Change We need, No matter what Lowasa is, CCM should Note that

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,194
5,598
CCM na wafuasi wake hapa JF juhudi zao kubwa ni propaganda ya Lowasa ni Mgonjwa, awezi ongoza nchi

Kwanza niwakumbushe kikwete pia ni Mgonjwa na aliongoza nchi, alianguka Jukwaani mara mbili, pale Jangwani wakati wa kampeni wote mnajua/tunajua, na kule Mwanza. (ushahidi upo mpk leo. Mitandaoni)

Kikwete ni anaumwa Tezi Dume (prostate Gland) bado anaongoza nchi na pamoja na magonjwa hayo tunayoyafahamu na imani kama binadamu anayo mengi tusiyoyajua lakn ameongoza nchi japo kwa udhaifu mkubwa (kiutendaji) .

Pamoja na Magonjwa hayo bado alimudu kusafiri kila siku nje ya Nchi. Na watafiti wa mambo wanasema walau katika miaka kumi ya uongozi basi miaka minne alikuwa nje ya nchi.

Rai yangu kwa wana UKAWA tujue kushugulika na propoganda za CCM, mtu akija na mada za ugonjwa hapa tutaijaza thread yake kwa kumjibu neno moja tu. Tunataka Mabadiliko Hata kama UKAWA watasimamisha Jiwe

Binafsi, nna Imani na Lowasa kuwa atakuwa Rais Bora kwa miaka ya Karibuni Tanzania (ukimuondoa Nyerere) maana Nyerere ana legacy zake.

CCM must Go no matter what hata kama UKAWA wangeweka jiwe. Tumechoka, adhabu kubwa kwa ccm nikuwapumzisha wajue nchi hii ni ya kwetu na vizazi vyetu vijavyo, tunataka chama kijue hakitatawala milele, Chama kijue kila kikishika Dola kinapaswa kufanya nn kwa wenye nchi.

Tunataka vyama viwe vinabadilishana madaraka ili kuchochea Maendeleo chanya, na ubunifu katika kutatua matatizo ya Nchi hii

Mabadiliko ni sasa, usikate tamaa mabadiliko ni mimi na wewe, Kura yako ya Ndiyo kwa Lowasa, itaibadili nchi Yetu, itatujengea Tanzania boranya kesho
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom