CHANGAMOTO ZA USTAWISHAJI WA MAKAO MAKUU DODOMA: Ujenzi holela washamiri Makulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHANGAMOTO ZA USTAWISHAJI WA MAKAO MAKUU DODOMA: Ujenzi holela washamiri Makulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Niambieni, Oct 3, 2012.

 1. Niambieni

  Niambieni JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 599
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Kwanza napenda kutoa shukrani nyingi kwa Serikali yetu kwa kufanya jitihada kubwa ya kuujenga Mji Mkuu wetu wa Dodoma. kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ofisi za Benk Kuu, Hazina, Nyaraka na nyinginezo nyingi zinazoendelea, zinaifanya mji wa Dodoma kujipanua yenyewe.

  Hata hivyo mbali na jitihada za Serikali, kuna changamoto zinazoletwa na wananchi wenyewe ambazo zinaonekana kushamiri kwa kasi kubwa sana. Mfano; Vitongoji cha Makulu, kuelekea UDOM na Ng'ong'ona nyumba zinajengwa bila kufuata mpangilio na ni za muda na zingine za kudumu.

  Upande wa Makuku, Kuna sehemu iliyopimwa lakini wananchi wanajenga hata kwenye sehemu za barabara, na zinasongamana. Hii inaonyesha kuwa baada ya muda miezi michache ijayo hakutakuwa na barabara bali ni vinjia tu, na maji taka kuzagaa. Sehemu hii haina tofauti na uwanja wa fisi wa Manzese.

  Capital Development Authority (CDA) haifuatilii, inaonekana kuwa hapa Dodoma hakuna Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu, bali kuna ofisi isiyofanya kazi. CDA haina mamlaka sehemu hizi. Dodoma ipanua na kuanzisha barabara hata za lami maporini ambako hakuna watu kama Itega, Ilazo na kwengineko pembezoni mwa mji au ambako hakuna watu. bali walipo watu kama Makulu na Ngong'ona hakuna hata dalili ya kuonyesha kuwa wataonyesha barabara au ujenzi wa mpangilio mzuri kama alivyo agiza Mh. Rais Dr. J. M. Kikwete.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na viongozi wengine wenye dhamana tunawaomba msaada wenu. Tumejaribu kumshirikisha Diwani na Viongozi wengine wa vitongoji bila mafanikio, Diwani naye ameonekana kujenga sehemu iliyopimwa barabara, na aamini CDA. Hii ni pamoja na maeneo mengine yanayozunguka UDOM kama Ng'ong'ona. CDA kama ingekuwa makini wakati wanawahamisha wananchi toka eneo la UDOM wangeli wapimia sehemu hizo wananchi na wafanyakazi wangelijenga kwa kufuata mpangilio mzuri. Wananchi wa Dodoma tumekata tamaa kabisa na CDA. Inawaachia wananchi wajenge holela.
   
Loading...