#COVID19 Chanjo ya China kuidhinishwa na WHO ni muhimu kwa mapambano ya COVID-19 barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111315391146.jpg



India ni nchi inayotengeneza na kutoa chanjo ya Corona kwa wingi zaidi kwa nchi za Afrika kupitia mpango wa COVAX, lakini wimbi jipya la maambukizi ya virusi linalotokea nchini humo litasababisha ugumu kwa utoaji wa chanjo. Kutokana na nchi nyingi za Afrika kumaliza sehemu ya kwanza ya chanjo zilizopata kupitia mpango wa COVAX, Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuwa Afrika itakabiliwa na hatari ya kutokea kwa wimbi jipya la maambukizi. Lakini pengine wasiwasi huo hautatokea.



Baada ya tathmini kamili iliyofanywa kwa karibu nusu mwaka, Shirika la Afya Duniani WHO hivi karibuni liliidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya Sinopharm, jambo ambalo limeonesha kuwa chanjo hiyo ya China imekuwa chanjo ya kwanza ya Corona kutoka nchi isiyo ya magharibi. Hadi kufikia tarehe 5 mwezi huu, dozi bilioni 1.1 zimetolewa kote duniani, lakini asilimia 80 ya chanjo hiyo imeenda kwenye nchi zenye mapato ya juu na kati, huku kiwango cha chanjo kwenye nchi za mapato ya chini kikiwa asilimia 0.3 tu. Hapo awali COVAX ilipanga kutoa dozi bilioni 2 kote duniani kwa mwaka huu, lakini kutokana na upungufu wa uzalishaji wa chanjo, na baadhi ya nchi zilizoendelea kuhodhi chanjo, hadi sasa mpango huo umetoa dozi milioni 54 tu. Idhini hii ya WHO itaiwezesha China kutoa mamilioni ya dozi za chanjo ya bei nafuu kwa nchi zinazoendelea na zilizo nyuma kimaendeleo, uzalishaji wake ukiwa mkubwa na mazingira ya kuhifadhi chanjo hiyo si magumu, na kutatua suala la uhaba wa chanjo linalozikabili nchi za Afrika zinazotegemea mpango wa COVAX kujipatia chanjo.

VCG111328899405.jpg


China ni nchi ya kwanza duniani kuahidi kufanya chanjo ya Corona kuwa bidhaa ya umma duniani, na kujiunga na mpango wa COVAX uliozinduliwa na mashirika ya kimataifa ikiwemo WHO kwa lengo la kuhakikisha chanjo zinatolewa kwa usawa, ili kuzisaidia kivitendo nchi zenye mapato ya chini kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti wa Uingereza Airfinity, China imetoa dozi milioni 240 za chanjo kwa nchi za nje, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko jumla ya dozi za chanjo hiyo zilizotolewa na nchi nyingine, na pia kuahidi kutoa dozi nyingine milioni 500. Hivi sasa Marekani na Umoja wa Ulaya wanasita kuunga mkono juhudi za kimataifa za kupambana na virusi vya Corona kutokana na kuenea kwa virusi hivyo nchini India, Brazil na kwenye nchi nyingine. Kwa hivyo, kama alivyosema mtafiti mwandamizi wa afya ya dunia kutoka baraza la mahusiano ya kigeni la Marekani Bw. Huang Yanzhong, “China sio tu ni nchi inayotoa chanjo kwa wingi zaidi duniani, kwa nchi nyingi, lakini chanjo ya China itakuwa ni chaguo pekee.”



Baada ya chanjo ya China kuidhinishwa na WHO, inatarajiwa kuwa China itatumia njia tatu kusaidia nchi za Afrika kukabiliana na virusi hivyo. Kwanza, itatoa mchango wake katika jukwaa la kimataifa. Kabla ya hapo, China imetangaza kutoa dozi milioni 10 za chanjo kwa COVAX. Hivi sasa kampuni ya Sinopharm inafanya majadiliano na Muungano wa Chanjo Duniani Gavi ili kuongeza kutoa chanjo kwa COVAX. Pili, China itaendelea na juhudi za kutoa msaada kwa nchi nyingine katika ushirikiano wa pande mbili mbili. China ni nchi inatoa chanjo kwa wingi zaidi duniani kwa nchi zinazoendelea. Hadi sasa imetoa msaada wa chanjo kwa nchi zaidi ya 80 zinazoendelea, ambapo nchi za Afrika zaidi ya 20 zimepata dozi cha chanjo zaidi ya milioni moja, na pia imeuza chanjo yake kwa nchi zaidi ya 50. Tatu, China itazisaidia nchi za Afrika kuwa na uwezo wa kuzalisha chanjo. Njia muhimu ya kuhakikisha Afrika inapata chanjo kwa usawa ni kuiwezesha kuwa na uwezo wa kuzalisha chanjo hiyo yenyewe, na kama Afrika itaendelea kutegemea sehemu nyingine kutoa chanjo, kama ukosefu unatokea, basi Afrika itakuwa ya mwisho kupata chanjo. Mapema mwezi huu, China na Misri zilisaini makubaliano ya ushirikiano wa uzalishaji wa chanjo nchini Misri. Inatarajiwa kuwa mwezi ujao, chanjo inayotengenezwa na kampuni ya Misri itaingia sokoni. Ushirikiano wa uzalishaji wa chanjo kati ya China na Misri sio tu utasaidia Misri kuwa na uwezo wa kuzalisha chanjo, bali pia utasaidia kutoa chanjo kwa nchi nyingine za Afrika ili kukabiliana na virusi hivyo, jambo ambalo hakika litatuliza wasiwasi wa bara la Afrika linaloachwa na jamii ya kimataifa katika kupata chanjo.



Imefahamika kuwa mbali na chanjo ya Sinopharm, chanjo nyingine ya China Sinovac pia iko katika kipindi cha mwisho cha kuidhinishwa na WHO kwa matumizi ya dharura, na matokeo yake yatatolewa hivi karibuni. Watu wanasema wakati virusi vya Corona vinapoenea, hadhi ya China kama nchi yenye nguvu kubwa duniani katika sekta ya afya inaimarishwa. China ikiwa nchi inayoendelea, mafanikio inayopata leo ni matokeo wala sio lengo. Kama ilivyosema makala iliyochapishwa tarehe 10, Mei na gazeti la Newsday la Zimbabwe yenye kichwa cha habari “mafanikio ya chanjo ya China si ya ajabu”, pengine nchi zilizoendelea zinajisifu kwa chanjo zao zinazosemekama kuwa na ufanisi mkubwa, lakini ni chanjo ya China inayotengenezwa kwa mbinu ya jadi inaisaidia dunia nzima kukabiliana na janga hilo kimya kimya. China itaendelea kutekeleza wajibu wake, na ikiwa mwenzi mzuri wa nchi za Afrika, China itafikisha chanjo moja moja katika kila kona ya Afrika, kuhakikisha watu wa Afrika wanapata chanjo salama, yenye ufanisi na bei nafuu, kutimiza lengo la kuwawezesha watu zaidi ya asilimia 60 barani Afrika kuchanjwa na kuepusha maambukizi mapya ya virusi vya Corona.
 
Wajitahid wasije kutengenez za Dunia ya 3 na za zanchi zilizoendelea
 
Wajitahid wasije kutengenez za Dunia ya 3 na za zanchi zilizoendelea

Binafsi namshauri Madam President SSH kwamba taifa letu likifikia uhamuzi wa kuchanja raia wake ni busara tukidunga wananchi chanjo zinazo zalishwa na Wachina - kwa nini nasema hivyo??

Sababu za kupendekeza chanjo za Uchina au (Urusi au Cuba zikipata kibali cha WHO) sababu yangu ni ya kisayansi zaidi kutokana na chanjo hizo zinazalishwa/tengenezwa kwa njia ya asili ambayo imetumika kuzalisha chanjo za aina tofauti Duniani kwa zaidi ya miaka themanini plus 80+, tofauti kabisa na hizi chanjo za COVID-19 za magharibi zinazo zalishwa kwa ku-tinker around na vinasaba (mRNA), mpaka sasa hakuna mwenye uhakika wa short na long madhara yanayo weza kusababishwa na chanjo zinazo zalishwa kwa njia ku-manipulate vinasaba - hata Big Pharma Companies za maghararibi zinazo zalisha chanjo za vinasaba ukiwauliza madhara yake ni yepi hasa wana baki kupiga danadana swali hawa kupatii jibu lenye uhakika!!

Bottom line is: Serikali yetu iwe makini na chanjo hizo za vinasaba, ili raia wetu wasije kutumika kama Guinea pig baada ya kuwadunga chanjo zinazo tokana na unproven teknolojia ya kijinetiki. Hayo ni maoni yangu.
 
Back
Top Bottom