Changia Mawazo kuboresha mchango wangu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changia Mawazo kuboresha mchango wangu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HKigwangalla, Jun 25, 2012.

 1. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ndg zangu, nataraji kupata fursa ya kuhutubia bungeni kwenye bajeti ya ofisi ya waziri mkuu iliyowasilishwa leo, hapa tutapata fursa ya kusema lolote la kisera na hata la kijimbo, kama mlivyoshuhudia leo wachangiaji wa mwanzo walivyoanza.

  Jina langu ni la 34 kwenye orodha ya wachangiaji hivyo nina matumaini makubwa ya kupata nafasi ya kuchangia endapo orodha hii itafuatwa kama ilivyo. Naomba mawazo ya nini unadhani ni nyeti sana na ungependa kisemewe na wabunge?

  Nitatoa fursa kwa watu watakaonipa issue nyeti na zenye mantiki na hususan zilizokaa kitaifa zaidi. Kwa wale wa Nzega na hata Tabora kwa ujumla, mnakaribishwa kunipa issue za Kijimbo, kiwilaya ama hata kimkoa ili nizisemee bungeni.

  wakatabahu,
  HK.
   
 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Mkuu tuseme hujui wananchi wako walicho kutuma bungeni? Unafikiri ng'ombe anaweza kunenepa siku ya mnada?. Yakupasa kujua matatizo ya wananchi wako na kuwasilisha mawazo yao Bungeni sio mawazo yako. Hapo ndo ccm mnakosea, mnakosa kuwasilisha matatizo ya wananchi nmawasilisha mawazo yenu. mia
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  wewe bana ulishaunga mkono lile bomu last week.. budget mbovu haijawahi kutokea, kwasasa kaa kimya kwakuwa wewe ulishiriki kikamilifu kupitisha lile janga..


  -matatizo ya wawekezaji ktk secta ya madini hukuyaona,

  -misamaa ya kodi wanayopata wawekezaji hukuona ni tatizo,

  -vyanzo vikuu vya mapato kutegemea soda na pombe hukuona ni tatizo,

  -kuongeza mshahara na PAYE juu zaidi hukuona ni tatizo,

  -marejesho ya mafanikio ya budget iliyopita hukuona ni tatizo

  -kupunguza budget ya wizara ya afya na elimu hukuona ni tatizo

  -kilimo kwanza kutengewa budget ndogo hukuona ni tatizo wakati ukijua fika % kubwa ya watanzania tunategemea kilimo

  ukaunga mkono hoja kwa NDIYO ya kishindo kama lusinde
   
 4. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Pole. Hujui demokrasia ya uwakilishi kwenye vyombo vya kufanyia maamuzi ikoje, take time to learn and then you will come back to this thread!
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Muafaka kuhusu umeya na madiwani wa Arusha, Mauaji ya raia yanayohusiana na siasa na mgomo wa madaktari
   
 6. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  ushauri wako mzuri, umeonesha unafuatilia mambo, lakini style yako ya kunifikishia ujumbe sasa...
   
 7. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  1: Serikali ihakikishe hospitali ya taifa ya muhimbili inakuwa na vifaa vyote vikubwa vya kisasa vya kuchunguza ugonjwa na ihakikishe inakuwa na wataalam mabingwa wakutosha ili wananchi wengi wahepukane na gharama za kutibiwa nje ya nchi.
  2: hospitali za mikoa ziboreshwe kwa kupatiwa pia vifaa vya kisasa
  3: madaktari na manesi waboreshewe masilai yao.
   
 8. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #8
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  I only have 10 precious minutes, hivi haya yana tija kweli?
   
 9. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #9
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Kwanza,

  Tembelea hii thread inayohusu mkoa wenu, acha pumba; kuna mchele humo, fanyia kazi yale muhimu.

  Wakati ukiwasilisha mchango wako, weka kando itikadi za kichama, zipitie vema hoja alizowasilisha Mbowe, nakusihi sana, usiziite "rubbish" maana itaku-cost sana. Ameongea mengi ya msingi, wewe waweza chagua kama mawili hivi, ukayavalia njuga.

  Tulimtuma January Makamba, sasa hana meno tena! Sasa nikutume, hoja ya "nyumba za kupanga" haina mpinzani wala mtawala, watanzania wanaendelea kuumia na taifa linakosa mapato!

  Niendelee?
   
 10. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #10
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Ukiwa kiongozi, lazima uwe na ngozi ngumu - Kikwete
   
 11. B

  Bob G JF Bronze Member

  #11
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  HKigwangalla,

  Mgomo wa Madaktari inaonyesha serikali haikushughulikia vizuri Madai ya madaktari, kama tulivowasikia Channel 10, Serikali inapandikiza chuki kwa madaktari kukwepa wajibu wake muhimu kabisa, Huduma za afya zimekua zikidhoofu siku hadi siku hakuna madawa hata Drip za Maji, Orksijen hakuna, na hata kutumia 7bn kutibu watu nje ya nchi na 5bn zihudumie hospitali 5.

  Hii haikubaliki kabisa. 2. Huu ni ushauri kwako utakapochangia changia hoja uliyo ingia nayo bungeni, usiokote hoja ndani ya bunge kama wengi wenu walivochangia, watanzania wamechoka na MIPASHO
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Matatizo yetu ni yale yale.. Umaskini, Ujinga na Maradhi..Kusahau maadui hawa na kujaribu kuiejenga nchi kiuchumi wakati wananchi wake ni maskini na wajinga ndio sababu ya kunawaliwa kiuchumi maana sisi wenyewe hatuwezi - hatuna mtaji wala elimu ya kuwezesha amaendeleo hayo. Turudi ktk basic UMASKINI, UJINGA na MARADHI yawe vipaumbele ya majeti nzima laa sivyo tutaendelea kupiga gwaride palepale.
   
 13. Top Thinker

  Top Thinker Senior Member

  #13
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Asante sana narubongo. Huyu jamaa kama kweli ni mzalendo from the heart basi roho yake itamsuta sana kwa kusema ndioooo kwenye lile bomu walilolipitisha.
   
 14. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #14
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hoja ya nyumba za kupanga kwani imekaaje? What is the catch?
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Pinda kawadanganya madaktari, sasa wamegoma na wagonjwa wanateseka siyo tija?
   
 16. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #16
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ebu tuambie kwanza we umejipanga kuongelea nini ili tujue pa kuanzia
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Hii ni ngumu kwako mkuu wangu, I know! ZZK can take care of it...

  Ushauri wangu, capitalize kwenye sekta ya afya! You fit there, play your cards well. Ukizingatia maslahi ya watanzania basi elewa una support yangu 100%.

  Wabunge waache kucheza siasa pasipohitaji siasa, it's your time to shine politically, kuwa tayari kutokueleweka ikibidi lakini ni wakati muafaka wa 'kutema cheche' na kuwafungua macho wabunge wenzako na tuyanusuru maisha ya watanzania.

  I'm pretty sure kuwa dk 10 ukizitumia effectively zinaweza kuleta mabadiliko makubwa kwako na kwa taifa.

  I insist: Taifa kwanza!
   
 18. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #18
  Jun 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa hajui issue ya nyumba za kupanga au anatania?

  Mh. Ongea na Januari kuhusu hili nami naongezea la uwajibikaji serikalini na mrudishe azimio letu la KIJENGE.
   
 19. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #19
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  I couldnt agree more
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Jun 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kama ulikuwepo kwenye kipindi cha maswali na majibu asubuhi ya last wk.. sikumbuki siku NB: rejea maswali ya wenje,,, (aliuliza kuhusu sheria za kulipa pango, alitaka kujua ni kwanini sheria ya zamani isirudishwe, govt kumonitor mikataba ya mpangaji/mwenyenyumba) etc waziri alijibu.. nadhani utakuwa umeshakumbuka mpk hapo
   
Loading...