kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,816
- 17,405
Chanjo ya Iran ya COVID-19 inaweza kukabiliana na 'kirusi cha Uingereza'
Jan 30, 2021 12:16 UTC
Chanjo ya Iran ya COVID-19 au corona ambayo majaribio yake yanakaribia kumalizika ina uwezo wa kukabiliana na aina mpya ya kirusi cha corona ambacho kimeibuka Uingereza.
Hayo yamedokezwa na Dkt. Hassan Jalili mkuu wa timu ya utengenezaji chanjo ya Iran katika Idara ya Utafiti ya Taasisi ya Utekelezaji wa Maagizo ya Imam Khomeini (MA).
Itakumbukwa kuwa mnamo Disemba 29 mwaka 2020 chanjo ya corona iliyotengenezwa na shirika la Barakat la Iran ilifanyiwa majaribio kwa mwanadamu. Chanjo hiyo ambayo inajulikana kama COVIRAN Barekat imetengenezwa na Shirika la Barakati ambalo liko chini ya Idara ya Utafiti ya Taasisi ya Utekelezaji wa Maagizo ya Imam Khomeini (MA).
Akizungumza na Shirika la Habari la Tasnim, Dkt. Jalili amesema majaribio yaliyofanywa yanaonyesha kuwa plasma ya damu ya watu waliodungwa chanjo ya COVIRAN Barekat wakati wa majaribio, inaweza kusambaratisha kabisa aina mpya ya kirusi cha COVID-19 kutoka Uingereza.
Mbali na chanjo ya COVIRAN Barekat iliyoundwa Iran kikamilifu, Iran iko mbioni kutengeneza chanjo zingine za corona ndani ya nchi na pia kwa ushirikiano na washirika wa kigeni. Aidha Iran pia itaagiza baadhi ya chanjo zake za corona kutoka nje ya nchi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuingizwa Iran chanjo kutoka Marekani na Uingereza ni marufuku lakini ameruhusu kuagizwa chanjo kutoka nchi zingine zenye kuaminika.
Tayari Iran imeshatangaza mpango wa kununua chanjo ya corona ya Russia inayojulikana kama Sputnik V.