Chanjo dhidi ya Ukimwi kufanyiwa majaribio Afrika Kusini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_92689300_p04j6l86.jpg


Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.

Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema.

Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.

Washiriki hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35.

Majaribio hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu

"Ikitumiwa pamoja na silaha tulizo nazo sasa za kuzuia maambukizi, chanjo hiyo inaweza kuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Ukimwi,"

Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Maradhi ya Kuambukizana na Mzio ya Marekani (NIAID) amesema kupitia taarifa.

"Hata kama mafanikio yake yatakuwa ya kadiri, hilo linaweza kupunguza pakubwa mzigo unaotokana na maradhi hayo katika nchi zenye viwango vya juu vya maambukizi, mfano Afrika Kusini."

Chanjo ambayo itafanyiwa majaribio chini ya HVTN 702 ina uhusiano na majaribio ya chanjo yaliyofanywa mwaka 2009 nchini Thailand.

Chanjo iliyofanyiwa majaribio mwaka huo iligunduliwa kuwa na mafanikio asilimia 31.2 katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika kipindi cha ufuatilizi cha miaka 3.5 baada ya mtu kupewa chanjo.

Wanasayansi wametayarisha chanjo hiyo mpya mahsusi kutoa kinga pana na kwa muda mrefu na kwa kuangazia zaidi aina ya virusi vinavyopatikana kusini mwa Afrika.

Watakaoshiriki katika majaribio hayo ni watu wa kujitolea.

Wanachaguliwa bila kufuata mpangilio wowote, ambapo kundi moja litapokea dozi ya chanjo kwa kipindi fulani na jingine kipimo kisicho cha chanjo. Washiriki wote watadungwa sindano tano katika kipindi cha mwaka mmoja.

Washiriki watakaoambukizwa virusi vya Ukimwi katika kundi hilo watatumwa kwa wahudumu wa afya ili kupokea matibabu ya kupunguza makali ya virusi hivyo na pia kushauria jinsi ya kupunguza hatari ya kueneza virusi hivyo.

Taifa hilo hata hivyo limezindua mpango mkubwa wa kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo na kuudhibiti, mpango ambao inasema ndio mkubwa zaidi wa aina yake duniani.

Kiwango cha wastani cha umri wa kuishi kilikuwa kimeshuka sana nchini humo na kufikia miaka 57.1 mwaka 2009 lakini kutokanana na juhudi hizo, kimepanda hadi miaka 62.9 kufikia 2014.

Matokeo ya majaribio hayo ya chanjo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka 2020.

Chanzo: BBC
 
Haitakuja kutokea dawa wala chanjo, ukimwi ni biashara kubwa sana kwa wazungu, walete chanjo au tiba wao waishi vipi?
 
Chanjo ya UKIMWI itaanza kutolewa kama majaribio kwa watu 5400 huko Afrika ya Kusini. Chanjo hiyo iliyopewa jina la HVTN702 ina uhusiano na ile chanjo iliyofanywa Thailand mwaka2009 na kuonyesha mafanikio kwa asilimia 31.2 baada ya miaka 3.5 ya mtu kupewa chanjo. Na majibu ya chanjo hii yatatolewa mwaka 2020.

Tuombeni Mungu chanjo hiyo iwe na mafanikio.
 
Hivi ni habari njema kwa wagonjwa au wasio wagonjwa? kwani chanjo inakinga sio kuponya
 
WAKATI REPORT ZA WHO zinasema wagonjwa wengi hawajijui kama wanaugua Ukimwi Duniani
Ni kweli mkuu Kuna mtoto mmoja kazaliwa na Wazazi wenye ukimwi hawajawahi kumwambia mpk Sasa na dogo Ana AFYA nzuri kabisa Kuna kipindi anaumwa tu kama week akipona hapo haumwi tena hata miezi 8.. Sasa hivi Ana miaka 16.naona bora wamwabie tu asije kusambaza
 
Ni kweli mkuu Kuna mtoto mmoja kazaliwa na Wazazi wenye ukimwi hawajawahi kumwambia mpk Sasa na dogo Ana AFYA nzuri kabisa Kuna kipindi anaumwa tu kama week akipona hapo haumwi tena hata miezi 8.. Sasa hivi Ana miaka 16.naona bora wamwabie tu asije kusambaza
hao wengi sana siku hz,unaweza dhani kadogo hakana wacha nikapge kavu nifaid,kumbe unajiumiza
 
Back
Top Bottom