SoC01 Changamoto za Malezi ya Watoto na sababu za wababa kufa mapema. Je, wamama wanahusika?

Stories of Change - 2021 Competition

emmapetertz

Member
Jul 15, 2021
12
28
WABABA: CHANGAMOTO ZA MALEZI YA WATOTO & SABABU ZA KUFA MAPEMA. JE, WAMAMA WANAHUSIKA?!!
Screenshot_20210716-142906.png

Wanaume ee,

Mnajionaje na hali wapambanaji wenzangu?!! Poleni na hongereni kwa siku nyingine tena. Ni matumaini yangu mko poa sana, mkiendelea na majukumu ya kila siku ya hapa na pale katika kuhakikisha heshima zenu kama waume na baba majumbani kwenu zinaendelea kujengeka vizuri. Iko uchi (wazi) kuwa, ni wajibu wa baba kuhakikisha familia inapata mahitaji yote muhimu ya kimaisha hususani malazi, mavazi na chakula ili watoto waendelee kupishana pishana kila mara kuingia na kutoka mlango wa chooni. Furaha ya mwanaume yeyote rijali ni kuona familia yake inasonga mbele, sawia?

Nazijua nukuu nyingi tu zitutiazo nguvu za kupambana na kutufanya tuwe na mioyo yabisi (migumu) katika kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha bila kuchoka. “Mwanaume hajaumbwa kushindwa, anaweza kuharibiwa mipango yake lakini kamwe hashindwi” – Ernest Hemingway. ‘Kuwa mwanaume ni juu ya kuchukua jukumu na kutumia nguvu yako kuwatumikia wengine katika kuunda na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii/familia yako’ – Francis Bacon. Kinachotufanya tuteseke sana sisi wanaume kwenye haya maisha ni upatikanaji wa kile kinachoitwa ridhiki ya familia (mkate wa kila siku).

Hata, kila nipatapo muda wa kutosha huwa siachi kuusikiliza tena na tena ule wimbo unaoimba; ‘wanaume tumeumbwa mateso ooh matesoo kuhangaika’, ulioimbwa na bendi ya Msondo - Ngoma ya Ukae (TX – William Moshi, Gurumo, Maina, Romario, Jumbe, Uvuruge & Mwanyiro), utunzi maridadi wa Maalim Mzee Gurumo na uimbaji mujarabu ulioongozwa na TX – William Moshi (marehemu kwa sasa). Tuzidi kuwaombea hawa wanaume wenzetu wawe na kauli thabiti mbele ya Allah (swt) kwa kutuachia jumbe zilizotukuka kutoka kwenye nyimbo zao. Wimbo huu ni miongozi mwa nyimbo chache zinipazo nguvu thabiti mara tatu zaidi ya nguvu niipatayo katika kinywaji chochote cha kuongeza nguvu (Energy Drink).

Sisi wanaume, ni mambo mengi tunayokumbana nayo katika mazingira ya kila siku ya kiutafutaji na mapambano ya maisha kama vile; migogoro, chuki, fujo, ajali na hatari nyingi za maisha kuliko wenzetu jinsia pinzani (wanawake). Yote haya huchosha miili na akili zetu na kupelekea tupate magonjwa mengi yakiwemo haya magonjwa mapya ya Kizungu kama vile Presha & Stress (Msongo wa mawazo). Pengine hii ndiyo sababu inayotufanya wanaume wengi tufe mapema, siku hizi wanaume hatudumu, tunapukutika tu kama masiala au ninyi mnaonaje, wanaume wenzangu?

Utafiti usio rasmi nilioufanya siku chache zilizopita unanifanya nitoke kifua mbele na kusema waziwazi kuwa, licha ya uchache wetu kiidadi katika sensa bado siku hizi wanaume tunakufa zaidi kuliko wanawake. Katika kila misiba kumi (10) utakayoisikia, ukichunguza uzuri utagundua kuwa marehemu sita (6) au zaidi ni wanaume, wewe unadhani ni kwanini? Majibu ya tafiti zingine nyingi zilizofanywa na watu binafsi ama taasisi mbalimbali yanatanabaisha sababu zingine juu ya swali la msingi kwanini wanaume wanakufa mapema na kuwaacha wake zao; ngoja nikushirikishe sababu hizi:

1. Msongo wa mawazo (stress): wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena ya matatizo yao na matatizo ya jamii/familia (watu wengine wa karibu wanaowazunguka kama vile; mke, watoto na wazazi wao). Dunia nzima inajua kuwa wanaume ndio wanaohusika na kugharamikia malezi ya familia (mke & watoto) na wakati mwingine wazee wa pande zote mbili. Hata wake zetu wanapokopa madeni huko kwenye vikundi vyao vya VICOBA bado wanatutegemea sisi kuwasaidia kuyalipa madeni yao. Unategemea nini kitokee pale mambo yanapotuzidia kama sio kupata magonjwa ya moyo na presha yanayotufanya tufe mapema wakati mwingine tukiwa tumekaa kwenye viti umauti unatukuta.

2. Kazi hatarishi: wanaume ndio tunaoongoza kwa kufanya zaidi kazi hatarishi duniani kuliko wanawake. Wanaume hulazimika kuajiriwa katika nafasi za kazi ngumu na hatari zaidi, kwa mfano; jeshini, viwandani, migodini, ulinzi na kadhalika. Sio tu kwa sababu wanaume tuna nguvu sana kuliko wanawake bali ni pamoja na ukweli kwamba wanaume hatuna double chance (nafasi mbadala) ya kufaulu kimaisha na kumudu kuendesha familia yake pasipo kujituma na kujishughulisha, tofauti na mwanamke ambaye yeye hata asipojituma anaweza kuolewa na mwanaume mwingine mwenye uwezo akabaki nyumbani na kustarehe. Mwanamke hata akiolewa na kalikonji (maskini) kama mimi, hata asipojituma kuihangaikia familia yake ni mwanaume (mumewe) ndiye atakayeubeba msalaba na kupokea lawama watoto wakilala njaa au wakikosa ada ya masomo.

3. Jamii haitujali sana wanaume: ni nani anayehangaika na matatizo mbalimbali yanayowakabili wanaume kwenye jamii? Nikumbushe - kuna taasisi au asasi ngapi za kiraia kama vile; TAMWA, TAWLA, UWT zinazoshughulikia matatizo ya wanaume kwenye jamii ukilinganisha na hizi za wanawake? Je, kesi za waume kunyanyaswa na familia zao (wake & watoto wao) zinasikilizwa na kutiliwa maanani kama zile za wanawake au ndio wanaume wanaachwa wapambane na hali zao? Ukweli ni kwamba wanakumbana na mambo mengi na mazito kwa sababu hawana pa kukimbilia kuomba msaada kutokana na mtazamo wa jamii kuegemea upande mmoja. Hata katika majanga kwa mfano; ajali, milipuko, ukame, njaa, magonjwa n.k, wanaume hawapewi kipaumbele cha msaada kama wanavyopewa wanawake na watoto, kwanini wasife mapema?

4. Ugomvi: wanaume ni wagomvi zaidi, kuliko wanawake ambao wao vita vyao huishia mdomoni tu (kuchambana). Ugomvi wa wanaume ni wa vitendo zaidi kuliko maneno, na hii huwaweka wanaume kwenye hatari zaidi za kupoteza maisha maema kwa mfano: kuchomwa visu, kupigwa risasi au kuuliwa kwa namna nyingine yeyote. Hakuna sababu za moja kwa moja zinazoeleza kwanini wanaume hupenda kupigana zaidi. Kisaikolojia kupigana hutokea pale mtu anapotafuta namna ya mwisho ya kulinda Heshima yake au kutetea himaya yake. Huenda hali hii ya ugomvi kwa wanaume inasababishwa na wingi wa homoni ya kiume ya testosterone kwenye damu zao.

BABA NI NANI? TUJIKUMBUSHE KIDOGO:

1. Ni mwanaume anayeweza kuvaa pea moja ya kiatu mwaka mzima ili kujinyima akibana matumizi na pesa zote zinazobaki akazitumia kuhudumia familia yake kuhakikisha inapata mavazi, malazi na chakula kwa wakati.

2. Ni mwanaume aliyetayari kutukanwa na kufedheheshwa na kila mtu awapo mahangaikoni na akavumilia ili mradi tu apate ridhiki ya kuipelekea familia yake (mke + watoto).

3. Katika familia nyingi; baba ni mtu wa kwanza kuondoka nyumbani (asubuhi na mapema) na wa mwisho kurudi nyumbani (muda umekwenda sana) kwa ajili ya kuihangaikia familia yake, ipate chochote kitu. Wanafamilia wengine (mama na watoto) wakibakia nyumbani wakikaangiza na kuangalia tamthiliya zilizotafsiriwa kwa Kiswahili na akina Dj Murphy & Dj Mack.

4. Ni mwanaume aliyetayari kupigana na kuhatarisha Maisha yake kwa namna yeyote kwa ajili ya kuwalinda kuhakikisha usalama wa familia yake.

*******
Neno la Mungu kupitia Biblia Takatifu linatufundisha kuishi kwa akili za wake zetu, “… Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake Watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote. Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke Heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima ...” 1 Petro 3: 5-7.

Biblia inatuasa kuwa wanawake Watakatifu wa zamani waliishi vizuri na waume zao sio kama hawa wanawake wetu wa sasa. Tunapewa mfano wa Sara mke wa Ibrahimu (baba wa imani) namna alivyomtii mumewe. Namimi leo hii nakuongezea pointi muhimu ya kukumbuka siku zote kwenye maisha yako, “Ishi na mkeo kwa uaminifu ila usimuamini”, kwa sababu hawa viumbe hubadilika muda wowote na huwa hawachelewi kubadilisha maneno na uhalisia wake. Ndio maana hata inapotokea wazazii wanalazimika kutalakiana, mama hupandikiza chuki kwa watoto dhidi ya baba yao na kumfanya baba aonekane mbaya , mama mzuri siku zote?!!!

Licha ya nguvu nyingi sisi wanaume tunazojitolea katika kuhudumia familia zetu. Kwanini sasa bado hatuonyeshwi upendo na heshima tunayostahili katika familia zetu? Tunatafuta kwa jasho kwa ajili ya kuwasaidia watoto wetu wakikua wanaimba nani kama mama, sisi tunasahaulika?!!! Kwanini watoto wetu wakikua wanawajali na kuwapenda zaidi mama zao kuliko sisi baba zao? Punguza sauti ya redio/tv mpendwa, kama ulikuwa umesimama tafuta kiti uketi, upoe kwanza, nikuonyeshe kosa linapoanzia.

Baba anapokuwa ana nguvu na bado yupo kazini huwa anakua na heshima na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake. Familia humsikiliza na huzingatia sana uwepo wake! Tatizo huanza pale baba anapozeeka na nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, au amestaafu! Pale watoto wanapokua wamekua watu wazima - wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba hugeuka! Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa zamani kama bread winner (mlezi wa familia) huanza kupungua taratibu.

Baba anapozeeka hukosa sauti tena (hasikilizwi kama zamani), isitoshe anakua hahusishwi sana kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa hana cha kusaidia maana pesa hana! Na kosa jingine tunalolifanya wababa ni kuoa wanawake tunaowazidi Miaka mingi kiumri. Wewe umekwisha mkeo ndo kwanza jua la sa sita. Badala yake mke huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe. Mama huanza safari kwenda kwa watoto kusalimia mara kwa mara, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lakini baba hakuna anayemtaka.

Wakiwa nyumbani yeye na mkewe, simu zinazopigwa kutoka kwa watoto, asilimia 90% anapigiwa mama tu. Baada ya maongezi marefu, ndio baba hupewa simu, anasalimiwa dakika mbili tu, imeisha hiyoo! Baba simu anayo, ila haoni sms wala calls za watoto wake wakimpigia. Ikitokea wamempigia ni kwa sababu maalumu tu, tena maongezi yanakuwa mafupi sana! Kiufupi hawana mzuka wala muda nae! Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe aliyoipigania kwa nguvu zote enzi za ujana wake!

Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae tena! Pale anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake kwa sababu ameshazeeka. Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke msongo wa mawazo unamkumba, na kufanya kinga ya mwili kushuka mwili unarusu kushambuliwa na magonjwa nyemelezi na haichukui muda anafariki! Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia jeneza la gharama na kumjengea kaburi zuri, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai, hakuna aliyemjali!

USHAURI KWA WANAUME KUMWEPA DHAHAMA HII:

1. Unapomwachia mkeo pesa ya chakula ya siku wenyewe mnaita kodi ya meza - mwachie hadharani (mkiwa mbele ya watoto) ili hata watoto wajue kuwa, baba ndiye anayehudumia familia. Wanawake wapumbavu ni wafitini – ukimuachia pesa ya matumizi chumbani mkiwa wawili tu atanunua chakula na kuwadanganya watoto kuwa yeye ndiye anayehudumia familia. “Mnaona ninavyowahangaikia, nimehemea vyote hivi na kuwapikia chakula kitamu. Mlishawahi kumuona baba yenu hata siku moja akinisaidia kazi? wenyewe - mnaona ninavyowapenda wanangu”, huwa wanasema hivyo. Kwa sumu hiyo ya maneno wanayolishwa watoto unategemea watakupenda na kukuheshimu watakapokua? Jibu unalo mwenyewe.

2. Mtoto akiomba ada mkabidhi mwenyewe ikiwezekana nenda naye shule/benki ukamlipie akiwa anashuhudia ajue mapema kabisa kuwa baba ndiye anayelipa ada za shule. Usimwachie pesa ya ada za shule za watoto mkeo. Ni kweli hata ukimwachia mkeo hatazitumia vibaya - atawapa watoto lakini mwanamke mpumbavu hatakuacha salama. Asiposema kuwa ameitafuta mwenyewe wewe baba uligoma kutoa atasema amekubembeleza sana haukuwa tayari kuwalipia watoto wako ada za shule.

3. Usitoe adhabu kwa watoto baada ya mama yao kukushitakia makosa waliyoyafanya watoto mchana muda ambao wewe hukuwepo nyumbani. Mtoto anaweza kukosea mchana lakini mama yake asitoe adhabu utasikia, “Subiri baba yako aje utamkoma.” Kila mzazi ana wajibu sawa wa kuonya na kuadhibu pindi mtoto wake anapokosea, lakini wake zetu hukwepa lawama kwa watoto kwa kutusubiri akinababa tuje tutoe adhabu ili watoto watuone hatuwapendi. Usinase kwenye mtego huo kijinga, watoto hubaki na Kumbukumbu ambazo huishi nazo mpaka ukubwani ni nani alikuwa akiwapenda/akiwanyanyasa, unategemea uzeeni kwako watakupenda?

4. Pesa ya nguo za sikukuu za watoto na zake mwachie mkeo mbele ya watoto, ili hata kama mama yao atakwenda kuwanunulia, wakipendeza wasisahau kuwa ni wewe (baba) ndiye uliyetoa pesa na mama yao amekwenda kuwanunulia tu, kiufupi amefanya kazi yake ya kuwachagulia tu kilicho bora. Ikiwezekana wakati mwingine, ingia madukani wewe mwenyewe wanunulie wanao nguo moja kwa moja, fanya hivyo utakuja kunishukuru baadae.

5. Watoto wakiomba pesa ya matumizi binafsi, wakati mwingine wape moja kwa moja wewe mwenyewe usimwachie mkeo awape - atawajaza maneno kuwa ni yeye amekopa kwenye vikundi vya VICOBA vya akinamama wenzie ili kukidhi mahitaji yao wewe baba yao ulisema huna pesa ya kuchezea.

6. Hata kama uko bize kiasi gani, jitahidi kutenga muda wa kufurahi na watoto wako ili wakuzoee, walifaidi pendo lako kama baba. hata ikitokea umechelewa kurudi nyumbani wakumisi. Leo hii ni akinababa wangapi wenye ukaribu/urafiki na watoto wao? Baba una wajibu pia wa kushiriki katika malezi ya watoto wako. Sometimes msaidie mkeo kuwabadilisha japo pampasi watoto wakijisaidia, cheza nao, usijenge uadui na watoto wako. Sasa wewe endelea kutafuta Heshima za kijinga kwa kutaka kila mtu akuogope mziki utaucheza vizuri huko uzeeni.

7. Jifunze kubeba zawadi kwa ajili ya familia yako (mke + watoto) kila unaporudi nyumbani kutoka mahangaikoni. Baba usirudi mikono mitupu hata kama umeacha pesa nyingi kiasi gani nyumbani za kukidhi mahitaji yote. Chochote kitu ni bora zaidi kuliko mikono mitupu, zawadi zina mchango mkubwa zaidi katika kuimarisha uhusiano mzuri baina ya mleta zawadi na mletewaji.

Tuwajali baba zetu tangu wanapokuwa hai, walijitoa na kujinyima sana ili kutufanya tufike tulipo kwa sasa. Ni dhambi mbele za Mungu, tena ni laana mbaya sana kuwapuuza baba zetu. “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja sikuile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee baba zao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.

******
Hongera kwa kusoma makala hii mpaka mwisho.

Asante.
 
Ahsante kwa makala hii, ni ndefu lakini nimesoma yote, baadhi ya uliyoyaandika huwa nafanya ,lakini nimepata elimu zaidi. NATAMANI NINGEIPATA KWENYE EMAIL AU WHATSAPP YANGU
 
Asante ubalikiwe sana kaka maana wanaume sikuizi nikama tumeivamia hii dunia na hatusitahili kuishi kabisa

yaan hata wanafunzi wakifanya mapenzi kwa laha zao yule wakike ikatokea bahati mbaya akapata mimba sheria zinaelekea anayetakiwa kufutwa juu ya uso wa dunia ni mtoto wa kiume 30 jela

Huku mtoto wa kike anabaki anasambaza upendo kwa wengine
Hii inaumiza sana na ndio maana hata watoto wa mitaani kamwe hawawezi kuisha

Maana watunga sheria wanatazama mtoto wa kike na haki zake tu,
Kuhusu mtoto wa kiume nikama kiumbe aliyevamia hii sayari kwa bahati mbaya na hasiye stahili kabisa kuishi ktk hii dunia

Sina uhakika sana na kule tuendako hofu yangu ni kwamba hii habari ya haki sawa ipo siku itatungwa sheria ya kumradhimisha mtoto wa kiume naye abebe mimba
Ili twende sawa
 
Asante ubalikiwe sana kaka maana wanaume sikuizi nikama tumeivamia hii dunia na hatusitahili kuishi kabisa

yaan hata wanafunzi wakifanya mapenzi kwa laha zao yule wakike ikatokea bahati mbaya akapata mimba sheria zinaelekea anayetakiwa kufutwa juu ya uso wa dunia ni mtoto wa kiume 30 jela

Huku mtoto wa kike anabaki anasambaza upendo kwa wengine
Hii inaumiza sana na ndio maana hata watoto wa mitaani kamwe hawawezi kuisha

Maana watunga sheria wanatazama mtoto wa kike na haki zake tu,
Kuhusu mtoto wa kiume nikama kiumbe aliyevamia hii sayari kwa bahati mbaya na hasiye stahili kabisa kuishi ktk hii dunia

Sina uhakika sana na kule tuendako hofu yangu ni kwamba hii habari ya haki sawa ipo siku itatungwa sheria ya kumradhi isha mtoto wa kiume naye abebe mimba
Ili twende sawa
Bado kwenye elimu mwanamke anapewa kipaombele hata akipata max ndogo
 
Makala nzuri sana. Somo la muhimu hapo ni ukaribu na watoto ni muhimu zaidi kuliko kulipa ada na kodi. Tupambane kutafuta maisha na pia tuwe na ukaribu na familia.
 
WABABA: CHANGAMOTO ZA MALEZI YA WATOTO & SABABU ZA KUFA MAPEMA. JE, WAMAMA WANAHUSIKA?!!View attachment 1855904

Wanaume ee,

Mnajionaje na hali wapambanaji wenzangu?!! Poleni na hongereni kwa siku nyingine tena. Ni matumaini yangu mko poa sana, mkiendelea na majukumu ya kila siku ya hapa na pale katika kuhakikisha heshima zenu kama waume na baba majumbani kwenu zinaendelea kujengeka vizuri. Iko uchi (wazi) kuwa, ni wajibu wa baba kuhakikisha familia inapata mahitaji yote muhimu ya kimaisha hususani malazi, mavazi na chakula ili watoto waendelee kupishana pishana kila mara kuingia na kutoka mlango wa chooni. Furaha ya mwanaume yeyote rijali ni kuona familia yake inasonga mbele, sawia?

Nazijua nukuu nyingi tu zitutiazo nguvu za kupambana na kutufanya tuwe na mioyo yabisi (migumu) katika kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha bila kuchoka. “Mwanaume hajaumbwa kushindwa, anaweza kuharibiwa mipango yake lakini kamwe hashindwi” – Ernest Hemingway. ‘Kuwa mwanaume ni juu ya kuchukua jukumu na kutumia nguvu yako kuwatumikia wengine katika kuunda na kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii/familia yako’ – Francis Bacon. Kinachotufanya tuteseke sana sisi wanaume kwenye haya maisha ni upatikanaji wa kile kinachoitwa ridhiki ya familia (mkate wa kila siku).

Hata, kila nipatapo muda wa kutosha huwa siachi kuusikiliza tena na tena ule wimbo unaoimba; ‘wanaume tumeumbwa mateso ooh matesoo kuhangaika’, ulioimbwa na bendi ya Msondo - Ngoma ya Ukae (TX – William Moshi, Gurumo, Maina, Romario, Jumbe, Uvuruge & Mwanyiro), utunzi maridadi wa Maalim Mzee Gurumo na uimbaji mujarabu ulioongozwa na TX – William Moshi (marehemu kwa sasa). Tuzidi kuwaombea hawa wanaume wenzetu wawe na kauli thabiti mbele ya Allah (swt) kwa kutuachia jumbe zilizotukuka kutoka kwenye nyimbo zao. Wimbo huu ni miongozi mwa nyimbo chache zinipazo nguvu thabiti mara tatu zaidi ya nguvu niipatayo katika kinywaji chochote cha kuongeza nguvu (Energy Drink).

Sisi wanaume, ni mambo mengi tunayokumbana nayo katika mazingira ya kila siku ya kiutafutaji na mapambano ya maisha kama vile; migogoro, chuki, fujo, ajali na hatari nyingi za maisha kuliko wenzetu jinsia pinzani (wanawake). Yote haya huchosha miili na akili zetu na kupelekea tupate magonjwa mengi yakiwemo haya magonjwa mapya ya Kizungu kama vile Presha & Stress (Msongo wa mawazo). Pengine hii ndiyo sababu inayotufanya wanaume wengi tufe mapema, siku hizi wanaume hatudumu, tunapukutika tu kama masiala au ninyi mnaonaje, wanaume wenzangu?

Utafiti usio rasmi nilioufanya siku chache zilizopita unanifanya nitoke kifua mbele na kusema waziwazi kuwa, licha ya uchache wetu kiidadi katika sensa bado siku hizi wanaume tunakufa zaidi kuliko wanawake. Katika kila misiba kumi (10) utakayoisikia, ukichunguza uzuri utagundua kuwa marehemu sita (6) au zaidi ni wanaume, wewe unadhani ni kwanini? Majibu ya tafiti zingine nyingi zilizofanywa na watu binafsi ama taasisi mbalimbali yanatanabaisha sababu zingine juu ya swali la msingi kwanini wanaume wanakufa mapema na kuwaacha wake zao; ngoja nikushirikishe sababu hizi:

1. Msongo wa mawazo (stress): wanaume ndio wabebaji wakubwa wa shehena ya matatizo yao na matatizo ya jamii/familia (watu wengine wa karibu wanaowazunguka kama vile; mke, watoto na wazazi wao). Dunia nzima inajua kuwa wanaume ndio wanaohusika na kugharamikia malezi ya familia (mke & watoto) na wakati mwingine wazee wa pande zote mbili. Hata wake zetu wanapokopa madeni huko kwenye vikundi vyao vya VICOBA bado wanatutegemea sisi kuwasaidia kuyalipa madeni yao. Unategemea nini kitokee pale mambo yanapotuzidia kama sio kupata magonjwa ya moyo na presha yanayotufanya tufe mapema wakati mwingine tukiwa tumekaa kwenye viti umauti unatukuta.

2. Kazi hatarishi: wanaume ndio tunaoongoza kwa kufanya zaidi kazi hatarishi duniani kuliko wanawake. Wanaume hulazimika kuajiriwa katika nafasi za kazi ngumu na hatari zaidi, kwa mfano; jeshini, viwandani, migodini, ulinzi na kadhalika. Sio tu kwa sababu wanaume tuna nguvu sana kuliko wanawake bali ni pamoja na ukweli kwamba wanaume hatuna double chance (nafasi mbadala) ya kufaulu kimaisha na kumudu kuendesha familia yake pasipo kujituma na kujishughulisha, tofauti na mwanamke ambaye yeye hata asipojituma anaweza kuolewa na mwanaume mwingine mwenye uwezo akabaki nyumbani na kustarehe. Mwanamke hata akiolewa na kalikonji (maskini) kama mimi, hata asipojituma kuihangaikia familia yake ni mwanaume (mumewe) ndiye atakayeubeba msalaba na kupokea lawama watoto wakilala njaa au wakikosa ada ya masomo.

3. Jamii haitujali sana wanaume: ni nani anayehangaika na matatizo mbalimbali yanayowakabili wanaume kwenye jamii? Nikumbushe - kuna taasisi au asasi ngapi za kiraia kama vile; TAMWA, TAWLA, UWT zinazoshughulikia matatizo ya wanaume kwenye jamii ukilinganisha na hizi za wanawake? Je, kesi za waume kunyanyaswa na familia zao (wake & watoto wao) zinasikilizwa na kutiliwa maanani kama zile za wanawake au ndio wanaume wanaachwa wapambane na hali zao? Ukweli ni kwamba wanakumbana na mambo mengi na mazito kwa sababu hawana pa kukimbilia kuomba msaada kutokana na mtazamo wa jamii kuegemea upande mmoja. Hata katika majanga kwa mfano; ajali, milipuko, ukame, njaa, magonjwa n.k, wanaume hawapewi kipaumbele cha msaada kama wanavyopewa wanawake na watoto, kwanini wasife mapema?

4. Ugomvi: wanaume ni wagomvi zaidi, kuliko wanawake ambao wao vita vyao huishia mdomoni tu (kuchambana). Ugomvi wa wanaume ni wa vitendo zaidi kuliko maneno, na hii huwaweka wanaume kwenye hatari zaidi za kupoteza maisha maema kwa mfano: kuchomwa visu, kupigwa risasi au kuuliwa kwa namna nyingine yeyote. Hakuna sababu za moja kwa moja zinazoeleza kwanini wanaume hupenda kupigana zaidi. Kisaikolojia kupigana hutokea pale mtu anapotafuta namna ya mwisho ya kulinda Heshima yake au kutetea himaya yake. Huenda hali hii ya ugomvi kwa wanaume inasababishwa na wingi wa homoni ya kiume ya testosterone kwenye damu zao.

BABA NI NANI? TUJIKUMBUSHE KIDOGO:

1. Ni mwanaume anayeweza kuvaa pea moja ya kiatu mwaka mzima ili kujinyima akibana matumizi na pesa zote zinazobaki akazitumia kuhudumia familia yake kuhakikisha inapata mavazi, malazi na chakula kwa wakati.

2. Ni mwanaume aliyetayari kutukanwa na kufedheheshwa na kila mtu awapo mahangaikoni na akavumilia ili mradi tu apate ridhiki ya kuipelekea familia yake (mke + watoto).

3. Katika familia nyingi; baba ni mtu wa kwanza kuondoka nyumbani (asubuhi na mapema) na wa mwisho kurudi nyumbani (muda umekwenda sana) kwa ajili ya kuihangaikia familia yake, ipate chochote kitu. Wanafamilia wengine (mama na watoto) wakibakia nyumbani wakikaangiza na kuangalia tamthiliya zilizotafsiriwa kwa Kiswahili na akina Dj Murphy & Dj Mack.

4. Ni mwanaume aliyetayari kupigana na kuhatarisha Maisha yake kwa namna yeyote kwa ajili ya kuwalinda kuhakikisha usalama wa familia yake.

*******
Neno la Mungu kupitia Biblia Takatifu linatufundisha kuishi kwa akili za wake zetu, “… Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake Watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote. Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke Heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima ...” 1 Petro 3: 5-7.

Biblia inatuasa kuwa wanawake Watakatifu wa zamani waliishi vizuri na waume zao sio kama hawa wanawake wetu wa sasa. Tunapewa mfano wa Sara mke wa Ibrahimu (baba wa imani) namna alivyomtii mumewe. Namimi leo hii nakuongezea pointi muhimu ya kukumbuka siku zote kwenye maisha yako, “Ishi na mkeo kwa uaminifu ila usimuamini”, kwa sababu hawa viumbe hubadilika muda wowote na huwa hawachelewi kubadilisha maneno na uhalisia wake. Ndio maana hata inapotokea wazazii wanalazimika kutalakiana, mama hupandikiza chuki kwa watoto dhidi ya baba yao na kumfanya baba aonekane mbaya , mama mzuri siku zote?!!!

Licha ya nguvu nyingi sisi wanaume tunazojitolea katika kuhudumia familia zetu. Kwanini sasa bado hatuonyeshwi upendo na heshima tunayostahili katika familia zetu? Tunatafuta kwa jasho kwa ajili ya kuwasaidia watoto wetu wakikua wanaimba nani kama mama, sisi tunasahaulika?!!! Kwanini watoto wetu wakikua wanawajali na kuwapenda zaidi mama zao kuliko sisi baba zao? Punguza sauti ya redio/tv mpendwa, kama ulikuwa umesimama tafuta kiti uketi, upoe kwanza, nikuonyeshe kosa linapoanzia.

Baba anapokuwa ana nguvu na bado yupo kazini huwa anakua na heshima na ushawishi mkubwa sana kwenye familia yake. Familia humsikiliza na huzingatia sana uwepo wake! Tatizo huanza pale baba anapozeeka na nguvu za uzalishaji mali zimekwisha, au amestaafu! Pale watoto wanapokua wamekua watu wazima - wameanza maisha yao! Hapo ndipo mambo kwa baba hugeuka! Mkewe huanza kumchukulia poa! Ile heshima aliyokuwa akipewa zamani kama bread winner (mlezi wa familia) huanza kupungua taratibu.

Baba anapozeeka hukosa sauti tena (hasikilizwi kama zamani), isitoshe anakua hahusishwi sana kwenye mambo ya mkewe sababu hata akiambiwa hana cha kusaidia maana pesa hana! Na kosa jingine tunalolifanya wababa ni kuoa wanawake tunaowazidi Miaka mingi kiumri. Wewe umekwisha mkeo ndo kwanza jua la sa sita. Badala yake mke huanza kuwafanya watoto kuwa washirika wake zaidi na kumuweka kando mumewe. Mama huanza safari kwenda kwa watoto kusalimia mara kwa mara, huko hukaa sana, baba kaachwa nyumbani peke yake! Watoto wanagombea mama aende kwao, lakini baba hakuna anayemtaka.

Wakiwa nyumbani yeye na mkewe, simu zinazopigwa kutoka kwa watoto, asilimia 90% anapigiwa mama tu. Baada ya maongezi marefu, ndio baba hupewa simu, anasalimiwa dakika mbili tu, imeisha hiyoo! Baba simu anayo, ila haoni sms wala calls za watoto wake wakimpigia. Ikitokea wamempigia ni kwa sababu maalumu tu, tena maongezi yanakuwa mafupi sana! Kiufupi hawana mzuka wala muda nae! Baba anajikuta anakuwa mpweke sana, anakua mgeni kwa familia yake mwenyewe aliyoipigania kwa nguvu zote enzi za ujana wake!

Wale ambao alizimalizia nguvu zake za ujana kuwatafutia hawana muda nae tena! Pale anapokuwa anaihitaji sana faraja ya familia yake kwa sababu ameshazeeka. Familia humpa kisogo! Upweke unamsonga! Sababu ya upweke msongo wa mawazo unamkumba, na kufanya kinga ya mwili kushuka mwili unarusu kushambuliwa na magonjwa nyemelezi na haichukui muda anafariki! Familia wataliaa, watachapisha matisheti, watatoa mapesa kumnunulia jeneza la gharama na kumjengea kaburi zuri, mitandaoni watampost sana! Lakini alipokuwa hai, hakuna aliyemjali!

USHAURI KWA WANAUME KUMWEPA DHAHAMA HII:

1. Unapomwachia mkeo pesa ya chakula ya siku wenyewe mnaita kodi ya meza - mwachie hadharani (mkiwa mbele ya watoto) ili hata watoto wajue kuwa, baba ndiye anayehudumia familia. Wanawake wapumbavu ni wafitini – ukimuachia pesa ya matumizi chumbani mkiwa wawili tu atanunua chakula na kuwadanganya watoto kuwa yeye ndiye anayehudumia familia. “Mnaona ninavyowahangaikia, nimehemea vyote hivi na kuwapikia chakula kitamu. Mlishawahi kumuona baba yenu hata siku moja akinisaidia kazi? wenyewe - mnaona ninavyowapenda wanangu”, huwa wanasema hivyo. Kwa sumu hiyo ya maneno wanayolishwa watoto unategemea watakupenda na kukuheshimu watakapokua? Jibu unalo mwenyewe.

2. Mtoto akiomba ada mkabidhi mwenyewe ikiwezekana nenda naye shule/benki ukamlipie akiwa anashuhudia ajue mapema kabisa kuwa baba ndiye anayelipa ada za shule. Usimwachie pesa ya ada za shule za watoto mkeo. Ni kweli hata ukimwachia mkeo hatazitumia vibaya - atawapa watoto lakini mwanamke mpumbavu hatakuacha salama. Asiposema kuwa ameitafuta mwenyewe wewe baba uligoma kutoa atasema amekubembeleza sana haukuwa tayari kuwalipia watoto wako ada za shule.

3. Usitoe adhabu kwa watoto baada ya mama yao kukushitakia makosa waliyoyafanya watoto mchana muda ambao wewe hukuwepo nyumbani. Mtoto anaweza kukosea mchana lakini mama yake asitoe adhabu utasikia, “Subiri baba yako aje utamkoma.” Kila mzazi ana wajibu sawa wa kuonya na kuadhibu pindi mtoto wake anapokosea, lakini wake zetu hukwepa lawama kwa watoto kwa kutusubiri akinababa tuje tutoe adhabu ili watoto watuone hatuwapendi. Usinase kwenye mtego huo kijinga, watoto hubaki na Kumbukumbu ambazo huishi nazo mpaka ukubwani ni nani alikuwa akiwapenda/akiwanyanyasa, unategemea uzeeni kwako watakupenda?

4. Pesa ya nguo za sikukuu za watoto na zake mwachie mkeo mbele ya watoto, ili hata kama mama yao atakwenda kuwanunulia, wakipendeza wasisahau kuwa ni wewe (baba) ndiye uliyetoa pesa na mama yao amekwenda kuwanunulia tu, kiufupi amefanya kazi yake ya kuwachagulia tu kilicho bora. Ikiwezekana wakati mwingine, ingia madukani wewe mwenyewe wanunulie wanao nguo moja kwa moja, fanya hivyo utakuja kunishukuru baadae.

5. Watoto wakiomba pesa ya matumizi binafsi, wakati mwingine wape moja kwa moja wewe mwenyewe usimwachie mkeo awape - atawajaza maneno kuwa ni yeye amekopa kwenye vikundi vya VICOBA vya akinamama wenzie ili kukidhi mahitaji yao wewe baba yao ulisema huna pesa ya kuchezea.

6. Hata kama uko bize kiasi gani, jitahidi kutenga muda wa kufurahi na watoto wako ili wakuzoee, walifaidi pendo lako kama baba. hata ikitokea umechelewa kurudi nyumbani wakumisi. Leo hii ni akinababa wangapi wenye ukaribu/urafiki na watoto wao? Baba una wajibu pia wa kushiriki katika malezi ya watoto wako. Sometimes msaidie mkeo kuwabadilisha japo pampasi watoto wakijisaidia, cheza nao, usijenge uadui na watoto wako. Sasa wewe endelea kutafuta Heshima za kijinga kwa kutaka kila mtu akuogope mziki utaucheza vizuri huko uzeeni.

7. Jifunze kubeba zawadi kwa ajili ya familia yako (mke + watoto) kila unaporudi nyumbani kutoka mahangaikoni. Baba usirudi mikono mitupu hata kama umeacha pesa nyingi kiasi gani nyumbani za kukidhi mahitaji yote. Chochote kitu ni bora zaidi kuliko mikono mitupu, zawadi zina mchango mkubwa zaidi katika kuimarisha uhusiano mzuri baina ya mleta zawadi na mletewaji.

Tuwajali baba zetu tangu wanapokuwa hai, walijitoa na kujinyima sana ili kutufanya tufike tulipo kwa sasa. Ni dhambi mbele za Mungu, tena ni laana mbaya sana kuwapuuza baba zetu. “Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja sikuile ya BWANA, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee baba zao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.

******
Hongera kwa kusoma makala hii mpaka mwisho.

Asante.
Ubarikiwe sana Mkuu
 
halafu mwanaume huyohuyo anatakiwa awe na nguvu za kiume
 
Back
Top Bottom