PSEUDOPODIA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 376
- 735
Jamani sitachoka kupiga kelele kuende kuileta hii kero yetu kwenu hasa viongozi wetu.
Sisi wananchi wa Chanika kitongoji cha Kidugalo hususani baadhi ya mashina ya kitongoji kero yetu kubwa ni umeme.
Tulipoona mradi wa Rea umefika tulifurahi sana nae kusema hatimae Mungu amesikia kilio chetu, lakini cha ajabu ni kuwa ulipo Anza ugawaji umeme tulimejikuta kwenye hali ya sintofahamu baada ya mkandarasi kupokea maagizo kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa kwamba kuna baadhi yae mashina hawaruhusiwi kupata umeme.
Mwenyekiti alitoa maagizo hayo kama adhabu kwa wananchi hao kwakuwa kipind cha uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa hatukumpigia kura kwenye uchaguzi wa ndani wa chama.
Hivyo basi mkandarasi akafuata maelekezo ya mwenyekiti na kweli kuna mashina mengi yanerukwa licha ya kuwa nguzo za umeme mkubwa zimepita kwao kwenda kwenye mashina mengine yanayostahili kupewa umeme. Tumejaribu kufuatilia kwenye ofisi za Tanesco zilizofunguliwa huku Chanika lakin hatujapata msaada, na mkandarasi anasema yeye mradi kashamaliza hukue kwetu nae kashakabizi.
Hivyo basi Mimi nawaomba viongozi wetu mnao husika na haya maswala mjaribu kutusaidia kwani na sisi ndoto yetu ni siku moja tuwashe umeme kwenye nyumba zetu kama wengine.
Ahsanteni.