Changamoto zilizotatuliwa ili kukuza biashara kwa vijana

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Idadi kubwa ya Watanzania ni vijana, nao ndio wanakabiliwa zaidi na tatizo la ajira, vijana wa kike wakiathirika zaidi.

Kukabiliana na changamoto hiyo, hatua hizi zimechukuliwa zikionesha kuwa Rais Samia Suluhu anahakikisa anawakwamua vijana na wanawake kiuchumi.

1. Mikopo/mitaji ya biashara; Benki zimeanzisha madirisha yanayotoa mikopo kwa riba nafuu. Taasisi za kimataifa za kifedha zinatoa fedha za ukuaji sekta binafsi

2. Kurekebisha mifumo ya kodi na tozo; Serikali ya Rais Samia Suluhu imerekebisha mifumo hiyo ili kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara wadogo

3. Kutoa vyeti vya ubora; Lengo la kutoa vyeti hivi vya TBS ni kuwawezesha wafanyabiashara kuyafikia masoko ya kimataifa maana Rais Samia Suluhu amefanikiwa kuimarisha diplomasia ya uchumi iliyofungua milango ya biashara kimataifa kwa watanzania

4. Kuboresha mifumo ya usimamizi; Serikali imefanikiwa kuondoa tatizo la taasisi nyingi kumsimamia mfanyabiashara mmoja

5. Masoko; Serikali inafungua masoko ya ndani na nje ili wafanyabiashara wawezee kuuza bidhaa na huduma zao kimataifa.

Hii ni baadhi ya mikakati iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu lengo ni kuhakikisha mazingira ya kujiajiri yanaboreshwa na vijana wengi kufanya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.
 
Changamoto bado ni nyingi sana kuhusu kuweza kukwamua vijana wengi. Bado wanakabiliwa na tatizo la kukosa dhamana za maana ili kuweza kupata mitaji mikubwa kutoka katika taasisi za fedha ili kuweza kuendesha biashara za ndoto zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mikopo ambayo inatolewa na halmashauri inawalenga wanaweka, vijana na watu wenye ulemavu hii mikopo ina masharti nafuu kijana yeyote mwenye ndoto ya kufanya biashara anaweza kukopo
 
Idadi kubwa ya Watanzania ni vijana, nao ndio wanakabiliwa zaidi na tatizo la ajira, vijana wa kike wakiathirika zaidi.

Kukabiliana na changamoto hiyo, hatua hizi zimechukuliwa zikionesha kuwa Rais Samia Suluhu anahakikisa anawakwamua vijana na wanawake kiuchumi.

1. Mikopo/mitaji ya biashara; Benki zimeanzisha madirisha yanayotoa mikopo kwa riba nafuu. Taasisi za kimataifa za kifedha zinatoa fedha za ukuaji sekta binafsi

2. Kurekebisha mifumo ya kodi na tozo; Serikali ya Rais Samia Suluhu imerekebisha mifumo hiyo ili kupunguza mzigo kwa wafanyabiashara wadogo

3. Kutoa vyeti vya ubora; Lengo la kutoa vyeti hivi vya TBS ni kuwawezesha wafanyabiashara kuyafikia masoko ya kimataifa maana Rais Samia Suluhu amefanikiwa kuimarisha diplomasia ya uchumi iliyofungua milango ya biashara kimataifa kwa watanzania

4. Kuboresha mifumo ya usimamizi; Serikali imefanikiwa kuondoa tatizo la taasisi nyingi kumsimamia mfanyabiashara mmoja

5. Masoko; Serikali inafungua masoko ya ndani na nje ili wafanyabiashara wawezee kuuza bidhaa na huduma zao kimataifa.

Hii ni baadhi ya mikakati iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu lengo ni kuhakikisha mazingira ya kujiajiri yanaboreshwa na vijana wengi kufanya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Awamu ya sita kazini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom