Changamoto za Sajuki,kujitambua kwetu na uhusiano wa kinafki

Mwambieni mkulu ile 10m ambayo angeitoa ya ubani aitoe sasa hivi ili kuokoa life ya huyo msanii
 
Uliyo yasema mkuu Fidel80 ni kweli akifa utaona watu wanavyo shona sare na miwani ya jua kudadadeki na wengine chekiza mil 10....

Unajua Crashwize tatizo lipo wapi?
Ni kwamba mtu akitoa mchango wa kuumwa hapewi promo kama akitoa rambi rambi mtu kafa.
Umeona promo anayo pewa JK mpaka leo zile 10m kwenye msiba wa Kanumba
 
Kama sijaelewa na sikuelewa, una uhakika gani kuwa ukiendelea kunijibu nitaelewa? FYI, mtu ambaye haelewi hapa ni wewe, unapofungua uzi kuwa tayari kwa mada yako kunyambuka, usitake watu waseme unachotaka wewe kusikia ili kujustify conclusion yako..acha kuwa one-sided and myopic, funguka na kuwa mpana, i mean kimawazo.

Kwa kweli hata mimi mpaka najiona siko Tanzania, who is Sajuki? Ningependa nami nimjue...au labda ni google?
 
Kwa kweli hata mimi mpaka najiona siko Tanzania, who is Sajuki? Ningependa nami nimjue...au labda ni google?
Wewe kama mie, ukiwa sio mpenzi wa the so-called bongo muvi, magazeti ya udaku na bongo fleva, utajihisi mkiwa na mgeni sana . Mie hadi leo sjui 'hakunaga' kaimba nani :tongue:
 
Kwa kweli hata mimi mpaka najiona siko Tanzania, who is Sajuki? Ningependa nami nimjue...au labda ni google?

Huu ni unafiki mwingine!Si ungegoogle sio mpaka uje useme hapa!
 
Jana mchana walionyesha live clouds tv watu wakimchangia...
Honestly kuna watu wameguswa labda kwa sasa hiyo fedha itakua imepatikana..
 
hem tuwekee picha ya huyo jamaa alivyo kwasas labda tukaguswa kuchanga.

Si muweke ata picha wengine hatumjui jamani

Sajuki mgonjwa.jpg

Picha ya kulia Sajuki alivyokuwa kabla ya kuugua.
Picha ya kushoto alivyo kwa sasa.
 
lkweli anaumwa jamni,watanzania wenye moyo 2jitolee chochote na kumuomba mungu ayaokoe maisha yake.nimesoma kwenye gazeti la mwananchi eti wasanii wa bongo movie aliyetoa hela ni wema sepetu pekee.jamni kinachoniuma ni kuona serikali inavyounyuti,ajira hakuna,wa2 wanajiajiri bt wanapata pesa ya kula2,hivi kweli kikwete na serikali yake wanashindwa kutoa hata 5mil?sajuki ni moja kati ya watanzania wengi wanaoteseka bt bila msaada na wanapoteza ma2maini ya kuishi.watanzani wengi 2naguswa bt on de other hand ugumu wa maisha unamfanya m2 afikiri mara 2
2.2cio na cha kutoa nadhani dua na maombi ye2 ni mchango pekee na nina amini Mungu yupo na atajibu
 
Pole nyingi kwa mgonjwa....Jamani jamani mbona inakuwa hivi???? Sajuki vile ni msanii ana bahati hata watu wakajitokeza na kuomba michango kwa ajili yake hususan wasanii wenzake na watu wengine wa kawaida walioguswa na hili. Tatizo hapa si Wizara ya Utamaduni kumpa msaada kijana huyu ni wangapi watahitaji msaada wa aina hii kutoka wizara husika....Mdudu hapa ni SERIKALI YETU NA WIZARA YA AFYA PERIOD...Kwa nini tukatibiwa India? Vipi kwa wale ambao si wasanii nani atawachangia endapo watahitaji msaada kama huu? Ina maana kila mtu akimbilie wizara husika akifikwa na janga kama hili! Serikali badala ya kufuja pesa za walipa kodi izingatie kuboresha hospitali zetu kwani mabingwa tunao. Kuliko hiyo pesa kuipeleka India ni bora ingebaki nchini. Nimeona baadhi ya wabunge walioguswa na hili lakini nadhani ni wajibu wao kuiambia serikali hii si haki kwa Mtanzania kwa nini tulie, kwa nini tuwe ombaomba kwa ajili ya afya zetu????
 
yaan mpaka machoz yananitoka sajuki huhuyu ndo wa kuwa vile kama kibabu, bongo movie mpo wapi? Sioni sababu ya kuendelea kuigiza maana kazi yao kuelimisha jamii na kuburudisha lakin wanafaidika na nin?
 
Huu ni unafiki mwingine!Si ungegoogle sio mpaka uje useme hapa!
ingekuwa malumbano ya hoja live nahisi watu mngepigana hapa...duu.Eiyer chukulia mtu alivyo laa sivyo utakasirika bure na mtu hamjuani mmekutana humuhumu tu.Take it easy:rant:
 
Duh! Kwelu hujafa hujaumbika, kweli Sanjuki anaumwa, Mungu atamponya

Jana nimesikia tena wajanja weshadivert namba ya mkewe ya Mpesa, hela haziingi tena kwenye account yake, sasa tunaogopa hata kutuma michango yetu
 
Naskia huruma na uchungu kwa hali alofikia,namuombea kwa mungu atie nguvu na kurejea katika hali yake ya mwanzoni,ndugu zangu tujijengee tabia ya kwenda kucheki Afya zetu japo mara moja kwa mwezi,hii itaturahisishia kuepukana na sapriz za magonja yanayokuja tutishia baadae yanapoamua kujitokeza. Itatusaidia sana kuwa wenye Afya njema daima.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom