Changing of Guard? CCM bado wako usingizini wakati CHADEMA wakijipenyeza kwa kasi Vijijini.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Wataalamu wengi wa Siasa nchini, wamekuwa wakikishauri Chama cha CHADEMA kufanya jitihada za kujitanua na maeneo ya vijijini kwa kuanzisha Ofisi angalao kwa kuanzia na ngazi ya Wilaya na kuwa na Waajiriwa permanent.

Tunashukuru, tangu 2016, CHADEMA kilianzisha mfumo wa kuajiri watumishi (makatibu) lakini ujenzi wa Ofisi huko wilayani umekuwa ni wa kusuasua sana kiasi cha kukatisha tamaa juu ya mikakati hasa ya Chama hicho kuelekea 2020.

CCM imekuwa ikifaidika sana na mfumo wa maisha wa wananchi vijijini, ambao hawakuwahi kuweza kutofautisha kati ya CCM vs Serikali (ya CCM).

Hata hivyo, mapinduzi makubwa ya mitandao ya kijamii, yamesababisha kuenea haraka kwa taarifa katika maeneo ya vijijini kiasi cha kuinufaisha CHADEMA na Wapinzani wengine kuwafikia wananchi vijijini kwa urahisi.

Ile perception ya zamani kuwa vijijini ni ngome ya upinzani, inafaa kubadilishwa kwani hali ya uelewa vijijini imeongezeka maradufu.

Cha ajabu, ukiacha kazi za Viongozi wa Kitaifa wa Chama, hapo katikati hadi chini, ni wazi CCM wako usingizini kwani hawajengi Chama chao kulinganisha na jinsi Upinzani unavyokibomoa huko vijijini.

Mind you, it was just 67% (just 15 million) of the registered voters (23 million) who turned out to the polling stations in 2015.

Pliz, CCM, Zama zimebadilika, mnaachwa nyuma kwani licha ya Rais Magufuli kueneza kwa kasi utendaji kazi wa Serikali yake, bado hakuna wana-CCM wa kuipeleka kwa wananchi. So, Mwalimu wangu UD, Dr. Bashiru utaliona hilo la uduni wa CCM (lumumba/buku 7) mitandaoni kulinganisha na CHADEMA (nyumbu).

Hongera sana CHADEMA but pliz muwalipe vizuri na kwa wakati makatibu wenu ili waeneze siasa zenu vyema vijijini. "Politics is a Science."

IMG_4034.JPG
 
Lengo la bandiko hili ni kuwakumbusha wana-CCM kuwa, watu wengi wanaojiandikisha huwa hawapigi kura, kama mnavyoona Uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo asilimia 33% ambayo ni almost exactly nusu ya wapiga kura. Hii inamaanisha kuwa, kwa kila wapiga watatu, mmoja hakwenda kupiga kura.
So, nategemea strategists, analysts na planners ndani ya Vyumba vya Kizota na Lumumba, wataliona hilo kwa mapana yake.
Kitu cha muhimu ni kufahamu sababu kuu ya idadi hiyo kubwa ya electorates kushindwa kupinga kura. Makundi hayo ni: kundi la vijana waliojiajiri ama kuajiriwa katika sekta binafsi - wengi wakiwa mijini; na kundi la wazee - wengi wakiwa vijijini.
 
Ccm bila jeshi la polisi na tume ya uchaguzi hawana maisha
Hizo ni hoja zinazotolewa na mfa maji. Kama ni vyombo vya dola, pamoja na Tume ya Uchaguzi, kwani Hivi viko Tanzania tu nchi nyingine havipo?
Kwa nini mwanaume ukimtongoza mwanamke akikukataa unasnza kumtuhumu kwa mambo mengi mabaya wakati wanaume wengine wanampata tu tena kwa urahisi? Hivyo, kushinda kwa CCM na kushindwa kwa Upinzani kumekuwa kunatokana na ama kukubalika bado kwa CCM au kutokubalika bado kwa Upinzani.
 
Kama wewe ni mfia ccm na serikali iliyoko madarakani huwezi kunielewa kamwe maana mawazo na fikra zako ziko ndani ya box, hivyo kuyaona yaliyo nje ya box ni issue pevu

Unapozungumzia Ded (mteule wa mwenyekiti wa ccm taifa) kuwa msimamizi wa uchaguzi ktk jimbo husika unazungumzia mbeleko ya kwanza kwa ccm

Unapozungumzia matokeo ya kura za urais kutokuhojiwa mahakamani tafsiri yake ni kuhalalisha wizi wowote wa kura unaotendeka, na hii ni mbeleko ya pili ya ccm

Mwenyekiti wa tume ni mteule wa mwenyekiti wa ccm taifa, hivyo hana nguvu ya kwenda kinyume na na matakwa ya bosi wake, hii ni mbeleko ya tatu ya ccm

Wakuu wa mikoa/wilaya ni wateule wa rais na ni wanaccm pure na ni wakuu wa kamati za ulinzi na usalama ktk maeneo yao, hivyo wanaweza kufanya lolote kwa wapinzani bila kuchukuliwa hatua zozote, na hii ni mbeleko ya nne ya ccm

Katika uchaguzi ambao sanduku la kura linaweza kuchukuliwa kwenye kituo cha kupigia kura na askari wakiwepo na likarudishwa bila hatua zozote kuchukuliwa na bado unaona haya nayazungumza hayana ukweli! Na hii ni mbeleko ya tano ya ccm

Jivue miwani ya mbao yenye rangi ya kijani ili uone mbele yako kuna nini kinatendeka, vinginevyo utabaki kuwa mtumwa wa fikra za wengine
 
Wataalamu wengi wa Siasa nchini, wamekuwa wakikishauri Chama cha CHADEMA kufanya jitihada za kujitanua na maeneo ya vijijini kwa kuanzisha Ofisi angalao kwa kuanzia na ngazi ya Wilaya na kuwa na Waajiriwa permanent. Tunashukuru, tangu 2016, CHADEMA kilianzisha mfumo wa kuajiri watumishi (makatibu) lakini ujenzi wa Ofisi huko wilayani umekuwa ni wa kusuasua sana kiasi cha kukatisha tamaa juu ya mikakati hasa ya Chama hicho kuelekea 2020. CCM imekuwa ikifaidika sana na mfumo wa maisha wa wananchi vijijini, ambao hawakuwahi kuweza kutofautisha kati ya CCM vs Serikali (ya CCM).
Hata hivyo, mapinduzi makubwa ya mitandao ya kijamii, yamesababisha kuenea haraka kwa taarifa katika maeneo ya vijijini kiasi cha kuinufaisha CHADEMA na Wapinzani wengine kuwafikia wananchi vijijini kwa urahisi. Ile perception ya zamani kuwa vijijini ni ngome ya upinzani, inafaa kubadilishwa kwani hali ya uelewa vijijini imeongezeka maradufu.
Cha ajabu, ukiacha kazi za Viongozi wa Kitaifa wa Chama, hapo katikati hadi chini, ni wazi CCM wako usingizini kwani hawajengi Chama chao kulinganisha na jinsi Upinzani unavyokibomoa huko vijijini.
Mind you, it was just 67% (just 15 million) of the registered voters (23 million) who turned out to the polling stations in 2015.
Pliz, CCM, Zama zimebadilika, mnaachwa nyuma kwani licha ya Rais Magufuli kueneza kwa kasi utendaji kazi wa Serikali yake, bado hakuna wana-CCM wa kuipeleka kwa wananchi. So, Mwalimu wangu UD, Dr. Bashiru utaliona hilo la uduni wa CCM (lumumba/buku 7) mitandaoni kulinganisha na CHADEMA (nyumbu).
Hongera sana CHADEMA but pliz muwalipe vizuri na kwa wakati makatibu wenu ili waeneze siasa zenu vyema vijijini. "Politics is a Science."

View attachment 795198
Ili wasiwe na Njaa
 
CCM awamu hii hawahangaiki kwa kuwa wanajua matokeo watayatangaza kwa jinsi wanavyotaka wao.

Upinzani wajiandae kwa hili zaidi kuliko uchaguzi wenyewe!!
 
Hiyo ratio ya Ccm vs chadema, 8:6, mpaka sasa imesha reverse.
Haiwi reversed na siasa za kitaifa, inakuwa reversed kwa matendo yanayo mgusa mpiga kura. Mtu wa kijijini. 95% ya watoto walifukuzwa UDOM ni wa wakulima, wenye vyeti feki, ni watoto wa wakulima, wanaovunjiwa nyumba kwa kujenga kwenye maeneo yasiyofaa ni watu wakawaida sana. Wanaoumuzwa na bei ya sukari, ni watu wa chini; ambao mazao yao yanauzwa kwa bei ya kutupa ni wakulima, wenye kipato kisichotosheleza milo mitatu ni watu wa chini na wameongezeka. Nani atawapa kura? Walioipa CHADEMA kura hawana sababu ya kupungua, ila walioipa kura CCM na rais wao zipo sababu lukuki za kupunguza kura. "Ajidhaniae amesimama aangalie asianguke"
 
OYEE wakati Kila chaguzi mnapigwa chini
polisi+ usalama wa taifa+ jeshi + tume ya taifa ya uchaguzi= ushindi wa kishindo ( ccm oyeeee)
KWANINI JECHA ALIFUTA UCHAGUZI ZANZIBAR? KWANINI COMPUTER ZA KUJUMLISHIA MATOKEO PALE HAKI ZA BINADAMU ZILIPOKWAAAA? vipi mtu yule aliyekimbia na box la kura pale kinondoni na akarudi nalo baada ya nusu saaa? unauita na ule ushindi?
 
Back
Top Bottom