#COVID19 Chanjo ya Coronavirus kuanza kutolewa kwenye Mikoa 10 ya Tanzania bara

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,853
2,000
Mikoa hiyo ya kipaumbele ni Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Kigoma, Singida, Dodoma, Iringa na Mtwara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kupokea msaada wa dozi zaidi ya milioni moja za chanjo ya corona aina ya Johnson & Johnson.

Alisema msaada huo umetolewa na Marekani ikiwa sehemu ya ahadi ya nchi hiyo ya kutoa angalau dozi milioni 25 kwa Afrika kati ya dozi milioni 80 zilizoahidiwa kwa bara hilo.

Waziri huyo aliishukuru Marekani kwa mchango mkubwa wa kutoa chanjo kwenye mpango wa COVAX Facility ambao umewezesha Tanzania kuwa nchi mojawapo kupata dozi 1,058,400 zitakazosaidia kupambana na corona.

Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha angalau asilimia 60 ya Watanzania wanapata chanjo hata baada ya hizo kutumika.

“Chanjo hii itaanza baada ya watalaamu kujiridhisha, wataalamu wetu wanafanya taratibu za kujiridhisha kabla ya kuanza mchakato wa kuchanja. Ninawaomba wananchi wajitokeze pindi tukianza,” alisema.

Dk. Gwajima alisema serikali itapokea chanjo ya aina nyingine katika wiki zijazo ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma hiyo na kipaumbele kikiwa ni wahudumu wa afya, watu wazima kuanzia miaka 50 na wenye magonjwa sugu katika mikoa hiyo 10.

“Tunaendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya corona kwa kuzingatia afua zote na sasa tujiandae kupata afua ya chanjo kama silaha bora.

"Afua ya chanjo siyo jambo jipya, Tanzania imekuwa ikipokea chanjo miaka mingi kwa ajili ya kudhibiti magonjwa,” alisema.

Waziri huyo alisema ujio wa chanjo hiyo umefuata taratibu zote ambazo serikali imekuwa ikitumia kujiridhisha kuhusu mapokezi ya bidhaa za afya.

“Kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli, ilielekeza kuwa ‘Wizara ya Afya ijiridhishe kabla ya kupokea chanjo hizo’, wizara haitapokea chanjo hadi ijiridhishe,” alisema.

Dk. Dorothy alisema kuwa kupitia uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wizara imetimiza wajibu wa kujiridhisha.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,359
2,000
Bado sijajua kwanini isitolewe kwa mikoa yote Tanzania kwa wakati mmoja kwasababu muingiliano uliopo ni mkubwa, lakini sio mbaya kwa kuanzia.
 
kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,000
2,000
-ukichanjwa huvai mask tena ?
-ukichanjwa huambukizwi tena ?
-ukichanjwa huambukizi tena ?

kama jibu ni ndio chanjo ni ya nini ?
 
50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
3,004
2,000
@Ms Zomboko

vipi kuhusu Zanzibar, huu msaada wa hizi chanjo milioni moja hauwahusu?
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,057
2,000
Mikoa hiyo ya kipaumbele ni Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Kigoma, Singida, Dodoma, Iringa na Mtwara.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kupokea msaada wa dozi zaidi ya milioni moja za chanjo ya corona aina ya Johnson & Johnson.

Alisema msaada huo umetolewa na Marekani ikiwa sehemu ya ahadi ya nchi hiyo ya kutoa angalau dozi milioni 25 kwa Afrika kati ya dozi milioni 80 zilizoahidiwa kwa bara hilo.

Waziri huyo aliishukuru Marekani kwa mchango mkubwa wa kutoa chanjo kwenye mpango wa COVAX Facility ambao umewezesha Tanzania kuwa nchi mojawapo kupata dozi 1,058,400 zitakazosaidia kupambana na corona.

Alisema lengo la serikali ni kuhakikisha angalau asilimia 60 ya Watanzania wanapata chanjo hata baada ya hizo kutumika.

“Chanjo hii itaanza baada ya watalaamu kujiridhisha, wataalamu wetu wanafanya taratibu za kujiridhisha kabla ya kuanza mchakato wa kuchanja. Ninawaomba wananchi wajitokeze pindi tukianza,” alisema.

Dk. Gwajima alisema serikali itapokea chanjo ya aina nyingine katika wiki zijazo ili kuhakikisha watu wote wanapata huduma hiyo na kipaumbele kikiwa ni wahudumu wa afya, watu wazima kuanzia miaka 50 na wenye magonjwa sugu katika mikoa hiyo 10.

“Tunaendelea kuchukua tahadhari zote dhidi ya corona kwa kuzingatia afua zote na sasa tujiandae kupata afua ya chanjo kama silaha bora.

"Afua ya chanjo siyo jambo jipya, Tanzania imekuwa ikipokea chanjo miaka mingi kwa ajili ya kudhibiti magonjwa,” alisema.

Waziri huyo alisema ujio wa chanjo hiyo umefuata taratibu zote ambazo serikali imekuwa ikitumia kujiridhisha kuhusu mapokezi ya bidhaa za afya.

“Kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Rais John Magufuli, ilielekeza kuwa ‘Wizara ya Afya ijiridhishe kabla ya kupokea chanjo hizo’, wizara haitapokea chanjo hadi ijiridhishe,” alisema.

Dk. Dorothy alisema kuwa kupitia uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, wizara imetimiza wajibu wa kujiridhisha.
Chanjaneni tu, mi naendeleza wanzuki na kimpumu kumuua COVID-19
 
Black belts

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,433
2,000
Hatimaye mama mwenye sura na roho mbaya ameacha maigizo ya kula matunda yaliyooza na kuhimiza chanjo baada ya mwendakuzimu kufa!
Huyu mama ni mnafiki, kigeugeu, hafai kuwa kiongozi!
Mwendazake Ni Nani katika hii nchi Hadi kila mtu afuate akili zake za ukichaa??????? Ye alidhani Ni sifa kuiletea dharau Covid19,ikaendanae mazima
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,766
2,000
Bado sijajua kwanini isitolewe kwa mikoa yote Tanzania kwa wakati mmoja kwasababu muingiliano uliopo ni mkubwa, lakini sio mbaya kwa kuanzia.
Kwenye suala la chanjo upo vyema sana, hongera. Ila akiguswa Mbowe au CDM huwa unakuwa mbogo haswaa haha
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
12,009
2,000
Hatimaye mama mwenye sura na roho mbaya ameacha maigizo ya kula matunda yaliyooza na kuhimiza chanjo baada ya mwendakuzimu kufa!
Huyu mama ni mnafiki, kigeugeu, hafai kuwa kiongozi!
Hakuna maajabu hapo! hata mm ningekuwa kigeugeu......
nafanya kile bosi anataka.....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom