Elections 2010 Changia Maendeleo ya Tanzania - Changia Chadema

Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
124
Changia CHADEMA kwa kutuma neno "CHADEMA" kwenda 15710 (Zain na Voda tu)

Hili si jipya jamani ila nimeona tukumbushane kidogo kuwa nguvu zetu zinahitajika hata kama ni kidogo kidogo kuweza.

Naona siku za karibuni malaria na mwenzie wako busy sana na vyama vyao vya kijamaa!


Makadirio ya Bajeti ya Uchaguzi Mkuu 2010
CHADEMA inakadiria kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 itatumia kiasi kisichozidi bilioni tano; kiwango ambacho kitahusisha kampeni zote za chama kwa ujumla wake kuanzia kwenye udiwani, ubunge na urais kwa matumizi yote ya uteuzi ndani ya chama pamoja na kampeni zenyewe.

Hata hivyo, Chama hakina kiasi hicho cha fedha na mikakati inaendelea kuandaliwa na kutekelezwa kwa ajili ya kukusanya fedha kwa wanachama na wapenzi.
 
SHALO ndugu yangu ? Unajua watu kama Akina MALARIA SUGU hawaepukiki katika jamii. Wewe tazama hata hujamaliza kuandika meseji yako kasha anza maswali yasiokuwa na kichwa!
 
Transparency ni kitu muhimu sana, kwanini toka ianze michango kwa njia ya simu zimeshapatikana Tsh ngapi?
 
Mbowe na Komu watatajirika zaidi mwaka huu. Uzuri wa CHADEMA, hata Mbowe akiiba wala haitwi fisadi maana anakuwa anachukua profit kutoka lichama la baba mkwe.
 
To be honest hii kitu ni biashara nzuri sana.. Bulicanas haiwezi gusa hapa wala Aishi Hotel. Mwisho wa siku watu watafanya wafanyavyo lakini watakao tajirika na Upinzani (T) Ltd. ni viongozi wa juu na CCM ambao wanahakikisha hawa mbuzi bado wanabaki too weak to gain real power..so sisimizi anakula kidogo na Nyangumi nae anakula portion kubwa... And the wheels on the... go round and round.. round and round...
 
Swali kwa Mods, vyama vingine vinaruhusiwa kuchangisha JF?

Hujaelewaka..Hapa ni sehemu neutral na Kulikuwa na sredi za kuchangia CCM na kujiunga na CCJ kwa njia ya simu..Hata wewe kama unachako unaruhusiwa kuanzisha sredi hapa....
 
wapendwa

Kama unaweza changia usisite changia kadri uwezavyo!
 
Hii nime copy na kupaste toka tovuti ya chadema. Kwa wale wasiofahamu.




Sifa na Masharti ya Mgombea Ubunge​
rt.bevel.gif
Je? Watumishi wa Umma wanaruhusiwa kugombea?
Soma zaidi..
lf.bevel.gif
rt.bevel.gif


Sifa za mgombea Ubunge

  1. Awe raia wa Tanzania​
  2. Awe na umri wa miaka 21 au zaidi​
  3. Awe ni Mwanachama na ni Mgombea iliyependekezwa na Chama cha Siasa​
  4. Awe hajatiwa hatiani na Mahakama yoyote kwa kosa la kukwepa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi​
  5. Awe anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza​


Kupoteza sifa za kuwa mgombea

Kwa mujibu wa Ibara ya 676(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, hata kama mtu ana sifa zote za kugombea hataruhusiwa kugombea Ubunge kama:-
  1. Ni raia wanchi nyingine; au
  2. Kwa mujibu wa Sheria inayotumika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitishwa rasmi kwamba mtu huyo ana ugonjwa wa akili; au
  3. Amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au
  4. Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma;
  5. Siyo mwanachama na siyo mgombea aliyependekezwa na Chama cha Siasa;
  6. Ikiwa mtu huyo ana maslahi yoyote katika mkataba wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa aina yoyote iliyowekewa miiko maalumu kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapo a mekiuka miiko hiyo;
  7. Ameshika madaraka ya Afisa Mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais anaweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, au Sheria iliyotungwa na Bunge;
  8. Kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge inayoshughulikia makosa yanayohusika na Uchaguzi wa aina yoyote, mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura au kupiga kura katika Uchaguzi wa Wabunge;
  9. Ni mgombea Urais au Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Masharti ya Mgombea

  1. Awe amedhaminiwa na wapiga kura wasiopungua 25 waliojiandikisha kupiga kura katika jimbo hilo
  2. Awe na dhamana ya Shilingi Elfu hamsini (50,000/=)
  3. Awe amekula kiapo mbele ya Hakimu kwamba anazo sifa zinazotakiwa ili kugombea Ubunge
 
You guys are jokers.

Mnataka mchangiwe bila kuonesha mchanganuo?

Uswahili tuuuuuu
 
Kuchangia ni vizuri na tunaviwezesha vyama vyetu, lakini tatizo ni namna hizo pesa zinavyotumika ni vyema vyama vikatangaza kiasi kilichopatikana na matumizi yake. Vyama vikifanya hivyo vitarudisha imani kwa wachangiaji na uchangiaji utaongezeka.
 
Back
Top Bottom