Changia Mawazo kuboresha mchango wangu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu!

Mkuu HK.
Mbona kabla hamja itikia ile ndiyo yenu itakayo tutoa kamasi hukuja humu kuuliza kuwa tuna maoni gani kuhusu kupitisha bajeti? Unanishawishi kuwa huenda unatafuta P. P (political popularity) kupitia hapa jf.
Mlisha chagua kujitenga na sisi kwa kupitisha bajeti mbovu.
Kama rafiki, nakuomba ufuate mkuu Invisible alicho kushauri hapo juu ila umenidisappoint sana kaka!
 
HK ushapanga kuunga mkono hoja 100%, umekuja hapa kutuzuga na kutuchosha tu, tangu lini magamba mkafuata ushauri wa watanzania, mnachojua nyinyi ni uchoyo na ulafi tu
 
Kigangwalla,
Hapa JF kuna mawazo lukuki nawe ni mwanachama sidhani kama hujadonoa hata 10 hadi sasa.

Unaweza kupata mawazo 99, tatizo ni kuwa hutaweza kuyafikisha kwa utimilifu wake kwasababu umefungwa mikono na kamba zinazoitwa CCM. La sivyo ningeweza kjapo kusema umuulize waziri mkuu haya

1. Deni la Taifa limeongezeka zaidi ya mara mbili.
a) Ni miradi gani ya kitaifa iliyoongeza deni hilo
b) Bunge kama chombo cha uwakilishi kilihusishwa vipi katika kuamua ukopaji huo?

2. Kwa vile serikali ina mkakati wa kubana matumizi na kufuatilia matumizi mabaya ya fedha
a) Ni kiasi gani cha fedha kimetumika kwa mwaka uliopita kwa safari za viongozi wa juu nchini akiwemo Rais

3. Ni nini matokeo ya uchunguzi wa kampuni za KAGODA, MEREMETA, TANGOLD na KIWIRA

4. MKURABITA NA MKUKUTA Zimefanikiwaje kupunguza umasikini nchini
 
Kutaka ushauri ni moja na kuufuata huo ushauri ni suala jingine kabisa ambalo hata halihusiani na lile la kwanza!
Hii ndio changamoto.....
Binafsi ningeamini utakaso wako kama kweli JF ingekuwa sehemu yako ya kuchota ushauri, kama ungetushirikisha toka siku ya kwanza kabla hamjapiga kura za "ndiyooo".....

Kila siku tunawaambiaga kuwa nyie ni makini zaidi ya hapa ila mmeamua tu kujitoa akili...
Ila mnasahau kuwa sisi tulio nje ya GAME tunawaona vizuri zaidi...!

Tujenge nchi tuache maigizo ya kupeleka mambo "kama kawaida"

Ukweli ni kuwa mmezingua toka hatua ya kwanza, kwa mara nyingine mmeendelea kuliumiza taifa kwa michezo yenu ya "kama kawaida".....

Huna unachoweza kufanya tena Mkuu sababu utamalizia kwa kusema "naunga mkono kwa 100%".....
 
Ndg zangu, nataraji kupata fursa ya kuhutubia bungeni kwenye bajeti ya ofisi ya waziri mkuu iliyowasilishwa leo, hapa tutapata fursa ya kusema lolote la kisera na hata la kijimbo, kama mlivyoshuhudia leo wachangiaji wa mwanzo walivyoanza.

Jina langu ni la 34 kwenye orodha ya wachangiaji hivyo nina matumaini makubwa ya kupata nafasi ya kuchangia endapo orodha hii itafuatwa kama ilivyo. Naomba mawazo ya nini unadhani ni nyeti sana na ungependa kisemewe na wabunge?

Nitatoa fursa kwa watu watakaonipa issue nyeti na zenye mantiki na hususan zilizokaa kitaifa zaidi. Kwa wale wa Nzega na hata Tabora kwa ujumla, mnakaribishwa kunipa issue za Kijimbo, kiwilaya ama hata kimkoa ili nizisemee bungeni.

wakatabahu,
HK.
Mkuu HK, binafsi nimependa jinsi umegeuka na kuwa humble and down to earth all over a sudden, kufikia kiasi cha kujishusha na kutaka mawazo yetu, hii move ni ++ on your side, nakupongeza kwa hili.

Kwa hizo dakika zako 10, mpaka hapa, naamini you have more than enough, ushauri wangu kwako ni just "be genuine!, be yourself"!.

Nimefurahishwa sana na the boldness in you uliionyesha kwenye yale maandamano yako, kama ni kweli ulikuwa genuine and its yourself, then "be it " hata katika michango yako bungeni, licha ya kuwa uko CCM, ukiweka maslahi ya "watu" mbele, with genuinity na honest, chochote utakachokisema, hata kama ni kwa dakika moja tuu, kita matter most na kitakuwa na very big impact kwetu ambayo kwako itakuwa ndio ngazi ya kupandia kuifikia runway ready to fly!.
 
Nitakuona wa maana sana kama utapinga swala la nyie wabunge kuongezewa/kujiongezea mshahara hadi milioni kumi kwa kazi yakwenda kugonga meza nakusinzia bungeni huku walimu wakitaabika na mishahara duni pa1 na mazingira magumu ya kazi,Madaktari wakiendelea na migomo baada yakuchoshwa na udhaifu wa Mkuu wa kaya,ugoigoi wa ccm pamoja na uzembe wa Bunge...Ina maana na haya hadi uambiwe!!
 
Daktari Kingwangallah, huna jipya ni heri ukubali kufa na madaktari wenzako ambao watakupokea kama itatokea Hussein Bashe akakuzidi tena maarifa kwenye kura za maoni.

Ubunge ni kazi ya kupita tu lakini ukumbuke wewe ni Daktari wakikuheshimu na kukubali madaktari wenzako ni heshima kubwa, usiwe na akili za panzi kama za Margreth Sitta aliyewasaliti Walimu wenzake baada ya kukaa kwenye high table.
 
Dr. mimi siipendi ccm, ila kwa hili nakupongeza. Nikiwa kama mtumishi wa serikali nimegundua mambo makubwa matatu yanayofanya budget yeti isitekelezeke.
1. Budget inayopitishwa hailetwi kama ilivyopangwa. Kwa mfano unakuta mpaka mwisho wa mwaka wa fedha ni asilimia 52% tu imeletwa na sehemu kubwa ya hiyo pesa inakuwa ni oc. Sasa unaleta oc bila kutoa fedha za miradi matokeo yake oc inatumiwa kwa shuguli nyingine za kiofisi zilizopangwa kwenye budget, mwaka unaisha na siku zinaenda.
2. Miradi mingi inayopitishwa inacheleweshwa kutengewa pesa, matokeo yake wizara zinatumia muda mwingi kutoa semina kwa watendaji ambao mpaka miradi inaletwa wanakuwa wameshahamishwa au kustaafu, au kwenda masomoni. ni vema semina ziwe zinatolewa pale ambapo pesa za miradi zimepatikana.
3. Mifumo ya halmashauri inaruhusu watendaji wengi kula pesa badala la kusimamia miradi. Bajeti inapitia sehemu nyingi kabla ya kupitishwa, vikao vingi sana.
Ni hayo tu kwa leo, nikipata nafasi nitaandika mengine!!!!
 
Iundwe tume huru ya bunge kuchunguza chanzo cha mgomo wa madaktari na kuchunguza iwapo kauli za waziri mkuu zinahusika na kuchochea mgomo kati ya madaktari na ukweli wa kauli zake jinsi wanajitahidi kuupunguza mgomo.

Selikali ifikie hatua iseme imefanyanini kupunguza mvutano na wafanyakazi na iwe wazi mishahara mikubwa na posho kubwa kwa wabunge inawaongezea mvutano na wananchi
 
ushauri wako mzuri, umeonesha unafuatilia mambo, lakini style yako ya kunifikishia ujumbe sasa...

mi naona staili nzuri tu,,,nyie wabunge si mmeamua kutukomoa bhana,,,,,mnajua kabisa mnachokifanya si kizuri pale bungen lakini mnatukomoa dr Kigwa,mnatufanyia kusudi kabisa,kuna mambo mnayoyapitisha pale kwakweli hayafai na mmeamua kutukomoa,kwakua mnajua mtakaa miaka 5 bila sisi kuwagusa,na unajua kuwa raia wana hasira na nyinyi kwa upuuz unaoendelezwa na nyinyi
 
Iundwe tume huru ya bunge kuchunguza chanzo cha mgomo wa madaktari na kuchunguza iwapo kauli za waziri mkuu zinahusika na kuchochea mgomo kati ya madaktari na ukweli wa kauli zake jinsi wanajitahidi kuupunguza mgomo.

Selikali ifikie hatua iseme imefanyanini kupunguza mvutano na wafanyakazi na iwe wazi mishahara mikubwa na posho kubwa kwa wabunge inawaongezea mvutano na wananchi

mdau tume hizi ndo zinazotuingiza kingi na matumizi makubwa yasiyo na tija,,,,ukumbuke tuna mzigo wa TUME YA KATIBA
 
Daktari Kingwangallah, huna jipya ni heri ukubali kufa na madaktari wenzako ambao watakupokea kama itatokea Hussein Bashe akakuzidi tena maarifa kwenye kura za maoni.

Ubunge ni kazi ya kupita tu lakini ukumbuke wewe ni Daktari wakikuheshimu na kukubali madaktari wenzako ni heshima kubwa, usiwe na akili za panzi kama za Margreth Sitta aliyewasaliti Walimu wenzake baada ya kukaa kwenye high table.
Mkuu Matola, huyu HK aliyepo sasa siye tena yule aliyeshindana na Bashe ndani ya CCM na hata baada ya ushindi, jinamizi la Bashe kuendelea kumtesa hivyo kumfanya aishi nyuma ya kivuli cha Bashe!. HK huyu wa sasa ni HK mpya ambaye amepata self realization kuwa kuwa hata kama amepita kwa tiketi ya CCM, lakini baada ya kuchaguliwa, yeye sasa ni mtumishi wa watu na sio mtumishi wa CCM!. Jukumu lake kubwa ni kuwatumikia watu wote wa Nzega, waliomchagua na wasio mchagua, wana CCM na wasio wana CCM!. Ameisha ukubali ule ukweli mchungu kuwa "Now CCM doesn't anymore", kinachomata sasa ni huduma yake kwa jamii yake na sio CCM tena!.

Mimi nimemuunganisha huyu HK wa sasa kwenye kundi la kina Deo Filikunjombe, la kusimama na kuhesabiwa!. Kwa msimamo wake wa sasa, mbele ya HK wa sasa, Bashe is nothing!. CCM ni chama kongwe na rushwa is the order of the day ndani ya CCM, msomali ameishaitandaza kisawasawa, hivyo CCM sasa ndio wanamhujumu HK ili 2015 wapate ground na justification ya kumtema na kumpitisha kipenzi chao Bashe!. HK ameshaona mbali, and he banks with the people who matter most, and by that time, kusimama kuwatumikia wananchi, sio lazima kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo HK akishikilia msimamo wake wa kusimama na wananchi, wana Nzega, watasimama nae, Bashe na CCM yake, down the drain, watakwenda nayo!.
 
Ungekuwa ume-spend muda wako kumshauri mbunge ungekuwa umefanya la maana sana kuliko kumwaga haya matusi yote yasiyo na tija. badaya ya kumuonyesha kuwa yeye ni mjinga kinyume chake wewe umeweka wazi ujinga wako sasa

bado tu mtu akisema ukweli anaambiwa anatukana jamani,,,,,hayo aloshauriwa pia ni ushauri we ulitaka asemeje????hakuna tusi amempa za uso na huo ni sehem ya ushauri
 
Je kwanini isiundwe tume ya bunge kuutafute ukweli juu ya kauli zinazokinzana kati ya madaktari na waziri mkuu. Kama waziri mkuu kadanganya basi awajibishwe mtu mmoja waziri mkuu hawezi kuwa muhimu kuliko wagonjwa na madaktari wote

tusitegemee sheria hizi zinazowabana wanyonge kuweza kuwabana madaktari wanachotaka ni kuanza kupuuzwa kwa maamuzi ya mahakama na hii ndio hatua ya juu ya mapinduzi
 
Mkuu Matola, huyu HK aliyepo sasa siye tena yule aliyeshindana na Bashe ndani ya CCM na hata baada ya ushindi, jinamizi la Bashe kuendelea kumtesa hivyo kumfanya aishi nyuma ya kivuli cha Bashe!. HK huyu wa sasa ni HK mpya ambaye amepata self realization kuwa kuwa hata kama amepita kwa tiketi ya CCM, lakini baada ya kuchaguliwa, yeye sasa ni mtumishi wa watu na sio mtumishi wa CCM!. Jukumu lake kubwa ni kuwatumikia watu wote wa Nzenga, waliomchagua na wasio mchagua, wana CCM na wasio wana CCM!. Ameisha ukumbali ukweli mchungu kuwa kinachomata sasa ni huduma yake kwa jamii yake na not CCM anymore!.

Mimi nimemuungani huyu HK wa sasa kwenye kundi la kina Deo Filikunjombe, la kusimama na kuhesabiwa!. Kwa msimamo wake wa sasa, mbele ya HK wa sasa, Bashe is nothing!. CCM ni chama kongwe na rushwa is the order of the day ndani ya CCM, msomali ameishaitandaza kisawasawa, hivyo CCM sasa ndio wanamhujumu HK ili 2015 wapate ground na justification ya kumtema na kumpitisha kipenzi chao Bashe!. HK ameshaona mbali, and he banks with the people who matter most, and by that time, kusimama kuwatumikia wananchi, sio lazima kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo HK akishikilia msimamo wake wa kusimama na wananchi, wana Nzega, watasimama nae, Bashe na CCM yake, down the drain, watakwenda nayo!.
sioni mantiki ya ccm na wadau hapa kumpigia chapuo huyo msomali wao,,,bashe si mtanzania its ova,BASHE NA RAGE SI WATANZANIA,WAENDE BAIDOA HUKO NA MOGADISHU WAKAENDESHE SIASA,,,,,,
 
Je kwanini isiundwe tume ya bunge kuutafute ukweli juu ya kauli zinazokinzana kati ya madaktari na waziri mkuu. Kama waziri mkuu kadanganya basi awajibishwe mtu mmoja waziri mkuu hawezi kuwa muhimu kuliko wagonjwa na madaktari wote

tusitegemee sheria hizi zinazowabana wanyonge kuweza kuwabana madaktari wanachotaka ni kuanza kupuuzwa kwa maamuzi ya mahakama na hii ndio hatua ya juu ya mapinduzi

willie nimekueleza hapo juu tume ni gharama,,,tume ya nini kaka,????tunapoteza hela na kuwanufaisha wachache mdau
 
ushauri wako mzuri, umeonesha unafuatilia mambo, lakini style yako ya kunifikishia ujumbe sasa...

ss ww hapo unakose kidogo, ulitaka KUPATA maoni ya watu, sio KUTEST wanaofuatilia bunge, hebu na ww badili attitude, uwe mbunge msikivu, utafika mbali.
Bahati haya ni maandishi utayarudia upate point, imagine ingekuwa ni maongezi ya mdomo, tayari ungeshayakosa.
Majibu yako yamenikwaza.
 
Ndg zangu, nataraji kupata fursa ya kuhutubia bungeni kwenye bajeti ya ofisi ya waziri mkuu iliyowasilishwa leo, hapa tutapata fursa ya kusema lolote la kisera na hata la kijimbo, kama mlivyoshuhudia leo wachangiaji wa mwanzo walivyoanza.

Jina langu ni la 34 kwenye orodha ya wachangiaji hivyo nina matumaini makubwa ya kupata nafasi ya kuchangia endapo orodha hii itafuatwa kama ilivyo. Naomba mawazo ya nini unadhani ni nyeti sana na ungependa kisemewe na wabunge?

Nitatoa fursa kwa watu watakaonipa issue nyeti na zenye mantiki na hususan zilizokaa kitaifa zaidi. Kwa wale wa Nzega na hata Tabora kwa ujumla, mnakaribishwa kunipa issue za Kijimbo, kiwilaya ama hata kimkoa ili nizisemee bungeni.

wakatabahu,
HK.

Kaka,kwanza nikupongeze kwa kuwa muwazi kutafuta mawazo ya wengine pia bila kujali vyama vya wanao kushauri.pia pole kwa kuwa kwenye Chana chenye mtazamo wenye mashaka.lakini jikite eneo la afya naamini unalijua, madaktari wanalipwa vibaya ukilinganisha na kazi Yao.

Mazingira ya kazi Yao si mazuri(uwe na takwimu ya uhisiano wa madaktari na wagonjwa) uwe na kiwango sahihi cha nini walipwe na kwa sababu gani ilimtunga sera awe na kitukamili.

Medical specialists niwachache mno,jengea hili hoja nini kifanyike kuwanao wakutosha anzia hapa watu wote kwa namna moja au nyingine lazima wa wawaone wataalamu hawa.Ila siku nyingine weka wazi mnafanyaje maamuzi ya hoja zenu ilitukushauri vizuri.
Kama unaweza ni Pm namba yako nikupe hoja za kusimamia kwenye sekta zingine.
Asante
 
Back
Top Bottom