Chanjo mpya malaria kuingia sokoni Oktoba Mwaka huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chanjo mpya malaria kuingia sokoni Oktoba Mwaka huu

Discussion in 'JF Doctor' started by Mahesabu, Apr 22, 2011.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Na Jane Mihanji

  TATHMINI ya chanjo mpya ya Malaria iko katika hatua ya mwisho ya majaribio ambapo Oktoba mwaka huu, inatarajiwa kuingizwa sokoni. Hayo yalisemwa Dare s Salaam jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Hadji Mponda alipokuwa akifungua mkutano wa kitaifa wa kudhibiti malaria ulioandaliwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara(IHI). Dk. Mponda alisema kutokana na tatizo kubwa la malaria duniani na hasa barani Afrika, watafiti wamekua wakihangaika kutafuta dawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo ambao umekuwa ukiua sana watoto na wanawake wajawazito. Alisema chanjo hiyo iliyoanza kufanyiwa utafiti na IHI mjini Bagamoyo na NIMR huko Korogwe tangu mwaka 2000, ikionekana inafaa itaongeza nguvu katika kinga dhidi ya malaria.


  Dk. Mponda aliwapongeza watafiti nchini kwa juhudi za kuhakikisha ugonjwa huo unapungua kama siyo kutoweka. “Serikali inaunga mkono juhudi zenu, ndiyo maana hata Rais Kikwete akizindua kampeni za malaria haikubaliki,” alisema. Akiwasilisha mada juu ya hali ya malaria Zanzibar, Dk. Mohmmed Jiddawi alisema hivi sasa wagonjwa wa malaria wamepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na siku za nyuma. Alisema malaria imepungua kwa asilimia 73 kutoka mwaka 2007 hadi 2010. “Hivi sasa wazanzibar wachache sana wana malaria na vifo vimepungua kutoka asilimia 35 mwaka 2007 hadi asilimia 5 mwaka 2009,” alisema.

  Sambamba na takwimu hizo, Dk. Jiddawi alisema hata idadi ya wagonjwa wanaolazwa kutokana na malaria imepungua. Akizungumza katika mkutano huo ambao ni maandalizi ya siku ya malaria duniani, mkurugenzi wa IHI Dk. Mohammed Abdullah, alisema hali ya maambukizi ya ugonjwa huo imepungua kwa kiasi kikubwa hasa katika maeneo ya mijini. Alisema hivi sasa taasisi yake inaendelea na utafiti wa dawa mpya ili iongeze idadi ya dawa za malaria katika kukabiliana na hali ya dawa sugu au upungufu wa dawa za malaria siyo tu kwa Tanzania, bali katika bara lote la Afrika. Aliwataka wanannchi kutumia chandarua chenye dawa kwa ajili ya kujikinga na malaria na kutunza mazingira katika jitihada za kupambana na mazalia ya mbu
   
 2. kure11

  kure11 Senior Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizo ni lugha za kisiasa tu kweli miradi ipo bagamoyo na korogwe na nchi nyingine za Africa, utafiti unaendelea vizuri Ila October chanjo haiwez kuwa sokon kwani hiyo chanjo bado ipo hatua ya majaribio na inatarajiwa kuwa imeisha Dec 2012.baada ya hapo inabidi ihakikiwe na wHO Na wengine.,Inawezekanaje iwe tayari by October??? Kwa upande wa korogwe na bagamoyo ni majaribio ya chanjo ya watoto under 5.
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Mkurugenzi wa IHI ni Dr Salim Abdulla...
   
 4. Kagondo

  Kagondo JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2016
  Joined: Jun 6, 2016
  Messages: 291
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
Loading...