Changia CCM

Kabengwe

JF-Expert Member
Oct 20, 2009
240
47
Hili zoezi la kuichangia CCM bado halijaniingia akilini vizuri.

Hawa jamaa ndo wamekuwepo madarakani tangia tunapata uhuru. Wametuibia kwa dizaini zote yaani hata makovu ya Richmond, mikataaba mibovu ya madini na EPA hayajaisha, wanakuja kutuomba tuwachangie warudi kutuibia tena. Hivi sisi watanzania ni nani ameturoga?!

Kuna kipya kweli cha kutarajia kutoka kwao baada ya kuwachangia!?
 
Wajanja tumeishutukia hatuwezi kuchanga, hii ni strategy ya chama hili wakiiba huku na huku waseme mlituchangia
HILA NAOMBA UBADILISHE HEADING YAKO MANA WANAJF WAKIONA "changia JF" wanaipotezea
 
Mnakumbuka mwaka 2005 walianzisha hii strategy na wafanyabiashara wakachangia kwelikweli na matokeo yake aliposhinda akawapa vyeo ili wapate kurudisha pesa zao. Matunda yake ndo huu ufisadi tulonao. Waacheni wachangishe tu but WaTZ wengi wameanza kuelewa. Tukutane oktoba!
 
Shame on them. Si wayauze yale magari waliyoyaingiza bila kulipia ushuru wapate hela za kukampaini? Kodi na ushuru ninaolipa kila mwezi hauwatoshi? CCM usinitibue kabisaaaaaaaa
 
hawa jamaaa wezi sana si wameiba bill 300 hazijatosha tu.jk nae kasafiri du sindbad huyu hachoki tu
 
Wataalam kama kuna jinsi ya kuzuia hizo sms zao zisiingie kwenye cm yangu, msaada tafadhali
 
Tuchangieni tu hakuna neno mabadilko yatakuja automatically wala msijali safari hii tutafanya changes za nguvu wananchi wangu.!!!
 
Wataalam kama kuna jinsi ya kuzuia hizo sms zao zisiingie kwenye cm yangu, msaada tafadhali

Jana cku yote wameniharibia mood kwa meseji yao ya kuomba mchango, hivi kwanini wasiwatumie wanachama wao tu?:hug:
 
CCM wanafanya danganya toto tu, asilimia 50 ya stimulus package wameshatia mfukoni kupitia ufisadi wa Makampuni EPA ya Makada wao sasa hiyo changia nyingione ni magirini tu
 
Ni kweli kabisa - kuchangia jamaa hawa unatakiwa uwe na moyo mgumu sana - pesa zote hizo walizonazo haziwatoshi hadi wanatuomba na hivi vi thumni tulivyonanvyo?

Good option to them is, just 3 mafisadis watoe mihela wazigawe kwa watu wajifanye wamechangia ili majina yaandikwe simple as that. Bongo hii kuna kitu kinashindikana? Imagine kama Rais anapigwa kanyaboya kusaini kitu kime editiwa itakuwa hili la uchangiaji?

Bongo tambaraaree - as people used to say. I support you 1stLandy asilimia mia kwamba hakuna kutoa hata ndururu!!
 
Mkuu hiyo ni zuga tu maji yakiwafika shingoni waseme wananchi walituchangia hamna lolote ukiona ivyo kuna sehemu wanataka kuchota ila walivyo na mahesabu ya mbali wanajua hali inaweza kuwa kama ya epa.
Hili zoezi la kuichangia CCM bado halijaniingia akilini vizuri.

Hawa jamaa ndo wamekuwepo madarakani tangia tunapata uhuru. Wametuibia kwa dizaini zote yaani hata makovu ya Richmond, mikataaba mibovu ya madini na EPA hayajaisha, wanakuja kutuomba tuwachangie warudi kutuibia tena. Hivi sisi watanzania ni nani ameturoga?!

Kuna kipya kweli cha kutarajia kutoka kwao baada ya kuwachangia!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom