diamond d
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 812
- 2,048
Ndugu watanzania, napenda kuanzisha Uzi huu muhimu Kwa maendeleo ya Taifa letu.
Ni kwamba, baada ya miaka mingi kupita, ni miaka hii jiji letu la Dar es Salaam limekuwa likitajwa sasa katika Top 10 tofautitofauti. Mfano:
Imo kwenye Top 10 ya miji mizuri Africa,
Top 10 ya miji inayokua Kwa kasi Africa,
Top 10 ya miji mikubwa Africa na ni mji mkubwa kuliko yote Africa Mashariki na Kati,
Top 12 ya miji tajiri Africa, nk.
Sasa Kama tumeweza kuingia kwenye List hizi, ni wazi kwamba kuna umuhimu wa kumaintain heshima na Sifa hizi.
Watanzania tumekuwa tukiwapuuza Jirani zetu kwamba wanajisifu Sana, nami Leo naungana nao kabisa kwamba vitu hivi tunavyoona si vya msingi ndivyo vinavyovuta watalii, na vinajenga taswira akilini mwa watu kwamba ndivyo ilivyo.
Sasa kwanini kuna umuhimu wa kumaintain Sifa hizi?
Ni kwamba itatufanya tufanye mambo makubwa zaidi ili tusipoteze hadhi yetu ya jiji letu hasa Dar es salaam.
Pia itatufanya tuwe na ukisasa zaidi hasa katika masuala mazima ya majengo na miundo mbinu.
Nchi Jirani wamekuwa wakiji tangaza na hata kujilinganisha na miji mingine mikubwa licha ya kuwa wao ni wakawaida tu.
Sasa Mawazo yangu!
Ni wakati sasa wa kuanza kuwa na majengo Unique, Matefu na makubwa ya kisasa, Barabara zenye ubunifu na ufurahishi inapo bidi.
Tutafute kuwa na majengo marefu Sana ili kuweza kufanya tutamkwe pia midomoni mwa nchi nyingine, na si kwamba sisi tutakuwa wa kwanza kufanya hivi Bali na wenzetu wanawaza hivi pia.
Ipo faida ya kujulikana kupitia sababu hizi tunazodhani ni za kijinga.
NAULIZA SWALI
Je, tumewahi jiuliza ni faida gani tulizo pata kupitia vitu vya kisasa kama vile,
Usafiri wa mwendo kasi,
Uwanja mkubwa wa mpira Afrika mashariki na Kati,
Daraja la kisasa la Kigamboni,
Mfugale Flyover,
Majengo marefu ya sasa Posta nk.
Ikumbukwe siku hizi utalii si tu kuangalia vitu vya kale (Kizamani), wanyama nk, Bali ni pamoja na vitu vizurivizuri na vya kisasa. MF, Dubai yenye majengo marefu zaidi duniani, South Africa nchi yenye miji ya kisasa Africa, Marekani nchi yenye miji mizuri na mikubwa.
Hitimisho:
Tujenge jengo hata moja REFU Sana ikiwezekana kuliko yote yajayo Africa mashariki na Africa Kwa ujumla ili pia tujipatie kujulikana zaidi Africa. Lakini pia ikumbukwe siku hizi lugha ya macho ndio inayo bamba Sana. Yaani Lugha ya Picha.
Mfano wenzetu Kenya, South Africa nk wameplani Kama inavyoonekana pichani;
TUKUMBUKE WENZETU WANAO FANYA HIVI SI WAJINGA, They win Investments kiutani utani. Tusiishie tu vi floor 35, 30, 12 nk. Au vijengo pacha no.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, AMEN.
Thanks.