Channel ten: Kipindi cha 'Je, tutafika' Makwaia unaboa!

Nali

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
1,155
812
Kipindi cha "Je tutafika" kinachorushwa na Channel Ten na kuongozwa na Mzee Makwaia, ni kizuri sana sema tu Mwongozaji/mtangazaji Makwaia anaboa mno kwa kumwingilia mzungumzaji wakati ana flow mpka anampotezea hoja na points zake!

Pia ana uliza maswali mareeeeeeeeeeeeeefu mwisho kipindi kinaonekana kama yeye ndio mzungumzaji then anapomruhusu mhusika kuongea ghafla anamwingilia tena!!! Dah!! sijui ni uzee?

Badilika taf!!!
 
Ni kweli,huyu mzee ni much know kwa hiyo anasababisha mvuto wa kipindi kupotea..mbona mwenzake Adam Simbeye wa This week in Perceptive yuko njema,na Hamza Kasongo kwenye Kasongo Hour wako njema?
 
Jamani mimi nilidhani anani bore peke yangu tangu alipoanza kujiuza katika TV nilishaachana naye siku nyingi kumbe bado anaendelea na kipindi chake.

Nadhani huyu Mzee kule mtaani kwake ni mjumbe wa nyumba kumi anadhani watu wameleta mashtaka. Makwaia unaowaalika hawapendi kualikwa tena kwa sababu ya kuwaingilia wanapo flow. Jirekebishe Bw.
 
Huyu mzee huwa anachapa ulabu wa kueleweka kabla ya kuongoza hicho kipindi chake
 
Anakuwa tayari ana malengo yamuelekeo wa kipindi chake, kwa hivo anavutia maneno anayoyata yasemwe na yale asiyoyataka anayaingilia kuyapotezea.

kwa maana nyingine yeye ndiye muulizaji na hapohapo ndiye anayetoa majibu. Wageni wake ni kanyaboya tu.
 
Ni king'ng'anizi huyo,mie nilishamchoka ,ile kuna siku alipata shida kwa Dr slaa,alimzibiti vilivyo aliacha mambo yake ,inatengemea na mtu anayemkaribisha kama ni boya mtasikia yeye ndo anaongea na anapendekeza,anatakiwa kupata watu wanaomsoma kabla hawajachangia ili umepinge rungu kubwa mpaka ajione wa kuja kwenye tansinia hii ya habari.
 
Kwani hicho kipindi kina any commercial sponsor? Kama kuna kampuni inadhamini basi haipati any business return.

Mimi nilishaacha kukiangalia na kusoma makala zake kwenye Daily News
 
Kwani hicho kipindi kina any commercial sponsor? Kama kuna kampuni inadhamini basi haipati any business return. Mimi nilishaacha kukiangalia na kusoma makala zake kwenye Daily News

Hakina mdhamini yeyote, kwa hiyo hakizalishi hata thumni! Nani atawekeza kudhamini kipindi kisicho na watazamaji?

Sijui watazamaji wake wanapata faida gani. Wakati kinaanza nilikuwa mfuatiliaji wake sana lakini ni miaka miwili sasa, wala sioni kuki-misi.
 
Amekaa kama mchekeshaji wa kicomedy. Ni mbinafsi sana kwa kweli hapendi mawazo ya wengine ya prevail. Inaonekana hata Channel 10 haina market basi.

How come do you keep mzee Makwaiya for more than 5 years kwenye prime time akiwa anatema vepa tu pale?
 
Kipindi cha "Je tutafika" kinachorushwa na Channel Ten na kuongozwa na Mzee Makwaia, ni kizuri sana sema tu Mwongozaji/mtangazaji Makwaia anaboa mno kwa kumwingilia mzungumzaji wakati ana flow mpka anampotezea hoja na points zake!! Pia ana uliza maswali mareeeeeeeeeeeeeefu mwisho kipindi kinaonekana kama yeye ndio mzungumzaji then anapomruhusu mhusika kuongea ghafla anamwingilia tena!!! Dah!! sijui ni uzee??? Badilika taf!!!
Wauza sura kwenye luninga ni wengi...lakini watangazaji wanaoijua fani ni wachache..tutafika tu!
 
Inawezekana Makwaiya ni muandishi mzuri magazetini lakini hana uwezo wa kuhost vipindi vya namna hiyo katika televisheni, kipindi chake kinaboa sana.
 
Back
Top Bottom