Changia uzinduzi wa kilimanjaro rangers fc

mimimkuu

Member
Oct 12, 2010
38
9
Ndugu wana Watanzania. Kwa kweli Mkoa wetu wa Kilimanjaro umepoteza dira katika michezo ya aina mbalimbali ikiwemo soka. Toka enzi za USHIRIKA kucheza ligi kuu umepotea kabisa na kuacha vijana wengi mtaani kufanya mabo yasiyofaa yakiwemo udokozi, uzururaji na utumiaji wa madawa ya kulevya mf. bangi n.k. Sisi kama vijana wenye malengo chanya ya kutaka kucheza soka katika ligi kuu ya Tanzania, tuna mpango mkakati wa miaka mitatu (3) katika kufanikisha hili. Timu yetu imesajiliwa rasmi September mwaka huu na tumeazimia ndani ya miaka mitatu tucheze ligi kuu, na kwa kuanza tumeshiriki ligi ya wilaya na haya ndio mafanikio yetu.

1. Tumefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali kwa kuzifunga timu za (Railway (2-0), Machava (1-0) na kutoa sare na Bonite (2-2))
2. Katika kundi la robo fainali hadi leo tumetoa sare 2 ( 1-1 na Mvuleni, 4-4 na Soweto na tumebakiza mechi moja itakayochezwa tarehe 9 December na Railway)

Tarehe 12 February tumeazimia kufanya KILIMANJARO RANGERS FC (KRFC) DAY ili kufanikisha yafuatayo;
1. Kueleza mafanikio ya timu toka Kuanzishwa(September 2010)
2. Uchangiaji wa hiyari kwa timu ikiwa ni pamoja na kuendesha mnada
2. Kuzindua tovuti(website) yetu Kilimanjaro Rangers Football Club
3. Kutafuta wafadhili na wadhamini
4. Kueleza mpango mkakati wa kukuza soka mkoani
5. Kueleza vitega uchumi vya timu ili kujikwamua kifedha na kuepuka utegemezi
6. Kusajili wanachama na kugawa kadi za timu kwa mashabiki wetu



Katika siku hiyo tumepanga kuanza kwa maandamano ya soka tukiwa na kauli mbiu ya "Sports and Youth Development" ikiwa na maana michezo na maendeleo ya vijana, tukifuatiwa na tafrija fupi ya uzinduzi wa timu, tovuti na mambo yaliyotajwa hapo juu na kisha kucheza mechi ya kirafiki na timu alikwa.

Hivyo basi tunaomba msaada wa dhati katika kufanikisha hili kwa makampuni, na watu binafsi. Msaada tunaopokea ni pamoja na fedha taslimu, tsheti zenye rangi nyeupe ama bluu, usafiri wa siku hiyo, matangazo (flayers & banners) na USHAURI ili kufanikisha juhudi zetu zilizoanza. Kidogo kidogo hujaza kibaba hivyo usisite kuchangia kwa chochote ulichonacho. tafadhali tumia namba zifuatazao kupata utaratibu wa kuchangia, 0754710465, 0712204205.

Kwa kutumia jina letu kama lilivyo tunataka kuwa mfano bora kwa timu za TANZANIA na kutangaza vivutio vya chi yetu ikiwemo mlima KILIMANJARO ndani na nje ya TANZANIA.

Tuwezesheni tuweze, na hakika hatutawaangusha.

Maoni tunapokea kwenye wall yetu ya FACEBOOK tafuta KILIMANJARO RANGERS (Kilimanjaro Rangers | Facebook)

http://http://www.kilimanjarorangersfc.com/
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom