Changudoa waongoza kwa kutumia kondomu za kike

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,886
Changudoa waongoza kwa kutumia kondomu za kike

2008-08-04 15:54:12
Na Mary Wejja, Jijini

Imedaiwa kuwa, idadi kubwa ya wanawake wanaotumia kondomu za kike, ni wale wanaofanya biashara ya kuuza miili yao (machangudoa), ambao wengi wameonyesha kuipokea elimu juu ya matumizi ya zana hiyo kwa furaha.

Hayo yamebainishwa na Bi.Janeth Shombe, mtoa huduma kutoka kampuni ya T.MARC ambayo inashughulika na utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya kondomu, usambazaji wa bidhaa hiyo nchini, na huduma nyingine zikiwemo za uzazi wa mpango.

``Unajua idadi kubwa ya wanawake bado hawatumii kondomu za kike ingawa elimu imetolewa kwa wingi...watumiaji wengi wa kondomu za kike ni madada poa (machangudoa), wao tuliwapa elimu na hali inaonyesha wameipokea kwa wingi, `` akasema Bi.Shombe.

Akasema, pamoja na hali hiyo T.MARC bado inaendelea kutoa elimu kwa wanawake kuhusiana na utumiaji wa kondomu hizo ambazo zinamsaidia kujiamini na kujiwekea usalama zaidi kwa afya yao.

Akizungumzia kuhusiana na uhaba wa kondomu za kike katika nyumba za wageni, alisema taarifa hizo zimeshawafikia na akasema tatizo hilo linashughulikiwa.

Hata hivyo Alasiri ilipojaribu kuongea na baadhi ya wanawake kadhaa Jijini kuhusiana na utumiaji wa kondomu za kike, walisema hawazitumii kwa kuwa zinaleta usumbufu wakati wa uvaaji.

Wengine walidai kuwa wanaona aibu kwenda kuzinunua kutoka kwenye maduka ya dawa.

``Mimi sijawahi hata kuiona kondomu ya kike,`` mama mmoja alidai.
 
...Wawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mwanawane!!!! halafu unataka Kova awafunge hawa????
 
Kondomu za kike ni adimu sana na hazipatikani. Mimi binafsi sijawahi kuziona. Inabidi pawepo na juhudi za makusudi kuzigawa kwa wanawake kwa gharama yoyote ile. Kwa kuanzia ninashauri zingetolewa bure kwani waliowengi wanadai ni ghali mno na ni ngumu au zinasumbua wakati wa kuzivaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom