Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,968
"Ndugu mteja, kuanzia trh 02/04/2018 faida kwa mauzo ya LUKU itapungua kutoka 2.5% hadi 0.5% kutokana na punguzo la kamisheni na TANESCO. Asanteni" Ujumbe kutoka SELCOM
======
Naona dalili za kuyumba kwa biashara za uwakala wa kufanya mimala ya LUKU kupitia Selcom na Maxmalipo hasa kutokana na Tanesco kupunguza kamisheni katika miamala ya kuuza LUKU kutoka asilimia 2.5 hadi 0.5 kuanzia April 2, 2018 Hii maana yake ni kuwa wakati zamani ukiuza umeme wa Sh laki moja ulikuwa unapata kamisheni ya 2,500/= kwa mabadiliko haya sasa ukiuza umeme wa kiasi hicho hicho kwa miamala tofauti au kwa pamoja utapata Sh. 500/= ambapo ukiweka float kwa njia ya simu unakatwa 1500 kwa laki 1.
Pamoja na faida hiyo ndogo bado wakala utakatwa Connectivity ya 2,500/= kwa mwezi pamoja na kodi. Sasa kwa kamisheni ya asilimia 0.5 ni kuwa ukifanya biashara ya Sh milioni 1 utapata kamsheni ya sh 5,000/= kisha hapo ukatwe connectivity, na kodi hapo bado hujaondoa gharama ya rola ambayo ni kati 2,000 hadi 3,000/ bado hapo hujakatwa unapoweka float. Hivyo ukijumlisha makato yote unaweza kukuta kamisheni yote inakatwa na unadaiwa ambapo watakata kwenye float au mtaji wako. Kwa namna hii wengi wataziground hizi mashine kwakuwa mitaani biashara kubwa ya mashine hizi ni kuuza umeme na kidogo kulipia maji na vocha rusha ambazo sio kubwa kivile. Maxmalipo mwanzoni ilikuwa inatumika hata kulipia faini za trafiki lakini waliondoa hiduma hiyo.
Makampuni haya yaangalie namna ya kusurvive na kuwafanya mawakala wabaki katika biashara vinginevyo wengi watashindwa na kuzifungia mashine kwenye makabati hasa ukizingatia kuwa huduma hizo zinafanywa pia kupitia mitandao ya simu hivyo siyo lazima mteja aende kwa wakala wa Maxmalipo au Selcom.
Ndugu mteja, Mauzo ya LUKU sasa yanafanyika moja kwa moja kwenye mfumo wa malipo wa serikali GEPG. Ada ya 1.1% itatozwa. Mf: Kwa LUKU ya Tsh 1000, Ada ni Sh 11
Cost TZS 4,098.37
VAT 18% TZS 737.70
EWURA 1% TZS 40.98
REA 3% TZS 122.95
TOTAL TZS 5,000.00