Changia CHADEMA Kupitia No 15710, Kuwa Sehemu ya Ukombozi

harakati gani za ukombozi mkuu. Ukombozi wa kuwajaza ndg zao na watoto kwenye ubunge viti maalum.

Nakuunga mkono mkuu.
Tatizo una udogo wa mawazo. Swali kubwa la kujiuliza, kwani chadema hawakutumia vigezo kuteua wabunge? Hebu hesabu ccm wako watoto wa wakubwa wangapi?Ulizia balozi zetu nani wamejaa huko. Nenda BOT nani wamejaa kule? Acha upuuzi
 
naunga mkono hoja...

nimetoa mikono mingi to kwa chama chetu...

kwa hili la sasa...100,000
 
nadhani hili lamchango kupitia simu lisifanywe kuwa siri.........itangazwe vizuri nina uhakika makusanyo yatakuwa ni mengi kuliko maelezo!
 
CDM kitachangiwa na wananchi wa kawaida na si mafisadi waliokubuu ndani ya CCM, swala la wewe kuwa na hasira na CDM inaonyesha CDM anakupokonya maslahi yako au ya baba yako au ya mama yako au mjomba n.k.....

Tuachie CDM yetu sisi watatzania wa kawaida tuliochoshwa na ukoloni wa CCM,

Naunga mkono hoja, Peoples power..............
Naunga mkono hoja na nimekwishachangia
 
Nimefurahi kwamba kwenye website ya chadema kuna namba 15710 unaweza kuchangia pesa moja kwa moja na unashiriki katika ukombozi. Kama ni mteja wa tigo, voda au airtel tuma neno chadema kwenda no 15710 na utakuwa umechangia sh 350. Hawajataja tigo kweye web ila ukituma inakubali.

Nawakumbusha tena chadema, tupo wengi wakereketwa wa mageuzi tumechoshwa na ccm. Anzisheni harambee maalum kwa njia ya simu ili tuweze kuchangia unzishwaji wa TV, Radio na Gazeti la chadema. Mkitangaza vizuri kwenye magazeti, mikutano ya hadhara, TV , Radio na mitandao ya kijamii kama hii mtaweza kupata bilions na tutakuwa na vyombo vyetu vya habari. Mkianzisha tu siku ya kwanza nitatoa 100,000 na wengine wengi wapo tayari. Do something before it is too late plzzzzzzzzzzzzzzz.

posho mmeongezewa juzi juzi na mka kaa kimya tu

ruzuku mnajivutia kwenu

bado michango

to hell CDM!!
 
Siungi mkono hojo.Naomba dr w.p slaa aniahidi kutopokea mshahara wa sh 7.3 m kwa mwezi na marupurupu kemkem hapo nitachangia.Hivi nyinyi mnaotaka tuchangie cdm mnakumbuka vizuri kilichompoteza Chacha Wangwe?.Pesa inaliwa makao makuu na wajanja kwa kisingizio cha harakat za ukombozi,kumbe ni harakat za tumboni.

Uropokaji ni tabia mbaya sana.Do you have evidence on what you are saying as per the bolded italics above.
 
Hili La Kuchangia Katika Simu Ni la Muhimu sana Tena Tunaomba Liwekwe Kwenye Matangazo ya Radio, TV, Kama TBC (Kodi Zetu) ITV na kwngineko!! Namaanisha Magazeti na Mikutano ya Hadhara kuwa namba ya Kuchangia Chama cha Ukombozi ni 15710. Hii Itakuwa Bora sana Mimi hapa nipo Tayari Kutuma hata msg 100!! Ila cha muhimu sisi kujua Je Hizo hela zitakifikia Chama? au TCRA Watachakachua? Ila nadhani Chama Kitatujuza Zaidi!!
 
posho mmeongezewa juzi juzi na mka kaa kimya tu

ruzuku mnajivutia kwenu

bado michango

to hell CDM!!

Mzee na thread ndefu zote unazoandika hum ndani imefika kwenye mchango umeruka!!! Waafrika tunapenda kupokea lakini ni wagumu kutoa. Hizo pesa wanazolipwa posho zinatosha kujenga chama? Mkuu we jiunge tu na CCM make wenyewe wana posho nyingi, wana pesa za kumwaga huhangaiki kuchanga. Au sio!!!!!!
 
Mimi nimesha changia Tsh 700/- kwa kutuma ujumbe mara mbili. Msisema mnaunga wazo na
viva humu jamvini wakati hamchangii. Wale mawakala wa mafisadi (read CCM) wanao beza mpango
huu wapuuzeni. Hata Obama hakuchangiwa na matajiri achilia mbali mafisadi kama CCM.

Tujitolee watanzania kwaajili ya nchi yetu, kama Nyerere alivyochangiwa kwenda UNO (zamani akiitwa hivyo)
 
imeshasemwa ni mchango wa hiyari jamani nyie wabongo wengine vipi ? mabilioni yanaliwa kila siku na wajanja serikalini mbona upigi
kelele tena zinazoliwa ni za kwa ajili ya kuwekea dawa mahospitalini na kadhalika nenda basi kamfungulie kesi chenge kwa kuiba mabilioni ya shillingi na kuyaficha nje ya nchi kama kweli una uchungu na pesa za wananchi. once again huu ni mchango wa hiyari.
Sijawahi kuona Watanzania wanafanya jambo la kimapinduzi na ambalo halitajuitiwa, tatizo hapana mahali pa reference, maana vyama karibu vyote kuna kundi la watu wachache ambao ndo wanatumia rasilimali za chama, angalia vyama vyote na uwapime viongozi wake, kuna matabaka makubwa sana, fursa zinatolewa kwa watu, either kwa kuwa karibu na mwenyekiti au viongozi wa chama hicho, kuwa vibaraka, na vyote vinavyofanana na hayo. Watanzania tuyapime sana tuyanyayo. Rasilimali zetu zinaliwa kila kona. Vijana amka
 
Uropokaji ni tabia mbaya sana.Do you have evidence on what you are saying as per the bolded italics above.
Nazani tuwe na utaratibu wa kuzifanyia kazi tuhuma, sio kutoka nazo kama zilvyo, na kuziacha zikielea bila ukweli.
 
aliyenacho anaongezewa...posho wanazopata haziwatoshi tuwaongezee na za kwetu!! Kweli tanzania ya wezi tu. Mimi siko tayari kutajirisha chama cha wachaga wa kishimundu..wizi mtupu. Ukombozi wa nchi hiii hauko mikononi mwa chadema. Tuwachangie afu waingie mitini kam babu wa loliondo.. Acheni wizi. Watanzania sio mbumbumbu..

ww umeambiwa umchangie mbunge?acha ukichwa maji unachangia chama na ili kipate mafanikio zaid tuikomboe tanzania yetu toka kwa mafisadi.
 
Naunga mkono hoja !viva Chadema viva makamanda wote!

Samahani, mimi siungi mkono si kuchangia CHADEMA bali kwa jinsi hoja imekaa kiufisadi fisadi sana. Kwani zile pesa zote zitokazo Ujerumani mmepeleka wapi. Lazima zitolewe maelezo hizo ili niweze kichanga, vinginevyo hampati hata kidogo pesa yangu.

Walaji wakubwa nyie, posho mpate na za mchango mnazitaka. Hii sio NGO ya ukoo au kabila fulani kuchuma fedha.
 
Siungi mkono hojo.Naomba dr w.p slaa aniahidi kutopokea mshahara wa sh 7.3 m kwa mwezi na marupurupu kemkem hapo nitachangia.Hivi nyinyi mnaotaka tuchangie cdm mnakumbuka vizuri kilichompoteza Chacha Wangwe?.Pesa inaliwa makao makuu na wajanja kwa kisingizio cha harakat za ukombozi,kumbe ni harakat za tumboni.

Wewe hela yako katafunie kiti moto na nyingine kanunue majini.
 
Back
Top Bottom