Elections 2010 Changia kesi dhidi ya Mahanga vs Mpendazoe

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
View attachment Changia Kesi.pdf

Ndugu watanzania wapenda haki, leo nimepata tangazo ambalo liko katika gazeti la Tanzania Daima. Ndugu yetu, mbunge wa jimbo la Segerea ambaye kura zake zilichakachuliwa, Mh. Mpendazoe amekuombeni kusaidia kuchanga fedha kwa ajili ya kesi aliyofungua kwa niaba ya wananchi wa Segerea dhidi ya Makongolo Mahanga.

Unaombwa uchangie maana wote tunajua kuwa demokrasia ina gharama zake. Nakushukuru kwa mchango wako.

Mungu akubariki

Mimi Quality
 
Asante kwa taarifa na nshachanga faster kwa jili ya mabadiliko ya ukweli Tanzania
 
hatuchangii waharifu, atafanyaje kazi na majambazi hadi wanashea usafiri, labda tuwasaidie polisi kumtia hatiani yeye na majambazi wenzake
 
Kama wewe huchangii kwani lazima ututaarifu wengine watachangia? Jamani ustaarabu mbona unatushinda. "Better remain silent and be thought a fool, than speak out and remove all doubt"
 
nitachangia yoyote anayetetea haki

Fred ntakuchangia, na hata wa CCM wanaoona haki yao imeppokwa

Acid
 
hatuchangii waharifu, atafanyaje kazi na majambazi hadi wanashea usafiri, labda tuwasaidie polisi kumtia hatiani yeye na majambazi wenzake

Mh!mbona unaenda mbali sana!imekuuma sana,pole mkuu!sisi tutamchangia!
 
Huyu Mpendazoe alimuiga Augustine Mrema, akapiga kelele bungeni, akajitoa CCM akifikiri atagombea urais Chama cha Jamii matokeo yake kajikuta anahangaika, siasa hesabu. Asingejitoa CCM leo si angeendelea kuwa mbunge, mwacheni aendelee kuumia
 
mpendazoe usikate tamaa segerea ni jimbo lako, tunaaminia kaza buti, zap yangu itaingia, i promisi 15,000
 
hatuchangii waharifu, atafanyaje kazi na majambazi hadi wanashea usafiri, labda tuwasaidie polisi kumtia hatiani yeye na majambazi wenzake

Hakuna ujambazi unaozidi aliyeiba kura halali za watanzania, na anajiona sio mwizi. anataka watu wenye vichwa-zero kama wewe ili wawatawale maisha yao yote!

Kama unashindwa kutambua kuwa Mpendazoe kawekwa ktk target tu ya kwamba anatumia gari 'inayohisiwa ya wizi' kama njama za hao manyang'au, wezi wa kura ambao wameiba ubunge wa Segerea na wanaogopa kesi iliyo mahakamani.
Utambue kuwa dawa ya moto ni moto. Ujanja wa kutumia polisi ili kuyumbisha upatikanaji wa haki ni kufillisika. Ndio CCM ipo hapo.

Fred tutamchangia, jimbo litarudi kwa washindi halali, na huyo 'naibu waziri' feki na fisadi wa elimu atarudi mtaani kumiliki baa zake alojenga kwa kukwapua viwanja vya wazi na maeneo ya kuchezea watoto.

Inatia hasira sana kuona mijitu inatetea uozo na hawana fikra halisi.
 
wewe kama nani? Au unataka tukuchangie wewe?

Ahsante kwa maneno yako mazuri. Taarifa hii ni ile ile iliyokuwa katika gazeti la Tanzania Daima Uk 3. So haunichangii mimi. Lakini unaweza kumpigia katika simu zilizoko katika gazeti na kupata maelezo zaidi. Ahsante sana
 
Kama wewe huchangii kwani lazima ututaarifu wengine watachangia? Jamani ustaarabu mbona unatushinda. "Better remain silent and be thought a fool, than speak out and remove all doubt"

Nimekumbuka msemo wa Robot/invisible.
 
Hakuna ujambazi unaozidi aliyeiba kura halali za watanzania, na anajiona sio mwizi. anataka watu wenye vichwa-zero kama wewe ili wawatawale maisha yao yote!

Kama unashindwa kutambua kuwa Mpendazoe kawekwa ktk target tu ya kwamba anatumia gari 'inayohisiwa ya wizi' kama njama za hao manyang'au, wezi wa kura ambao wameiba ubunge wa Segerea na wanaogopa kesi iliyo mahakamani.
Utambue kuwa dawa ya moto ni moto. Ujanja wa kutumia polisi ili kuyumbisha upatikanaji wa haki ni kufillisika. Ndio CCM ipo hapo.

Fred tutamchangia, jimbo litarudi kwa washindi halali, na huyo 'naibu waziri' feki na fisadi wa elimu atarudi mtaani kumiliki baa zake alojenga kwa kukwapua viwanja vya wazi na maeneo ya kuchezea watoto.

Inatia hasira sana kuona mijitu inatetea uozo na hawana fikra halisi.

Tupambane daima, tuungane, si kwa kesi ya Fred pekee bali popote ambapo unyang'au umefanyika kuiba haki na ushindi, kesi za kupinga matokeo ni lazima kufanywa na haki kupatikana
 
Tuko tayari kumchangia. Sasa kuna account number au namba ya simu, tuwekeeni hapa tuchangie.

kuchangia, tumia njia zifuatazo:
(i) Akaunti namba 010-00263962 Benki ya posta- Mpendazoe & Friends
(ii) M-Pesa simu namba 0762 926556
(iii) Zap simu namba 0787 638575 na
(iv) Tigo pesa simu namba 0717 050335 au 0656 650334
 
Hakuna ujambazi unaozidi aliyeiba kura halali za watanzania, na anajiona sio mwizi. anataka watu wenye vichwa-zero kama wewe ili wawatawale maisha yao yote!

Kama unashindwa kutambua kuwa Mpendazoe kawekwa ktk target tu ya kwamba anatumia gari 'inayohisiwa ya wizi' kama njama za hao manyang'au, wezi wa kura ambao wameiba ubunge wa Segerea na wanaogopa kesi iliyo mahakamani.
Utambue kuwa dawa ya moto ni moto. Ujanja wa kutumia polisi ili kuyumbisha upatikanaji wa haki ni kufillisika. Ndio CCM ipo hapo.

Fred tutamchangia, jimbo litarudi kwa washindi halali, na huyo 'naibu waziri' feki na fisadi wa elimu atarudi mtaani kumiliki baa zake alojenga kwa kukwapua viwanja vya wazi na maeneo ya kuchezea watoto.

Inatia hasira sana kuona mijitu inatetea uozo na hawana fikra halisi.

Hapo umelenga. Kwa sasa anaitwa "mtaalam wa open space". Katika jimbo la Segerea, anaongoza kwa kuvamia maeneo ya wazi. Wengi mtakuwa mnajua Nyantale ...
 
Tuwekee wazi jinsi ya kuchangia. Wenye akili fupi bado wanaamini dhuluma inaweza kutawala ulimwengu daima. Si kweli. Mwisho wake ukweli utashinda na huyo Mahanga kama hijui mwisho wake hauko mbali
 
Hivi bado ipo ile sheria sijui ukitaka kupinga matokeo ya ubunge unatakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 15?

Naomba kuelimishwa
 
Back
Top Bottom