junky
JF-Expert Member
- May 11, 2017
- 413
- 976
Kata nyingi Dar es salaam ukiacha mitaa ya kishua kama masaki,osterbay,msasani,upanga na nyinginezo zinazofanana na maeneo hayo pia kuna kata za kistaarabu yaani za wastani kidogo zina afadhali na unafuu
Lakini asilimia kubwa za kata jijini Dar ni mchanganyiko ya wa walionacho na wasio nacho ,sehemu nyingi hapa dar kuna watoto wanaoitwa number D
Number D ni vijana wanaochipukia na kupenda usela hivyo wamebatizwa jina la number D..maeneo mengi dar watoto kusoma kwao mwisho form 4 na wengi hio form 4 hawafiki na shule zao ni shule za kata na tunafahamu vijana wengi wanaosoma shule za kata ni nadra kuvuka na kufaulu
Ndipo ukienda kata nyingi unakuta vijana wengi wanakaa maskani na kusikiliza nyimbo za singeli na kuvuta bangi siku hizi kuna maskani nyingi za mabinti wadogo wanavuta bangi sasa hawa wa kiume ndio usiseme na wengi wanapenda usela na usiku wanatoka mchomoko aidha kwenda kuvunja au kukaba sababu wengi hawafanyi kazi na hawataki kazi
Ndio maana kuna kata nyingi saizi wameweka sungusungu ili kulinda mtaa na wakabaji na wanaovunja na kuiba,saizi ukienda sehemu kibao usiku utaona unasimamishwa na kuanza kuhojiwa
Lakini kata ambazo hazina sungusungu ni rahisi kuwa wahanga sababu wezi wa mchomoko wanajua rada za mitaa na hivyo sehemu tulivu au za kimwinyi ni rahisi kuingia na kuiba huku ninapoishi kulikuwa na umwinyi sana ikawa kila siku watu wanaibiwa mwisho wa siku vijana wakajikusanya na kuanza doria kimya kimya na kufanikiwa kuwadaka wanaonyata usiku na kuiba na kuwaadabisha tokea hapo wezi wakawa hawagusi mtaani wanapaogopa
Maeneo mengi dar kuna hawa number D na wako wengi kazi yao ni kuitana unakuta mtaa una sura ngeni ya vijana wengi sababu wenyeji ndio wanaowaleta hao marafiki wa maskani za mbali na huwa ni rahisi kufanya michongo
Kimara palikuwa panaonewa sana mwisho wa siku vijana wengi wamekufa ,tabata kuna vijana wengi wameuliwa kikatili na sungusungu
Yaliyotokea chanika yametokea maeneo mengi ,na maeneo mengi dar kuna maskani za kijinga sana na asilimia kubwa ya vijana ni wahovyo wapenda usela,matusi,watukutu na sifa za vijana hawa hufanana
Kuna eneo tandika wakisikia kijana kafanya ujinga wa kipumbavu alikuwa anafuatwa huyo mtu hadi chumbani kwake na kutolewa na kupewa adabu
Kilichotokea chanika ni umwinyi kupitiliza maana kuna sehemu palikuwa panasifika kwa usela,uhuni na kila aina ya ujinga kama Tandale na mwananyamala? Lakini vijana wa Tandale na mwananyamala wanaishia kutumia tu kwa kunywa pombe na umalaya mtaani lakini wizi wa kijinga hukuti ukifanyika kwasababu ya kanuni zilizowekwa mtaani kila mtaa kuna sungusungu mwisho wa siku wale watukutu wanaenda kuiba kata za mbali
Kwahili natumai Chanika mtajifunza ulizeni kwanini mwananyamala ,Tandale na maeneo mengine wameweza kutuliza mitaa na wakati sehemu hizo kuna wahuni wengi tu...