Changamoto zipi utakutana nazo ukivaa fulana au Kapelo ya CCM?

Mzee wa kurekebisha

Senior Member
Sep 29, 2012
178
169
Siku nilifanya kama mzaha tu, nilivaa Kapelo(kofia) ya CCM, kipindi hicho uchaguzi mkuu (2010) ulikuwa unakaribia
Kona kadhaa nilizopita nilikutana na mambo yafuatayo.

1. Matusi ya chinichini huku watu wakitoa shutuma
kuwa kijana Mzima anaikumbatia CCM!

2.Sura zilizokuwa zinaniangalia kwa ghadhabu, dharau na hasira.

3.Wengine walinisonya.
NB. Hakuna aliyenipiga.

Tafadhali naomba utueleze huko uliko ni changamoto zipi unaweza kukutana nazo kwa kuvaa nguo za CCM.
 
Kwa Moshi unaonekana kama Mwendawazimu, utaangaliwa vibaya, na ole wako ujaribu kuongea maneno ya kusifu ccm, utashambuliwa kwa maneno mpaka ukome, inafika mahali watu wanatamani wakutie makofi kwa hasira.
Kwenye daladala ndo usisubutu maana hata hujaongea na mtu wanaanza kukuzomea.
Hivyo Moshi hata wale wanachama wa ccm huwa wanapokuwa na vikao vyao huwa mtu anavaa nguo ya kawaida kusudi aweze kupita kwa amani barabarani na ile zare anaweka kwenye mfuko akifika eneo lake la tukio ndo anazifaa.
 
ngoja nifikirie kwanza, nitamfanyaje kijana huyo maana daah!!!!!!!!!!!!
 
mie siku 1 nilipiga top yangu ya ukweli ina rangi ya kijani na weupe pembeni, then nikawa na trip nje ya jiji la arusha so nikaenda stendi, duu wacha vijana waanze kunitupia maneno, but mie nikawatuliza munkari kwa kuonyesha ishara ye2 ya vema, wakanambia aina noma sista!! umesomeka
 
Back
Top Bottom