Changing of Guard? CCM bado wako usingizini wakati CHADEMA wakijipenyeza kwa kasi Vijijini.

Haiwi reversed na siasa za kitaifa, inakuwa reversed kwa matendo yanayo mgusa mpiga kura. Mtu wa kijijini. 95% ya watoto walifukuzwa UDOM ni wa wakulima, wenye vyeti feki, ni watoto wa wakulima, wanaovunjiwa nyumba kwa kujenga kwenye maeneo yasiyofaa ni watu wakawaida sana. Wanaoumuzwa na bei ya sukari, ni watu wa chini; ambao mazao yao yanauzwa kwa bei ya kutupa ni wakulima, wenye kipato kisichotosheleza milo mitatu ni watu wa chini na wameongezeka. Nani atawapa kura? Walioipa CHADEMA kura hawana sababu ya kupungua, ila walioipa kura CCM na rais wao zipo sababu lukuki za kupunguza kura. "Ajidhaniae amesimama aangalie asianguke"
Mkuu uko sahihi kabisa kwa analysis ndogo tumkama hii unaweza kuona jinsi jamaa alivyo na stress.....amewastress watanzania badala ya kuwa impress.
 
polisi+ usalama wa taifa+ jeshi + tume ya taifa ya uchaguzi= ushindi wa kishindo ( ccm oyeeee)
KWANINI JECHA ALIFUTA UCHAGUZI ZANZIBAR? KWANINI COMPUTER ZA KUJUMLISHIA MATOKEO PALE HAKI ZA BINADAMU ZILIPOKWAAAA? vipi mtu yule aliyekimbia na box la kura pale kinondoni na akarudi nalo baada ya nusu saaa? unauita na ule ushindi?
Hahahaa cccm na ushindi wao wa aibu
 
Kama wewe ni mfia ccm na serikali iliyoko madarakani huwezi kunielewa kamwe maana mawazo na fikra zako ziko ndani ya box, hivyo kuyaona yaliyo nje ya box ni issue pevu

Unapozungumzia Ded (mteule wa mwenyekiti wa ccm taifa) kuwa msimamizi wa uchaguzi ktk jimbo husika unazungumzia mbeleko ya kwanza kwa ccm

Unapozungumzia matokeo ya kura za urais kutokuhojiwa mahakamani tafsiri yake ni kuhalalisha wizi wowote wa kura unaotendeka, na hii ni mbeleko ya pili ya ccm

Mwenyekiti wa tume ni mteule wa mwenyekiti wa ccm taifa, hivyo hana nguvu ya kwenda kinyume na na matakwa ya bosi wake, hii ni mbeleko ya tatu ya ccm

Wakuu wa mikoa/wilaya ni wateule wa rais na ni wanaccm pure na ni wakuu wa kamati za ulinzi na usalama ktk maeneo yao, hivyo wanaweza kufanya lolote kwa wapinzani bila kuchukuliwa hatua zozote, na hii ni mbeleko ya nne ya ccm

Katika uchaguzi ambao sanduku la kura linaweza kuchukuliwa kwenye kituo cha kupigia kura na askari wakiwepo na likarudishwa bila hatua zozote kuchukuliwa na bado unaona haya nayazungumza hayana ukweli! Na hii ni mbeleko ya tano ya ccm

Jivue miwani ya mbao yenye rangi ya kijani ili uone mbele yako kuna nini kinatendeka, vinginevyo utabaki kuwa mtumwa wa fikra za wengine
Mkuu umewamaliza aisee, i reserve your commwnt in my notebook.
 
Back
Top Bottom