Changamoto zinazo walazimisha watoto kuacha masomo Sudan

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
1579516460651.png


Utafiti uliofanywa na wizara na Unicef

Utafiti uliofanywa na Wizara ya Elimu kwa ushirikiano na UNICEF umebaini kuwa zaidi ya watoto milioni 3 hawahudhurii masomo nchini Sudan

Watoto wa Sudan huondoka nyumbani kutafuta ajira kila siku badala ya kuhudhuria masomo, kutokana na umasikini uliokithiri na pili mfumo wa elimu usiyo na rasilmali za kutosha kuweza kuwahudumia

Sudan imeorodheshwa kama mojawapo ya mataifa masikini zaidi duniani.

Licha ya hali ya kisiasa kutulia, uchumi ungali unasusua. Mjini Khartoum, ni kawaida kuona watoto wadogo wakifanya kazi za useremala, ufuaji chuma pamoja na biashara

Watoto hawawezi kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu ya maisha. Baba zao huwapeleka sehemu tofuti tofauti ili wapate cha kuwaingizia ujira kutokana na ugumu wa maisha. Hata hivyo siyo wengi ambao huvumilia hali hii.

Maafisa wa serikali ya Sudan wametia saini mikataba ya kimataifa ya kutoa elimu ya bure kwa watoto pamoja na kusitisha ajira za watoto, lakini sheria hizo hazijatiliwa mkazo anasema Siddiga Kibeida mfuatiliaji haki za watoto.

Kibeida : "Umasikini ulioko Sudan unaathari kubwa kiasi cha kutoweza kuzuia ajira za watoto ingawa kuna sheria inayowazuia kufanya kazi kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Kudhibiti Umasikini ni suala muhimu kabisa."

Waziri wa Elimu anaeleza : "Nchi hii haiwezi kutekeleza haki za watoto. Ilichofanya ni kuweka mfumo wenye uwezo wa kusaidia asilimia 60 ya watoto pekee huku asilimia 40 wakibaki bila nafasi ya kupata masomo na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kuwa na watoto milioni 3 ambao hawahudhurii masosmo kulingana na ripoti ya UNICEF
 
Back
Top Bottom