#COVID19 Chanjo ya COVID-19: Tuchague kusuka ama kunyoa

MenukaJr

Member
Apr 24, 2021
50
128
Serikali kusema uongo ni kosa. Kamati inayoundwa na Rais wa nchi nzima kusema uongo ni kosa zaidi. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa kusema uongo au kupumbaza watu. Chanjo ya korona, tuchague moja. Kusuka ama kunyoa!! Kama haina madhara, ni ya ufanisi kama ilivyopendekezwa na Kamati tuichukue. Kama ni ya bahati nasibu, bado kuthibitika vizuri ubora wake tungoje ithibitike na kama ni batiri, biashara ya watu isiyo na manufaa wala msaada kwa watu tuikatae. Hakuna hiari katika chanjo yenye kuhusika na janga la nchi nzima. Kama nchi yetu ipo katika matatizo ya korona chanjo ni lazima hakuna shortcut, kama nchi yetu ni salama chanjo haina maana yoyote. Tuachane nayo, tuchague kusuka ama kunyoa!

Serikali iseme ukweli iache kusema uongo. Serikali kudanganya watu ni tabia mbaya, iseme ukweli kama nchi yetu inakabiliwa na tatizo lenye kuhitaji chanjo au nchi haina tatizo. Serikali iseme ukweli ikiwa chanjo inayohitajika ina manufaa kwa watu kwa kuthibitishwa na vyombo vyetu wenyewe au haina manufaa ni bahati nasibu. Nchi hii ni huru, inapaswa kujiamulia mambo yake kwa uhuru bila kuogopa au kufuata mkumbo. Serikali ndiyo yenye wajibu wa kulinda usalama na afya za watu wake isiweke hiari katika mambo ya msingi kama afya.

Tujiulize, itakuaje ikiwa nchi ipo katika matatizo makubwa halafu watu wakagoma kuchanja kwa kukosa elimu sahihi na kwa sababu ni hiari. Maana yake nchi inaweza kufa yote na Serikali ipo. Kwa uzembe huu, Serikali itakua umeua watu wake kwa kushindwa kusimamia ukweli. Hatuwezi kuwa na Serikali ya namna hiyo, ni lazima Serikali isimamie usalama wa watu kwa nguvu zote.

Tujiulize tena, itakuaje ikiwa ni kweli chanjo hazina faida, ni hatari kwa watu halafu nchi nzima ikachanja kwa sababu ya hofu, hiari na haraka ya kuchukua tahadhari. Maana yake, nchi nzima itakua imeangamia kwa uzembe wa Serikali. Kwanini tunaweka hiari katika jambo lenye kuhusu maisha ya watu wote katika nchi. Hiari maana yake nini, kwamba mtu akitaka sawa asipotaka sawa. Kwa kawaida jambo lenye kutegemea utashi wa mtu huwa si la lazima, si la mhimu wala lenye maana. Kwanini Serikali inaiingiza nchi katika mambo ya bahati na nasibu, yasiyo ya lazima, mhimu wala maana. Kwenye jambo linalohusu maisha ya watu, hakuna hiari.

Hatuwezi kuweka hiari kwenye uhai wa watu aktika nchi nzima. Haiwezekani!! Chanjo ya Polio ina manufaa, imethibitika ndio maana sio hiari. Kila mtoto anachanja kwa sababu inahusu tatizo la kitaifa. Kwanini korona inafanywa hiari, hakuna hiari katika usalama wa watu. Serikali iache uongo, kuna mtu anadanganywa hapa. Ama Kamati imemdanganya Rais au Rais anawadanganya wananchi.

Kamati ya Rais kwa tathmini ya korona imesema chanjo ni hiari, Rais Mwinyi kwa ajili ya Zanzibar amesema chanjo ni hiari. Mtiririko huu unaonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano atapita humohumo (japo amewahi kugusia) kuwa chanjo ni hiari. Kwa ajili ya Tanganyika, tunamshauri Rais wa JMT achague kusuka ama kunyoa. Aachane na mzaha huu, hakuna hiari katika jambo la maana linalohusu afya ya Wananchi. Hatuwezi kuwa na hiari katika jambo linalohusu usalama wa nchi nzima, ni ama iwe LAZIMA kwa wote kama chanjo ni mhimu au ISIWEPO kabisa ikiwa haina umhimu. Kama ni hiari, Serikali ijitenge na uhalifu huu, isiagize chanjo yoyote wala isiwaulize watu kama wamechanja ama la. Mwenye kutaka kwenda Macca atajua cha kufanya achanjwe ikiwa ndio kigezo.

Hatuwezi kuwa na nchi ya mchanganyiko wa watu salama na wafu watarajiwa. Tutaishije waliochanjwa na wasiochanjwa. Tuamue kuchanja ama kutochanja, fullstop Serikali iache kusema uongo, kama haina ubavu wa kuipinga, chanjo ni lazima kwa wote tujiandae!

#BurianiJPM.
MenukaJr,
Da'slama.
 
Eti mchanganyiko wa watu wazima na wafu watarajiwa! Kachanjwe wewe na familia yako muishi milele. Waulize dawa ya Madagasca utafiti wake uliishia wapi? Corona imekuzwa mno ili kuogopesha watu waingie kwenye mtego waliotegesha. Jiulize lockdown imeishia wapi?
 
Kwani wewe ukichanja unaogopaje wasiochanjwa? Mbona wajawazito ni lazima kuchanjwa ile ya pepopunda lakini wanaume hawachomi mpk mtu ajichome na bati au kitu chenye kutu ndo achome. So chanjo ibaki ihari kwa mtu. Kila mtu ni marehemu mtarajiwa na hatujui sbb itakayokutoa duniani. Chanjo si tiketi ya kuishi milele
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom