Channel 10, Nani anamiliki?

Du Channel 10 siku hizi haikamati kwenye dish langu. Au ndo imeshauzwa na inakarabatiwa?? Mhhhhhhhhhhhh, mambo hayo.
 
Mhh Jamani yamekuwa hayo tena Tanil Somaiya (Shivacom, Ultimate Security, Radar, Umoja wa Vijana TZS 400,000,000/=) kachukua na Channel 10 tena. Mhh 2010 hiyo karibu na mambo yanabadilika katika mission na vision ya tv kuendana na mmiliki mpya. Patamu hapo!
 
Atanunua kila kitu kwa vile iko pesa aliyoipata kwa ubwete. Kelele zikizidi ananunua na Muhimbili ili adhibiti hata matibabu ya wale wenye kuchonga sana juu yake.
Hivi kazi inapatikana vipi hapo? Asaa kheri tunaweza tukatengeneza senti.
 
Sasa wafanyeje? Pesa ya bureeeee, tena bure wanayo, We mtu mkuu wa nchi anakwambia nenda kakwapue 40bn. Uzigawe kama njugu ili chama kishinde, hapo hazina mkaguzi, wala muhazini, sasa hata ukiwagawia 5bn ukawaambia zimeisha nani wakukuhoji?

Ndio maana wakiamua wata tununua hata sisi na ka nchi ketu mwe!
 
Nawashangaa watanzania wenzangu, kumbe Somaia na Rostam ndo vodacom, sasa bado tunashupalia vodacom, eti tigo ni mtandao wa wanafunzi! Tuachane na vodacom kwani tunazidi kuwatajirisha hawa washenzi
 
nadhani bado vyombo vingi vya habari vitaendelea kununuliwa tukielekea 2010

...labda ndio maana 'mkuu' anaanza kutapatapa, watanzania wenye asili ya kiasia wameamua kushindana naye kibiashara, waliwanunua ze komedi, sasa wananunua TV stations na magazeti..., au?
 
Kama ni RA na Tamil amenunua Channel 10 ni dhahiri sasa kwa nini RM awaite mafisadi. Huyu mzee mwoga sana wa ushindani. Wananchi angalieni msijiingize kwenye vita vya tembo
 
Kama ni RA na Tamil amenunua Chanel 10 ni dhahiri sasa kwa nini RM awaite mafisadi. Huyu mzee mwoga sana wa ushindani. Wananchi angalieni msijiingize kwenye vita vya tembo

Ni rahisi kumwelewa rm na kuwa upande wake. Ni vigumu kuwaelewa hao kina ra na somaia na kuwa upande wao.

Rm anasema hao jamaa wametuibia/wametuchukulia kilicho chetu kilichokuwa kitumike kujenga hospitali, shule na barabara zetu. Jamaa wananyamaza au wanasema oh, rm ana wivu na kashindwa kuendesha biashara zake na maneno kama hayo. Hawatoi utetezi au maelezo ya maana kwa uchafu unaosemwa juu yao.

Wakati huohuo hatusikii alipokomba rm. Sasa mtu wa kawaida kama mie nimwamini nani? Labda wataitumia channel 10 mpya kutuelezea tukawaelewa kuwa hawakuchukua kilicho chetu
 
Atanunua kila kitu kwa vile iko pesa aliyoipata kwa ubwete. Kelele zikizidi ananunua na Muhimbili ili adhibiti hata matibabu ya wale wenye kuchonga sana juu yake.

Mkuu, Hii ni kubwa kuliko! Thanx. Leo kulikuwa na mawingu lakini you have made my day! :D
 
Kitila,
Not only CCM tutelage, but the fisadi wing of CCM. Tumekwisha!

Aminia, its all making sense now, mwache mengi abanane nao before its too late.."project wash epa money" is almost complete. After 2010 there will be no traces.
 
Back
Top Bottom