Channel 10 wametishwa na serikali kuhusu kipindi maalumu cha Mwangosi

Channel 10 siku kadhaa zilizopita walitangaza kwamba siku ya jumamosi ambayo ni leo majira ya saa 2 usiku watakuwa na kipindi maalumu kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Iringa, ajabu mida hii wanaonyesha kipindi cha bongo fleva hapa sijui inamaanisha nini tena au SERIKALI IMEWAPIGA MKWARA?

Wakuu hicho kipindi kitarushwa kesho Jumapili kuanzia saa 2:3o usiku na sio Jumamosi kama ambavyo ilikuwa imesemwa hapo awali.Poleni sana kwa usumbufu Hamza Kasongo Hour ni Jumapili na sio Jumamosi.
 
Wakuu hicho kipindi kitarushwa kesho Jumapili kuanzia saa 2:3o usiku na sio Jumamosi kama ambavyo ilikuwa imesemwa hapo awali.Poleni sana kwa usumbufu Hamza Kasongo Hour ni Jumapili na sio Jumamosi.

Asante mkuu
 
Walitangaza kwa msisitizo kwamba tusikose kipindi maalumu siku ya jumamosi saa 2 hivyo vyote nimeviona na kwa jinsi walivyokinadi hicho kipindi maalumu watu walitegemea kuna mambo mengi mazito ambayo hayawa covered, kuwasha TV ndio hivyo tena bongo fleva na kutoka zanzibar

Labda ni jumamosi ijayo kwani walitaja ni jumamosi tarehe 08/09/2012?:bange::bange:
 
Labda ni jumamosi ijayo kwani walitaja ni jumamosi tarehe 08/09/2012?:bange::bange:

Ndio ukienda ofisi zinazofanya mambo kwa uhakika huwa wanatumia tarehe badala ya kutaja siku ila kuna mdau amesema kitarushwa leo jumapili tarehe 9 saa 2 na nusu usiku kwani kipindi Hamza Kasongo ni jumapili na si jumamosi kama walivyotangaza
 
Nilichoona mimi kwenye youtube ambayo link ilitolewa na mwana JF, ni mazungumzo kati ya Hamza Kassongo na jamaa wawili ambao majina siyakumbuki tena! Kabla hawajaanza mjadala, waliweka "clip" ya mwandishi yule aliyekuwa anafuatiliwa kwa ukaribu na polisi kutoka kule Nyololo. Hata hivyo, sikuweza kudownload kwasababu PC zetu internet speed ni ndogo.(kuangalia tu inabidi uibembeleze iwe inafanya "buffering)
 
Jamani mm nimechelewa kuna waliosema leo Jumapili saa 2:30 usiku kutakuweko na Kipindi maalum licha ya ile YouTube tuliyotuma hapa JF
Leo je maana hapa Channel 10 ipo Filamu tu
 
Nilichoona mimi kwenye youtube ambayo link ilitolewa na mwana JF, ni mazungumzo kati ya Hamza Kassongo na jamaa wawili ambao majina siyakumbuki tena! Kabla hawajaanza mjadala, waliweka "clip" ya mwandishi yule aliyekuwa anafuatiliwa kwa ukaribu na polisi kutoka kule Nyololo. Hata hivyo, sikuweza kudownload kwasababu PC zetu internet speed ni ndogo.(kuangalia tu inabidi uibembeleze iwe inafanya "buffering)

Mbona kwenye youtube nilisikia watu wakipiga simu ina maana kile kipindi kilishaenda hewani tayari
 
Mbona kwenye youtube nilisikia watu wakipiga simu ina maana kile kipindi kilishaenda hewani tayari
Maajabu leo saa 3:15 Hamza Kassongo anamhoji Mzindakaya wakati nishuhudia mwandishi km sikosei Godwin akijieleza ktk tangazo hilo nimeamini wamebanwa kurusha hizo Documentary ila ktk Taarifa ya TBC saa hizi yupo Waziri NCHIMBI akiikosoa JAMII FORUM wakati akijibu maswali matatu la msg ya Dr Slaa kwnda kwa IGP
 
hawa jamaa wamemsaliti mfanyakazi mwenzao kwa degree ya hali ya juu sana, laana na iwe juu yao kwa kukubali kununuliwa kwa bei poa
 
Yaani kitendo hicho kinazidi hata Yale masikitiko ya wale watu Wa kwenye tangazo la Airtel kwamba 'WAMEKATA' yaani mtu unaisubiri habari kwa hamu watu wanakata! Very unfair!
 
kawaida ya television station zetu hazipendi kukwaruzana na serikali ,sijui kama watarusha hicho kipindi huenda wakasema kinahatarisha usalama wa nchi tusubiri tuone....

sio hazipendi, ni waoga wanawaza kazi zao na uhai wao.maana siku hizi ukienda kinyume tu na matakwa yao utaambiwa mchochezi au wewe CDM. kama hautafukuzwa kazi unaweza ukapotea au wakakulimboka.
 
Back
Top Bottom