#COVID19 Chanjo ya Corona ina-expire kila baada ya miezi sita (6). Serikali imejipangaje?

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,406
2,000
Ndugu zangu,

Kwa walichoma chanjo ya Corona wanachoma sindano mbili ndani ya wiki tatu (3) na baada ya hapo unapata cheti ambacho kinakuwa halali ndani ya miezi (6) kisha unatakiwa kuchanjwa tena ili uwe na kinga.

Ikumbukwe Tanzania ina watu zaidi ya milioni hamsini (50),kama angalau watu milioni 30 wakichoma kila mwaka inaweza kugharimu dola milioni 90-120 kila baada ya miezi sita ikiwa dozi itauzwa dola 3-4 ambayo ni bei ya AstraZeneca kwa wastani.

Serikali inapaswa kuweka mpango madhubuti ili kukabiliana na gharama ya chanjo kama wananchi watahamasika la sivyo tutaishia kugawa chanjo kwa awamu ya kwanza kisha tukashindwa kuwa endelevu kwa tatizo la afya sio covid-19 tu!

Ni natumaini kuna mpango madhubuti kwani tukilemaa wajanja watatumia hizi chanjo kupata rasilimali zetu kwa bei mchekee.
Kwani Gwajima anasemaje?
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,885
2,000
Hili nalo ni neno lkn hili ni gonjwa lamlipuko kama kilivyo kipindupindu yaani!

Malaria ipo ipo japo huko pia serikali haiko nyuma nadhani unaona hatua inazochukua (vyandarua bure, kupulizia majumbani nk)

Kiufupi huyu Delta hana masiharaha kabisa aiseeee! Tupateni chanjo tujikinge sisi na wapendwa wetu
😁😁🤣 Ngosha mashine,mhala jomba!
 
myoyambendi

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
106,918
2,000
Ndugu zangu,

Kwa walichoma chanjo ya Corona wanachoma sindano mbili ndani ya wiki tatu (3) na baada ya hapo unapata cheti ambacho kinakuwa halali ndani ya miezi (6) kisha unatakiwa kuchanjwa tena ili uwe na kinga.

Ikumbukwe Tanzania ina watu zaidi ya milioni hamsini (50),kama angalau watu milioni 30 wakichoma kila mwaka inaweza kugharimu dola milioni 90-120 kila baada ya miezi sita ikiwa dozi itauzwa dola 3-4 ambayo ni bei ya AstraZeneca kwa wastani.

Serikali inapaswa kuweka mpango madhubuti ili kukabiliana na gharama ya chanjo kama wananchi watahamasika la sivyo tutaishia kugawa chanjo kwa awamu ya kwanza kisha tukashindwa kuwa endelevu kwa tatizo la afya sio covid-19 tu!

Ni natumaini kuna mpango madhubuti kwani tukilemaa wajanja watatumia hizi chanjo kupata rasilimali zetu kwa bei mchekee.
🤣 🤣 🤣 🤣 UMESOMA WAPI HIYO.....
 
Kitombile

JF-Expert Member
Mar 21, 2021
789
1,000
Ha
U

Unajua death rate ya Malaria kwa mwaka wewe? Corona yako itakaribia hata kwa robo?
Kaa kijiweni kunakokufaa wewe, matusi na kucheza pool,haya ya kitaalamu waachie walioenda shule.
Ambao hujibu kwa hoja siyo upupu Kama wako.
Au wewe utaishi milele?
Hakika
 
geranteeh

Senior Member
May 21, 2015
128
250
Kwenye baraza la mawaziri,kuna mawaziri watatu wanaojua "undani" wako. Umeshindwaje kuwauliza au kuwapa angalizo hao!!??
Baraza hilo hilo la mawaziri walihusika na kupitisha kujenga kituo cha mwendo kasi jangwani wakijua kuna mafuriko yalipokuja yaliharib magari yaliyonunuliwa kwa kodi zetu alaf baraza hlo hlo kupitia waziri wa miundombinu and blaa blaa blaa waliamua kujemga daraja la salender lisilo na umuhim wakaacha jangwani tuzunguke pindi mvua inaponyesha
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,319
2,000
Kamanda jadili hoja
Baraza hilo hilo la mawaziri walihusika na kupitisha kujenga kituo cha mwendo kasi jangwani wakijua kuna mafuriko yalipokuja yaliharib magari yaliyonunuliwa kwa kodi zetu alaf baraza hlo hlo kupitia waziri wa miundombinu and blaa blaa blaa waliamua kujemga daraja la salender lisilo na umuhim wakaacha jangwani tuzunguke pindi mvua inaponyesha
 
mohamedjohn

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
467
500
Ukiuliza mateja wengi mara ya kwanza kutumia dawa walinunua kwa pesa yao ?wengi watakwambia walipewa bure au kununuliwa lakini walipokuwa addicted wale waliowanunulia ndo waligeuka wauzaji na kuwauzia ... sasa mnapewa bure lakini ikifika huko mbele mtanunua kwa pesa yenu hapo ndo mtawekewa mpk kodi ya kutembea barabarani

Watakao piga Chanjo watakuwa watumwa wa watengenexa chanjo mfano mmepiga then baada ya miaka 2 wanasema hyo chanjo baada ya muda fulani inakuwa sumu kuna booster yake na dose ni dola elf 7 hapo ndo mtakapouza vijumba vyenu vya urithi wengine kuingia ktk madeni ambayo hayalipiki kwa kitu ulichopewa bure na ndo shobo zitawaisha
nimeipenda hi ukiwauliza mateja ???
 
makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
17,442
2,000
Hili nalo ni neno lkn hili ni gonjwa lamlipuko kama kilivyo kipindupindu yaani!

Malaria ipo ipo japo huko pia serikali haiko nyuma nadhani unaona hatua inazochukua (vyandarua bure, kupulizia majumbani nk)

Kiufupi huyu Delta hana masiharaha kabisa aiseeee! Tupateni chanjo tujikinge sisi na wapendwa wetu
Je, nikishachanjwa, naweza kuishi bila masharti kama kuvaa barakoa, kukaa kwenye mkusanyiko wa watu?
Je, siwezi kuambukizwa?
Je, nikiupata siwezi kufa kwa korona!?
 
Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
2,933
2,000
La tunatumia nguvu kudhibiti ugonjwa ulioua wazungu takribani 4m. Wa Afrika laki mbili.
Badala ya kutumia nguvu kwenye Malaria inayoua mamilioni ya wa Afrika?
Kiongozi umenena ukweli usiokubalika na wengi. Tumenunua risasi kuua panya na tunatumia fimbo kupambana na simba.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom