Channel ten pamoja na kupewa sh 200mil na Rais Magufuli lakini bado picha na sauti ziko vilevile, why?

Nimesikitika kuona namna matangazo mubashara ya mkutano wa Waziri mkuu na wafanyabiashara wa jijini Dsm yalivyokosa ubora.
Picha zinachukuliwa upande mmoja tu, sauti haisikiki vizuri sanasana zinaonekana sare za kijani tu sasa sijajua kama hao nao ni wafanyabiashara.

Channel ten badilikeni bhana

Maendeleo hayana vyama!
Katika Chanel ya hivyo,hii inaongoza,picha chafu,sauti ya hovyo,watangazaji hata kiswahili kinawapa shida.
Wanaonesha hisia za ovyo wakiwa wanaongea na watazamaji.
Kuna mmoja juzi,ilikuwa ni kipindi kinazungumzia lishe bora,akipokea simu asipokupata vzr,anaikata kwa hasira kama vile anakukumoa,mpaka mwenzie,kama sikosei anaitwa Albert akamwambia,amwambie msikikizaji apige tena.
Leo nimemuona tena wakati anarusha breaking news ya kuungua kwa kiwanda cha Bora,anakuwa kila muda anajiweka/anajishikashika shati kujiweka sawa utafikiri anapiga picha studio,wanataka kuongea kwa mbwembwe wakati hana mvuto,anafanya "show off" ili watu wamuone.
Sura lenyewe baya,limetokeza mbele kama boneti ya cruzer,anataka aonekane handsome boy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani TBC baada ya kufunga mitambo ya kisasa imebadilika?
Kila kitu kikiguswa na CCM kinaharibika!
TBC1 hakuna kitu kabisa,bora wakati Hassan Marin,anatangaza au kufanya mahojiano,alikuwa analeta vionjo.
Kuna mtangazaji wao,anasauti baya la kukwaruza,ndie wanamtumia sana kwenye matamasha yanayo kwenda mubashara,au kufanya mahojiano.
Sura yake imebondeka kama mlevi,
Watangazaji wanawake,wanavaa minguo ya ovyo,ligauni likubwa kama BURQA wanazovaa wanawake kule Afghanistan,jifunzeni Azam jinsi ya kupangilia muhonekano wa studio,na kuvaa,ajiri watu wenye weredi.
Ukienda ITV kwenye kipimajoto,ukimsikiliza Kambaya,anamuhoji mshiriki,utafikiri anabishana nae,baada ya kumuuliza maswali yatakayo leta elimu kwa umma,aanamuuliza kwa ubishi ili ashinde mjadala tu,yaani ni ovyo kabisa.
Jirekebisheni.Jifunzeni kupitia Chanel za Kenya.
Dotto burendu,Ivona,,walipokuwa Startv,ilikuwa poa
sana,sasa HV ni madudu matupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesikitika kuona namna matangazo mubashara ya mkutano wa Waziri mkuu na wafanyabiashara wa jijini Dsm yalivyokosa ubora.
Picha zinachukuliwa upande mmoja tu, sauti haisikiki vizuri sanasana zinaonekana sare za kijani tu sasa sijajua kama hao nao ni wafanyabiashara.

Channel ten badilikeni bhana

Maendeleo hayana vyama!
Kitu chochote ukishakihusisha na ccm maana yake unakiuwa kifo cha kikatiri sana ! mifano ni mingi mno , TBC 1 , TOT , SUKITA , GAZETI LA UHURU , REDIO UHURU NK
 
200 MIL,loo ni fedha nyingi mno ILA ni FEDHA ambayo imetoka kwenye mfuko wake binafsi au ni fedha ya watanzania wote?je Bunge liliidhinisha hizi fedha ili zitolewe?na hii station inawajibika kwa nani ili kuleta mrejesho wa matumizi yake?,ninapopata muda ninasoma na kufuatilia yanayotokea pale Africa ya Kusini kuhusu tume ya STATE CAPTURE,NINAOMBA nayo hii ije kutokea hapa nchini in my life time,mengi yatatushangaza from CHAVDAS TO LADWAS etc etc
Ile dhana ya kupunguza matumizi ya serikali. Bila kujali sheria za matumizi ya fedha za umma sivioni kuleta welfare kwa watanzania zaidi ya kujenga madaraja ya kinyonyaji.

Wale wa juu kutumia fedha za umma vibaya wakati wa chini wakusanyaji hata kunusa hawaruhusiwi.

Mwisho itajenga hujuma zaidi kuliko uzalendo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilipokuwa ingeweza badilika kwa namna chanya,ila ilipo sasa ndio itabadilika kwa namna hasi kabisa.
Muda ni msemaji mzuri,utatuambia.
Nimesikitika kuona namna matangazo mubashara ya mkutano wa Waziri mkuu na wafanyabiashara wa jijini Dsm yalivyokosa ubora.
Picha zinachukuliwa upande mmoja tu, sauti haisikiki vizuri sanasana zinaonekana sare za kijani tu sasa sijajua kama hao nao ni wafanyabiashara.

Channel ten badilikeni bhana

Maendeleo hayana vyama!

Loyalty To country Alyways,To government When it deserves
 
Back
Top Bottom