Changamoto za Sajuki,kujitambua kwetu na uhusiano wa kinafki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto za Sajuki,kujitambua kwetu na uhusiano wa kinafki

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, May 5, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Kwanza nampa pole kijana Sajuki pamoja na familia yake kwa ugonjwa unaomsumbu.Nilisikia uchungu sana jana nilipomsikia mke wa Sajuki,Wastara akiomba msaada redioni ili mumewe akatibiwe India,kilichonifanya nipate uchungu ni kiasi cha fedha alichokua anahitaji,milioni 25!Hivi ni kweli kwa kiwango alichofikia Sajuki katika bongo muvi anakosa fedha hizi?Kama kweli hana namshauri akipona atafute shughuli nyingine ya kufanya.Ni jambo la ajabu sana kwa alipofikia Sajuki halafu akose kiasi hicho cha fedha.Halafu wasanii wenzie wako wapí?Hivi kweli wameshindwa kuchana kiasi hicho cha fedha?Msiniambie hawana fedha wasanii wote hao,hii mikogo yao tunayoiona ya kujibandua ngozi,kuendesha magari,ulevi n.k wanatoa wapi hela?Plz msiniambie wanaazima,bongo muvi itakua haina maana kabisa na bora isiwepo.Kama mnashindwa kumsaidia mwenzeu muda huu mnataka afe ili mje na mikogo yenu ya kijinga msibani?Jamani hata wasanii wenzie wa bongo fleva?Jamani mpaka mkewe huyu kijana aende redioni?I don't believe this,it's a shame!Wizara ya utamaduni na michezo,wabunge mko wapi?Au mnataka msimame bungeni au muende msibani na msururu wenu wa magari kwenda kusaini kitabu cha maombolezo kwa mikogo huku mkisema "kijana alikua anajituma,mchango wake tunautambua" huku sauti yake ikiwa ringtone ya simu zenu,eti mnamuenzi!!Shame in both of you!Siamini kama hatujitambui kiasi hiki,uko wapi utu wetu?
   
 2. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  kama sijakosea nilimsikia mkewe akiongea na Dina siku moja akasema kwa sasa alishaenda India na kurudi na yupo katika kutumia dawa ya mara moja kwa wiki iliyomgharimu karibu dola elfu moja kwa wiki, na anatumia kwa wiki 8 au 10 na najua kwa sasa bado anatumia as wiki hazijaisha tangu atoke india na alivyoanza dozi.

  Kwa hiyo ameshatumia pesa kama alikuwa nazo au la za kuazima mie nashangaa.

  Ungeshangaa kwa nini ameshindwa kupata msaada wa serikali unaopeleka watu bure India kutibiwa as kama wamefanya au wangefanya application basi wangeshapata a go ahead as ingewapunguzia costs i guess.

  Ila ndio maisha hayo, kwani unajua wasaniii wanapata shilingi ngapi waki act movie? embu nambie.

  Kumbuka sio wajibu wa wasanii wengine kusaidia wenzao. as haya ndio maisha. hata nadhani unajua hii ipo kila kona ndio maana ukienda makanisani unakuta matajiri na masikini na hakuna eti weye tajiri saidia maskini wote wa hapa kanisani. Kila mtu na maisha yake.

  HATA NDUGU WENGINE TABU KUSAIDIANA ITAKUWA WATU WANAOFANYA KAZI PAMOJA?

  KUTOA NI MOYO.
   
 3. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,837
  Trophy Points: 280
  binafsi ninachokiona hapa siyo swala la kuwa msanii au nini hapa inatakiwa sisi kama watanzania basi tusaidiane mwenzetu atibiwe, na siyo lazima kwa kutoa hela bali yupo mwingine anaweza kuwa na mbinu mbadala like anaweza kumsaidia kupata msaada kwa yale mashirika yanayopelekaga watu huko india kutibiwa, kama ambavyo huwa tunafanya kwa wengine wanao ugua na kuomba misaada kwenye tv na redio. mwenye nacho jamani ajitolee. waache hao wanaopenda kuhudhuria misiba waanze kuandaa mavazi mazuri ya kuja kuzikia.
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mungu ampe nafuu ....and the rest I reserve my comment
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  mzurimie what i was wondering ni jambo lilivyo.Hivi nini maana ya kutambulika na kuitwa kioo cha jamii?Angefanya jambo la kijinga angelaumiwa anapotosha jamii,ila sasa wanamuangalia tu.Acha mambo ya kufikiri kuhusu wanaopelewa kutibiwa bure,Sajuki ni zaidi ya hilo.Kwanza kupelekwa kutibiwa bure ni dili!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana tena sana.
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mungu amsaidie apate uponyaji na michango yetu inahitajika kuna namba za simu pia tunaweza kuchangia any amount ili kijana apate msaada
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Who is Sajuki? what is so special na kuumwa kwake?
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Ni binadamu ndo maana kuumwa kwake ni spesho.

   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  kuna binadamu zaidi ya bilioni moja na wapo wengi wanaoumwa na kuhitaji immediate treatment ili wasiage dunia. yeye ni tone tu ktk bahari. hana uspesho wowote.
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Kijana,sijazungumia unayosema wewe,Sajuki ni mtu kama watu wengine na ana thamani kama wengine.Ninachosema ni wewe mimi na wengine kujipima kama tuna utayari wa kusaidiana kwenye changamoto tunazozipata katika maisha yetu bila unafki!
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Huu u-spesho unaousema nani ameusema kama sio wewe?Soma thread uelewe!
   
 13. ChaterMaster

  ChaterMaster JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  hem tuwekee picha ya huyo jamaa alivyo kwasas labda tukaguswa kuchanga.
   
 14. vanilla

  vanilla JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  o wengi tu wanaohitaji msaada lakini hamna anayejali.sajuki angekuwa sio msanii leo hii nani angemtambua na kumuombea misaada? mbona wanajitokeza wengi tu kwenye TV kuomba msaada wa angalau laki nne lakini hamna anayeona kwamba wana uzito wa kusaidiwa? huu ni utabaka tunaojijengea wenyewe. kisa mtu anajulikana ndio kila mtu anapiga kelele asaidiwe. binadamu wote ni sawa na pia kutoa ni moyo so kama mkewe ameomba msaada redioni then asubiri wenye mioyo ya kutoa watoe ustaa aweke pembeni.otherwise she will expect a lot kwasababu ya status zao kwenye jamii halafu akawa dissapointed. nasi twaendelea kumuombea Mungu ampe afya njema soon!
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wabongo kama kawaida yetu tunasubiri afe kisha twende kushindana kutoa rambi rambi
  Anahitaji pesa za matibabu wabongo wote wameuchuna akifa utasikia watu wanavyo ibuka nimeguswa sana na msiba huu natoa milioni mbili kipindi hiki wamebana masaburi yao.
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Naam mzee,
  Hakika, na sijasema vinginevyo.
  Taib, tupo pamoja.
  Wengi wetu tunakabiliwa na changamoto ya kukosa cha kusaidia, hivo huu uzi ni mzuri kifikra lakini kipraktiko hauna mashiko.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kama sijaelewa na sikuelewa, una uhakika gani kuwa ukiendelea kunijibu nitaelewa? FYI, mtu ambaye haelewi hapa ni wewe, unapofungua uzi kuwa tayari kwa mada yako kunyambuka, usitake watu waseme unachotaka wewe kusikia ili kujustify conclusion yako..acha kuwa one-sided and myopic, funguka na kuwa mpana, i mean kimawazo.
   
 18. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  naibu waziri mpya wa vijana utamaduni na michezo -amos makala ni mdau mkubwa wa filamu na ni mtu aliye na ukaribu na wasanii wa filamu naomba ukishaingia ofisini fnaya kweli basi sajuki akatibiwe-kama vipi piga donee wewe na wenzako fasta mgonjwa akatibiwe,UNAWEZA KAKA!
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama mnamchango mchangieni acheni Longolongo kama Kikwete anae subiri afe akatoe rambi rambi mil 10.....

  Namba ya M-Pesa ya Mke wake Wastara Juma ni 0762189592
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Uliyo yasema mkuu Fidel80 ni kweli akifa utaona watu wanavyo shona sare na miwani ya jua kudadadeki na wengine chekiza mil 10....
   
Loading...