Zogoo da khama
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 622
- 582
Waungwana khali zenu,
Leo nakuja na maada ambayo inaigusa jamii hasa ya waliokwenye mahusiano
(kwa maana ya mapenzi) mjadala huu umetawala hisia za wengi na hata Toleo la juzi la RAIA Mwema Toleo Na:330 ukurasa wa 18 kwenye Kona ya Privatus Karugendo nimeikuta .
Kwa kifupi ni changamoto za ndoa, Mahusiano.
Tata Madiba heshima yake ilipanda juu zaidi baada ya kujitokeza kama mtu mwenye kusamehe na kusahau.
Mfano,
Aliwasamehe waliomfunga na kumtesa kwa kipindi cha miaka 27, aliwasamehe wale walioendesha mauaji ya waafrika wa Soweto, watoto wa Soweto waliotetea haki zao za msingi.
Sasa swala au mada yetu kuu ambayo ningependa tuijadili katika jukwaa letu ni kwanini Madiba aliwasamehe watu wote hadi wauaji, akashindwa kumsamehe mke wake Winnie? Winnie alifanya kosa gani kubwa kiasi cha kutopata msamaha? Na Je ingelikuwa ni wewe ungefanyaje?
Haya mambo yanatokea katika jamii zetu, mfano hai, kuna mwanamuziki mmoja alipokuwa kwenye kambi ya BSS mkewe wa ndoa alimsaliti na kibaya zaidi alikuwa mjamzito, jamaa alimsamehe mapenzi yakaendelea, haya sasa tuanze mjadala wetu, Je!! Mume/Mke ukisalitiwa na mwenza wako uko tayari kusamehe na maisha yakaendelea? karibuni