Changia CHADEMA Chato ili kukata rufaa ya hukumu ya mwenyekiti wake kufungwa 5 years | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changia CHADEMA Chato ili kukata rufaa ya hukumu ya mwenyekiti wake kufungwa 5 years

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Sep 20, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kama mlivyosikia kwenye vyombo vya habari kuwa

  MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela, mwenyekiti wa kijiji cha Minkoto, Alphonce Kanungu (44), na wenzake wawili baada ya kupatikana na hatia ya kuhamasisha vurugu, kuchoma nyumba na kuwakatakata ng’ombe 30 na mbuzi 20 kinyume cha sheria.


  Wengine waliohukumiwa kifungo kama hicho ni Marco Elias (36) na Cosmas Kanungu (30) wote wakazi wa kijiji cha Minkoto, kata ya Bwanga.


  Habari kutoka Chato zinaeleza kuwa mbali na kifungo hicho, washtakiwa hao wametakiwa kulipa fidia ya sh milioni 38 kwa mlalamikaji, Paul Mhunda.


  Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Khasan Koja alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Mkwasi Rashid.

  Washtakiwa hao walidai kuwa April 3, mwaka huu, majira ya saa 2 usiku waliongoza kundi la wananchi, kwenda kufanya uharibifu mkubwa wa nyumba, mifugo na mali ya Paul Mhunda na kusababisha hasara ya sh milioni 38.

  Response

  Kwa imani na ushahidi mkubwa kuwa hukumu hii imetolewa kwa kuihusanisha na siasa, wanaharakati na wapenda Chadema wa Chato wameamua kuchanga mchango wa hiari ili kuwezesha kukata rufaa. Hadi hivi sasa tayari mwanasheria amemwandikia hakimu kutoa nakala ya hukumu ndani ya siku kumi ili tuweze kusonga mbele.

  Kwa mwenye kuweza kuchangia aliyeko Chato amuone bwana Mange ambaye ni Katibu wa Chadema Chato au mchango kwa M pesa kwa

  FAUSTINE KITASANJA - 0753 277741 - Katibu wa Tawi Chato

  COSMAS MAKUNE - 0753 945 888 - Mwanaharakati

  Appreciation itatolewa kwa wote watakao husika na jumla ya kiasi kilichochangwa kitatajwa kwa wahusika wote.

  Asanteni........by Ta Muganyizi - Activist Kagera
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kutoa ni moyo. Pia wananchi na wanachama wa CDM muelewe kuwa viongozi wetu wanasaidia kutuelewesha kuwa chama ni cha wanachama na tuungane kuutetea umma. Tunapoona haki haikutendeka tuanze mara moja kudai haki kwa kufuata misingi iliyowekwa. Tukisubiri amri bila kuwa na moyo wa kusonga mbele wenyewe itatuchukua muda mrefu kulikomboa taifa hili.
   
 3. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  watu wengine kila jambo ni harakati inamana mnataka hata waharifu wasifungwe?
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Tafadhali tueleze kisa cha matukio kwa undani zaidi. Hasa kuhusuana na siasa.
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Utetezi ukoje!
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ta Muganyizi,
  Tutachangia lakini kwanza tujiridhishe kuwa hatuchangii kuendeleza uhalifu ila ni kutetea HAKI inayotaka KUPOKWA. Hebu tupatie maelezo ya kina kuwa tukio hilo lililosababisha kufungwa kwa mwenyekiti huyu.
  1. Je, ni kweli kuwa idadi ya ng'ombe na mbuzi hao waliteketezwa?
  2. Waliofungwa katika tukio hili, walihusika/hawakuhusika je katika tukio hili?
  3. Kwa nini unahisi kuwa tukio hili linahusiana na siasa ndani yake?
  4. Je, lilikuwa ni tukio la kupanga, kama ndio ni kinanani walihusika na mpango huo?

  Naomba nisaidie hayo machache kwanza.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mleta mada tukumbushe issue nzima ilivyo kuwa..kabla hatujaanza kutoa vijisenti vyetu..
   
 8. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu tunashukru binafsi ntakurushia. poleni sana wanaharakati na alaaniwe huyo hakimu gamba!
  M4C hakuna kurudi nyuma, daima kusonga mbele.
   
 9. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,634
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mzee wa baraza ningekazia na hukumu ya viboko juu yake.Kuwa Chadema sio tiketi ya kuwafanyia fujo na kudhulumu wengine.
   
 10. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,393
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Mdoa mada elezea ilikuwaje ili tujue nani kaonewa. Then tuanze kutuma michango
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Ok mtakumbuka kuwa niliwahi kuleta matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa vijiji katika maeneo mbalimbali CHATO ambapo kati ya vijiji 11 CCM iliambulia 3 na CDM ikaambulia vijiji 8. Aliyeshitaki ana rekodi ya kuvunjiwa nyumba na kuuliwa mifugo yake kwa sababu ana historia ya kuhifadhi mali za wizi. Kabla haja hamia Minkoto ambako mwnyekiti ni wa CDM alikuwa sehemu moja iitwayo Katende. Akiwa katende ng'ombe wapatao 80 waliuliwa na wananchi kwa sababu ya wizi, na kuhifadhi ng'ombe wa wizi.

  Jamaa huyo hakushitaki akakimbia na kuhamia monkoto. Wananchi wakashuhudia ng'ombe wengine wanaingia kijijini hapo kwenda kwake. Wawavamia ng'ombe hao na mbuzi. Wakimshinikiza ahame. Kwa vile kiongozi wa eneo hilo ni wa CDM ikapatikana nafasi ya kumtaight kwa kudai kuwa yeye ndo kaongoza wananchi kumshambulia mlalamikaji. Mashahidi wakuu ni pamoja na wake wa mlalamikaji kuwa walisikia sauti.

  Pili mwenyekiti huyo alishinda uchaguzi mwaka 2009 lakini akatangazwa wa ccm ikawa mpaka kesi ikaenda mahakamani na baadae uchaguzi kurudiwa mwaka huu akashinda huyuhuyu wa CHADEMA na hiyo kuwaudhi wana CCM....kwa hiyo kilichofanyika ni kutafuta njia ya kumpoteza.
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hapa ndo ubaguzi unaonekana ndani ya CDM kwani kwenye rufani ya LEMA mliwanyang'anya wananchi kidogo walicho nacho?
   
 13. t

  thatha JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kuchanga kunaanzia hapo kwa nini? mbona kwa LEMA kulikuwa hakuna kuchangishana? ukabilization siyo?
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Tukizoea kuchangia fedha za rufaa, watazoea na kuubadilisha kuwa mradi tena kama walivyobadili M4C kuwa mradi wa MBOWE, SLAA na HECHE.
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hivi unategemea mtu anayefikiria kuchangisha pesa kwa ajili ya matumbo ya akina MBOWE, SLAA na HECHE akupe majibu ya maswali magumu kama hayo?
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh, kumbe ninyi hamjawagundua CDM hizo fedha zitakazo patikana hapo, siyo kwamba zitakata rufaa ,bali ni mwendelezo wa kusafisha fedha zao chafu, wana mbinu hawa jamaa we acha 2. wakigundulika huku wanaibukia kule, kama kinyonga vile. NAPE wamulike na huko.
   
 17. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,531
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kuna mambo mengine viongozi wanatakiwa kuwa makini sana,wananchi wameshakata tamaa vijijini hivyo kiongozi lazima atumie busara zaidi na asiwe na kauli za kuchochea.

  Kuna kipindi nilisafiri hadi Bariadi nilikuta kitu kama hiki kimetokea kwa mganga wa kienyeji kuvamiwa usiku na kijiji,ng'ombe 40,magunia ya mahidi 30,20 mpuga pamoja na nyumba kadha wa kadha kuteketezwa japo familia ilinusurika kwa kutoroka kabla ya tukio.

  Kisa mganga anazuia mvua kunyesha kijijini,je,hii ndo ilikua adhabu stahili? Katika masuala ambayo katiba haiyatambui ni hili la uchawi/ushirikina na kama unaamini katika ushirikina nawe ni vizuri kumalizana na mbaya wako kwa kishirikina.

  Pia la sivyo katiba haitokuacha ukitamba mtaani,suala la chato sijajua chanzo chake lakini kama lilifanyika katika mazingira kama la bariadi tuache jamani sheria ifanye kazi na tusiwe wepesi wa kusema eti hukumu ziko kisiasa,kama chama.

  Chadema wahatakiwi kulea mtu wanayeona anavunja sheria na haki za binadamu lakini kama watakumbatia kila mmoja kwa kuitana makamanda ata wakati mnavunja sheria tutakuwa tunakosea sana tunakiua chama chetu ambacho ndo tunaona taa ya kijani imeweka wakati vingine vyote akiwemo Mabwepande wametuwashia taa nyekundu kabisa.
   
 18. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  Kuna hakika kuwa wameonewa?
  Maana huko vijijini wenyeviti huwa wanajifanya miungu watu.
   
 19. TEMPOLALE

  TEMPOLALE JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina pesa sana lakini siwezi kukosa hata ki-elf10.
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Anachofikiria huyo ni mlungula wa walala hoi, inaonekana naye ana kamgao nini?
   
Loading...