Channel Ten na CCM zazindua matangazo ya kumchafua Dr. Slaa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Channel Ten na CCM zazindua matangazo ya kumchafua Dr. Slaa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,797
  Trophy Points: 280
  Leo jioni channel Ten na CCM wamezindua matangazo ya kumnadi JK huku wakichakachua aliyoyasema Dr. Slaa katika kampeni zake.

  Jk anaonekana mikutano yake ya mijini mahudhurio watu wamejaa na huku mkutano ya Dr. Slaa kijijini hauna watu kabisa.

  Jk akisindikizwa na muziki wa kizazi kipya anaonekana mambo ni shwari lakini huku kwa Dr. Slaa yuko kijijini ambako hata watu ni wachache..

  Dr. Slaa anaonekana akitoa ahadi za kufuta kodi ili elimu na afya ziwe bure na mmoja wa mhudhuria mkutano huo ambaye yupo karibu na mtu mwenye gwanda la Chadema ambaye haonekani usoni ikithibisha ya kuwa ni picha za kuchakachuliwa tu alimwuliza swali hivi shughuli za uendeshaji wa serikali zitaendeleaje huku hakuna kodi ambayo inakusanywa.......Tangazo hili halimpi Dr. Slaa nafasi ya kujibu bali anasisitiza tu elimu na afya ndiyo vitakuwa bure ikionyesha ya kuwa hakuna uhusiano wowote ule na swali lililoulizwa....

  Tangazo hilo linakwisha kwa kudai hayo yote yalikwisha kujaribiwa na yalishindikana......ikimaanisha ya kuwa huko nyuma serikali iliacha kukusanya kodi lakini iliendelea kutoa huduma za jamii bure na wakashindwa kuendesha serikali jambo ambalo siyo kweli.............................

  Tatizo hapa ni kuwa mmiliki wa tangazo hili hajulikani. Kiutaratibu ni haki ya wateja wa Channel Ten kujua ni nani anayegharimia tangazo hili na kwa kiasi gani ana ubia na CCM ili kuwapa nafasi wapigakura waamue wamwamini vipi na wafahamu fedha za tangazo hilo zinatoka wapi........

  Kwenye nchi zilizoendelea mmiliki wa tangazo kuonyesha uaminifu wake kwa wasikilizaji hujitokeza na kusema mimi ninaafiki tangazo hili.

  Si Channel Ten au CCM ambao wapo tayari kujitokeza hadharani na kujimilikisha tangazo hilo kwa sababu limejaa madudu na linamshushia heshima yule aliyelibuni kwa sababu halisemi ukweli..........mahudhurio yote ya Dr. Slaa hakuna mahali ambapo yamekuwa kiduchu kama kwenye picha hizo.......Na hakuna mahali ambapo Dr. Slaa ameahidi kufuta kodi zote......hivyo tangazo hili linasema uongo........

  Chama cho chote ambacho kitataka kuingia madarakani kwa njia ya kuchakachua hata ujumbe wa kampeni za wenziwe hakina uadilifu hata chembe na hakifai kuaminiwa na wapigakura kuliongoza taifa hili.

  CCM na Channel Ten wanapaswa wajisafishe kwa kuueleza umma wa watanzania ni nani aliyecheza mchezo mchafu huu na fedha alizozitumia zinatoka wapi........vinginevyo NEC ina haki ya kulifuatilia suala hili pamoja na msajili wa vyama vya siasa...........ili kulinda utu wa mtanzania ambao una maadili yanayoeleweka ya kuheshimiana...........siyo kutungiana uongo

  SOURCE: CHANNEL TEN LEO JIONI
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nimeiona leo live nkashangaa CCM wamekuwa vioja!
   
 3. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  hata mimi nimeliona na nimestuka na hawa chanel ten
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  kwa kweli jambo hili hata mimi mwana CCM damu sikulipenda hili tangazo, linakiuka misingi ya kidemokrasia na tena linaweza kuhatarisha hali ya amani, nafanya mawasiliano na viongozi kujua kama CCM inahusika waliondoe.
   
 5. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Unashtuka leo kuhusu Channel 10? Hujui kama fisadi Manji ana mkono hapo.
   
 6. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hiyo chanel mpaka wenye ungo ndo wanaiona nje ya Dar, so wanajifurahisha. tunataka majibu ya mambo magumu kama suala ya matibau na watoto wetu kusoma, pia tunataka kujua anavyowashugulikie wezi wa kozi zetu na namna tunavyoweza kujenga nyumba bora. bila hayo bado kazi ipo!
   
 7. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Kuna kampeni na propaganda ambazo badala ya kumfanya mhusika shujaa/valliant linamfanya coward/enemy. Inaonesha ni jinsi gani kipofu na kipofu wanavyoongozana huku kila mmoja akidai kuiona njia sahihi zaidi ya mwenzie.
   
 8. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hiyo chanel tunajua ya Manji, hayo matangazo hayawezi kuuficha ukweli wa matatizo tuliyonayo vijijini kama vile ukosefu wa nyumba bora, elimu na miundombinu ya kilimo, kwanza hiyo chanel mnaiona nyiye wa mjini huku ushagoo mpaka wenye madishi kwa hiyo kazi bado ipo. Hajajibu hoja ya kuwapigia debe watuhumiwa wa matumizi mabaya ya kodi zetu
   
 9. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  I used to think that you were a big pain in the neck. Now I have a much lower opinion of you.
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata kama wangechakachua vipi, hata kama wakipaka matope, wananchi wameshafanya maamuzi. Jioni hii nilikuwa naongea na wamachinga kwenye foleni wanasema mbona j2 mbali hivyo? Wamechoka wamepigika
   
 11. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hata swali walilouliza hapa kwa mgombea la kisenge tu
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Kilichonishangaza ni pale alipokua akiongea Sumaye akiwa katika jimbo la SLAA huku wakionyesha picha za sehemu nyingine??? ujinga mwingine bwana
   
 13. majata

  majata JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Kwa hali ya channel ten na matangazo ya uchafuzi wa wenzao namna hiyo sitashangaa nikiona uvunjifu wa amani ukitokea kwakuwa inaonekana hatuna serikali kabisa Tanzania ila tunavibaraka tu wa Mkwere wasio jua kitu na hatari za uongo wakuwadanganya watanzania.
   
 14. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mtoto wa Oysterbay nimekukubali kwa hilo...
   
 15. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yana mwisho haya :......::.......:
  Jumatatu mtu hana kazi !!!
   
 16. K

  KICHAPO Member

  #16
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sisi wataalamu wa computer tunasema wameADOBELISE.Hawana jipya ndio wamemjenga DR.wa ukweli.Si huyo wao wa kichina
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  sasa hivi shekh Mohamed na Gamanywa wanagombeza udini Star TV wanaweka picha za mikutano ya CHADEMA propaganda ambayo itawarudia wenyewe Gamanywa sijui wakristo gani wanaomuheshimu hata sielewi katokea wapi kupe mkubwa
   
 18. K

  KICHAPO Member

  #18
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maji ya utosi usije ukashangaa kusikia JK AMEKUFA kesho,pressure inapanda na kushuka hata kile kiti kwenye mdahalo alikuwa anahangaika nadhani haja ilikuwa inataka kumtoka.
   
 19. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Ni hayo tu, wenyewe mtaongeza
   
 20. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wamechanganyikiwa. Iweje JK anajitangaza kupitia Dr. Slaa na wala si Lipumba au wengineo??? Wamefulia.

  Mwaka 2010, ......... HATUDANGANYIKI
   
Loading...