Jenerali Leopold Massiala. Alipokamatwa Kazadi, ilikuwa ni fursa adimu kwake.

Kwa mujibu wa wataalamu wa uchunguzi wa mauji, aina ya mauji huamua nini msukumo wa muuaji na hivyo kuamua muuaji ni nani. Kazadi alikamatwa kwa tuhuma za ujambazi, lakini aliuliwa kwa kukatwa katwa mwili, na kutupwa mtoni. Ishara kubwa kuwa muaji alisukumwa na chuki dhidi ya Kazadi. Mapenzi ni moja ya jambo ambalo hupelekea mauji ya kikatili. Lakini mimi binafsi nashindwa kushawishiwa na dhana hii kwa hoja ya nature ya mauji. Kwa sababu, waliokamtwa wote waliuawa katika mtindo mmoja.

Unaweza soma kwa kina kisa hiki kwenye kitabu cha Gilbert Aonga Ebolu L’Histoire de Chantal Kazadi (The Story of Chantal Kazadi) kipo Amazon (Amazon product ASIN 2754307052). Nimejaribu kutafuta toleo la Kiingereza sijapata, ila unaweza soma mapitio yake hapa (bookshelf )

Kwetu wadau, naomba neno lenu.

Cc: Safari_ni_Safari luambo makiadi mfianchi Mkereketwa_Huyu papag Mtu baki
Mercie mingi brooo
 
Back
Top Bottom