Channel 10 hongereni kwa Taarifa zenu, lakini boresheni TV yenu na uvaaji

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,314
IMG_20170315_074222_240.JPG

Tunapoangalia habari au kipindi flan tunaangalia mambo mengi. Moja wapo pia ni namna msomaji anavyosoma uchaguzi wa maneno na uvaaji ni muhimu sana. Na ndo maaana wenzetu huwa wanahakikisha mtangazaji amevaa vizuri kabisa akapendeza ndo anaenda kusoma taarifa ya habari. Kuna aina ya uvaaji unapoteza credibility kabisa. Ukimtizama tu mtangazaji unakata tamaa na kuhisi pengine hata taarifa anayoitoa pia si makini.

Hebu mwangalie mtangazaj huyo wa channel 10 uvaaji wake wa kachumbali na shati lake la bei chee kabisa na tai. Mwangalie hata kola ya shati ilivyokaa. Angalia aina ya shati na tai yake. Unaishiwa nguvu kabisa. Kwa nini avae hovyo hivi?
 
View attachment 481072

Kiufundi na Kiutaalamu Kibwana Dachi hafai na hatoshei kuwa Mtangazaji wa tv hata kama atafundishwa mara 10000 kwani hana tv Personality ila anafaa sana kuwa Mtangazaji tu wa Radio au kuwa mpiga picha au program producer na mtafuta Habari ( msaka nyoka ) na kwa muda mrefu hata katika baadhi ya posts zangu nimekuwa nikilisemea hili ila kama kawaida sikio la kufa halisikii dawa.

Matatizo makubwa la Channel Ten ni :

  1. Management ya hovyo hovyo.
  2. Wanaajiri Ki hovyo hovyo.
  3. Mahaba na Upendeleo Kazini vimeshika kasi.
  4. Budget ndogo inayoratibiwa na Ubahili wa Media owner wao.
  5. Low level of Professionalism kwa 95% ya Watangazaji wake.
  6. Ni watimiza wajibu zaidi na si washindani katika Tasnia.
  7. Waoga wa Kuthubutu kama wenzao kitu ambacho kinawaathiri kila uchao.
Tanzania tukiwa na Media outlets Kumi ( 10 ) kama Azam tv itapendeza sana japo kwa kiasi fulani hata hao Azam tv nao wana mapungufu kadhaa ila siyo mengi na yanarekebishika endapo na Wao watakubali kukosolewa.

Nimalizie tu kwa kusema Mkuu kuwa kwa tunaojua maisha halisi ya hapo Africa Media Group ambapo Channel Ten ni mmoja wa Mtoto wao wala hatushangai kumwona Kibwana Dachi anavaa hivyo. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
kwani lengo na focus yako ni kuangalia news,habari au unaangalia mavazi ya mtangazaji.
Hiyo ni taarifa ya habari masuala ya uvaaji angalia fashion TV

Umejibu kipuuzi mno kwani Kiueledi kabisa Mleta uzi ana hoja tena ya kimsingi sana. Ungekuwa hata angalau una a,b,c's za Journalism wala usingepovuka na kutokota hivi. Kwa kukusaidia tu ni kwamba audience psychology hasa ya tv Viewers hulenga mambo yafuatayo :
  1. How presentable you're ( uwasilishaji wako na mwonekano wako mzima )
  2. Marvelous in articulation ( uzungumzaji wako kiusahihi na kiufasaha kabisa )
  3. Confidence and Controlling level ( uwezo wako wa kujiamini na kutawala eneo / meza )
Kila la kheri.
 
Dah hawa jamaa huwa wananifurahisha sana, hawabadiliki na ukikutana na yule jamaa wa kibonzo cha Mwagito ndio basi tena!!!!!
 
Back
Top Bottom