Changia Mzumbe Onesha Uspecial wako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changia Mzumbe Onesha Uspecial wako!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kilongwe, Jul 29, 2009.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wakubwa nina uhakika kwamba humu ndani kuna idadi kubwa mno ya wazumbe,Na wengi wao wapo kwenye vitengo muhimu ndani na nje ya nji hee(hehehe).
  Sasa nina hii mission,Kwanini tusijiunge pamoja tukasaidia maendeleo ya shule yetu,kuanzia kifedha.kihali na hata kimawazo.Humu ndani kuna watu wa fani tofauti,Kuanzia maprogramer ambao watatutengenezea website,Malawyer wataotupa direction na mamanager watakaotupa mwanga jinsi ya kufanikisha hili.Waalimu watakaokuwa wanajitolea kipindi cha likizo zao kwenda kufundisha.
  Kw mfano huku nje vitabu ni bei murua mno,so tunaweza tukawa tunawatumia hardcopy,Pia nina imani kama kila wazumbe kumi tukajichangisha tukanunua computer moja kw idadi ya Vichwa vilivyopitia MAVI tutapata hata computa mia nne na server kadhaa,then baadae tukadownload vitabu kibao na kuwawekea kwenye Library(Electronic),Mimi binafsi nipo tayari Bureee kwenda kuwatengenezea Intranet ambapo vitabu,tutorials na nondo nyingine zote zitakuwa mumo,Hii ni changamoto tu ambayo mimi binafsi nimefikiria,Nina uhakika watu mutakuja na mawazo kibao katika hili,nini tufanye na nini kina utata,Tulio nje na walio Nyumbani kwa pamoja tukishirikiana tunaweza kulifanikisha hili.
   
  Last edited: Aug 2, 2009
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Poa haya ni mawazo ya kizalendo! Je sisi tuliosoma pengine tunakaribishwa kuchangia?
   
 3. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mkuu wazo lako zuri ila hapo juu umenitatiza. Naona chembe chembe hai za ubinafsi. Kwa nini usiangalie hilo swala kwenye seti kuu ambayo ni utanzania na sio u-mzumbe? Huu ni ubaguzi.
   
 4. A

  Aluta Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Aug 16, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa nini baadhi ya watu wakisoma shule kama Mzumbe wanajiita kama Vichwa; taifa kubwa na kujigamba mbele za watu...kuna watu wanaenda mzumbe na point seven na wanagonga mzinga wa div. two. Je, nao ni vichwa sababu wamesoma Mzumbe? au maana ya kichwa ni nini?
   
 5. L

  Lukundo Member

  #5
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wizi mtupu. uspecial ule wa kukariri. wazumbe, wairiboru, watb boys, na wakilakala, inawezekana kweli walikuwa wazuri kwa mitihani ile ya marudio ya sekondari zetu za tanzania, lakini fuatilia maendeleo yao vyouni ambapo hapakuwa na uspecial, utalia. hata hivyo mtakuwa wachache sana hapa jf kwani kwa asili ma bookworm sio wakosoaji, au wasemea jamii, ni wabinafsi, na watu waoga siku zote,
  sina hakika kama utafanikisha azma yako hapa, kwa sababu hiyo, na kama wapo humu ni waliofrustrate kwa usongo wao kutomeet matarajio yao uraiani,ambao nao kiuhakika hawatakuwa msaada kwako. samahani kwa ujumbe ambao unaweza kukukatisha tamaa, lakini ndo ukweli ambao unabidi kuuzingatia kufanikisha azma yako.
   
 6. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  NImewasikia wakuu,Lengo langu halikuwa baya na ukweli ni kuwa asilimia kubwa ya watu wanaoenda zile shule wana uwezo mzuri darasani ingawa hilo la ubebaji ni kweli na kwa sababu ya mfumo wetu wa elimu.
  Lengo langu lilikuwa ni kutoa changamoto kwa wazumbe kama sisi na endapo kila Shule itakuwa na hari kizi basi tutafika mbali.Sioni cha ubaguzi.
   
 7. B

  Bata Senior Member

  #7
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna mwaka enzi za wibonile(physics ---walikuwa wana maswali ya necta na majibu yake yote ,,loh,nkayachek nilikuwa minaki enzi hizo 2003 nkasema hayatatoka...

  nusu nijiarishie siku ya necta ,yote yalitoka, paper 1,2 na practical.

  <<nahoji--na huu ni usipeshooo>>

  labda wa kukopi na kupesti.
   
 8. B

  Bata Senior Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wote kimya kuhusu mzumbe,,,,,,?
   
 9. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hata Obama alipoanza harakati za kugombea urahisi alipata mapingamizi mengi mno,hao wanaojiita Maniga ndio wlimuita si Mmarekani na si Nigga,Ila baadaye walipoona mambo mwake wakageuka na kuwa mstari wa mbele,
  NINI maana yangu,katika kila movement kuna watu ambao wapo -ve muda woote,sasa hawa kama haupo makini nao wanaweza wakakuvunja moyo na kujiona ni lofa,Binafsi binadamu kama mimi hawezi kunirudisha nyuma na adhma yangu ila anaweza kunisababisha nibadilishe jinsi ya kwenda.Adhma bado ipo palepale na Ukweli bado upo kuwa Mzumbe ilikuwa ni Special na Hili tutalitekeleza,Iwe leo au kesho.
  Tega sikio......Wakuu kama kawaida ni PM kama baadhi mulivyofanya kuangalia tunapanga vp mikakati.
   
 10. B

  Baba Lao Member

  #10
  Aug 1, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15

  Ebu tuondolee hoja za ubinafsi.Watu kama nyie ndo mnaoendeleza fikra za kifisadi.Kwa hoja yako ya kibaguzi ni wazi kabisa kuwa ukiwa kwenye POSITION lazima uweke mbele UBINAFSI.Badilika mwanangu kama si mjukuu wangu
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nimesoma uzumbeni,nimeishi shabaan robert!LAKINI MTOA MADA ANA DHANA ZA KIBABAISHAJI,NA ZA KIBINAFSI!
  ............ananikwaza sana kwakweli,natamani nimshushie tusi!''uspesho ndo nin bwana?''mbona upo kawaida sana na kakompyuta sayansi kako?wenzio kibao wako asia,america,europe,ocenia WE UMEKOMAA NA USPESHO!
  ...........tuondokee bwana
   
 12. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Join Date: Fri Jan 2009
  Location: DAR ES SALAAM
  Posts: 922
  Kwa analysis ndogo tu inaonesha si mtu aliye Serious.Na una muda mwingi wa kubishana na kukaa online kazi kutuma post so utanisamehe mkubwa,sina kamuda hako.


  Waswahili walisema asiyejua maana haambiwi maana.
  Hii ni mission Impossible so lengo limefanikiwa kwa almost 90% .Thanks wachangiaje na washiriki,mada imefungwa kwani sasa tunaenda kwenye utekelezaji!
   
  Last edited: Aug 2, 2009
 13. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #13
  Aug 2, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huo uspecial unamwonesha nani? Wazumbe tupo wengi hapa ila hatupendi tabia za kujigamba namna hiyo. Inaonesha wewe ni mtoto sana na unatutia aibu mno. Lengo la kuchangia ni zuri ila zana ya kuonesha uspecial ni ya kijinga sana. Hapo ofisini kwako nahisi hutapendwa ukiwa hivyo, kama ni mwanafunzi basi una kazi ya ziada kujifunza namna ya kuishi na jamii huku mtaani. Natumaini wazumbe wataendelea kukusaidia kwa mawazo ya kukujenga maana vinginevyo utachanganyikiwa tu huko uendako.
   
 14. B

  Bata Senior Member

  #14
  Aug 2, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  great
   
 15. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2009
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Nakuunga mkono na mguu kwa hii!!
   
 16. l

  lageneral Member

  #16
  Aug 8, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jambo la kuchangia shule na vyuo tulivyosoma ni jambo zuri nalinatakiwa kupigiwa jepuo.Wana wa mzumbe chukueni nafasi hii kuichangia shule yenu.Bravo for this
   
Loading...