Changamoto za maendeleo kwa Amiri Jeshi wetu

Huduma

Member
Jan 26, 2008
68
1
MAMBO mengi makubwa huko Amerika chanzo chake ni tafiti na ugunduzi uliofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo. China, Russia, Korea na Japan hali kadhalika sehemu yao kubwa ya maendeleo imetokana na kazi na shughuli za majeshi ya nchi hizo hapo siku za nyuma. Mojawapo ni hii blogi tunayoitumia leo ambayo asili yake ni internet ambayo iligunduliwa na jeshi la Marekani. NJe, sisi tuna mipangogani ya kulipa jeshi letu changamoto ili liweze kutukwamua kutoka kwenye umasikini.

JE JESHI LINAWEZA wakati huu wa amani pamoja na kuendelea na kazi zake za ulinzi kuanza kushughulikia ULINZI WA AINA mpya sasa ambao pengine ni muhimu kuliko Ulinzi wa mipaka:

. Tuanze kujilinda huko huko kwenye matatizo na siyo mipaka yetu. Kupeleka majeshi Kongo ili kuwaondoa wahuni na nchi itawalike. Aidha Burundi, Somalia, Chad na Afrika ya Kati. Kote huku nchi za magharibi zinajihakikishia upatikanaji wa uranium kwa bei rahisi kutokana na kuendelwa kuwepo mitafaruku na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

. Ulinzi muhimu sana ni ule wa kujilinda na chakula kibovu toka nje. Je, jeshi letu linaweza kuwezeshwa kwanza kwa matrekta toka nje na kisha kupewa changamoto ya kutengeneza matrekta yetu wenyewe kama vile Nyumbu ilivyotengenezwa?

. Ulinzi muhimu pia ni kwa nchi kuwa na maji safi ya kutosha ili kuondokana na mabalaa ya kila aina ambayo yanaweza kuua asilimia kubwa ya watu wetu hata kuliko vita vya kawaida. Kwanini jeshi lisipewer ruhusa na kuwezeshwa ili kuhakikisha maji ya maziwa makubwa yanayotuzunguka yanainufaisha Tanzania sawasawa na yanavyowanufaisha watu wengine? Ninadhani jeshi watalielewa hili zaidi kuliko mvua za ndege zinazopiga mabomu mawingu.

. Kwanini jeshi wasiwe na vituo mbalimbali vya utafiti vitakavyoweza kuchangia Tanzania kuwa na vyanzo vinavyoaminika na kutabirika vya mali ghafi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, viwanda vya msingi,

. Ulinzi sasa hivi haupo kabisa katika masuala ya TEKNOHAMA na tusishangae nyaraka za serikali na fedha kwenye mabenki yatakapoanzwa kuibwa na wataalamu wa nje na ndani tunaowajiri leo. Ni muhimu kwa jeshi letu pia kujikita kwenye eneo hili kwa kuwa na wasomi angalau wachache lakini ambao wamepevuka na kupitukia katika masuala ya TEKNOHAMA.

. Mpaka leo tumeshindwa kuwa na MELI za maana za kivita kwa ajili ya ULINZI wa bahari, maziwa na pengine mito yetu. Je, Jeshi limepewa changamoto gani katika hili. Au tutawaachia watu tu kutoka kilomita elfu kadhaa kuja kuvua kamba na samaki wengine kwenye maeneo yetu huku watu wetu wakiendelea kuwa masikini?

. Sanjari na hilo ni ule ukweli pia kuwa ULINZI mkubwa sana unahitajika katika kulinda madini yetu. Na hili haliwezekani ila kwa kuwa na wasomi wa jiolojia au sayansi ya madini na vilevile nchi kuwa na uwezo wa kuigilizia angalau mashine chache za msingi zinazohitajika katika uchimbaji madini. Kama vile jeshi lilivyoweza kutengeneza madaraja kwa siku kama sio masaa machache ni lazima jeshi letu tukufu liepewe changamoto inayolingana na saizi yake nayo ni kutengeneza mashine na mitambo ya kuchimba madini ili tuondokane na vibaka na wezi wa kimataifa.

. Nina hakika jeshi letu linaweza kutengeneza pia darubini na vifaa vingine vya kufuatilia matukio na majambo au kuziboresha zilizopo ili kulinda pia wanyama wetu kama rasilimali asili.

. Kwa kushirikiana na nchi kama Uchina, Korea, Brazili, Venezuela na kadhalika jeshi letu lina uwezo wa kuanza kutengeneza ndege ndogo na zile za kivita kama kanchi kadogo ka-Israel kilivyoweza. Tatizo ni kuwa tunajirudisha nyuma tu na kutaka kuendelea kuwa watu wa kufadhiliwa wakati ambapo wachimbaji madini wakitulipa fedha nzuri pakawa na ziada ya kutosha hivi vitu wallahi vile tunaweza kuvifanya sie. Sio tunakuwa na marubani wa kijeshi wanaoishia kufa kwa kunywa kupita kiasi eti tu kwa kukosa changamoto. Maana ukishajua kuendesha ndege hakuna jipya tena. Rubani huyo angelihitaji leo awe anatangeneza ndege mpya sio kukarabati iliyopo.


TAFAKARI: Wizi wa mawazo hauna tofauti na wizi au ufisadi wa aina nyingine. Angalau kiri mawazo haya si yako umeyapata toka kwa mtu mwingine.

ideas.unlimited
 
WATANZANIA WENYE UWEZO NA VIPAJI VYA UVUYMBUZI WAPO TATIZO SERIKALI NA ROHO MBAYA!

MFANO: OTHMAN OMARI MSEKENI

Alirekebisha landrover kubeba mizinga tukamshinda nduli Iddi Amin Dadah na leo tumemsahau!

HII habari kwa kweli imekuja wakati mwafaka sana. Wakati ambao vyombo vya habari huru vimeanza kufichua jinsi ambavyo wanasiasa na viongozi wa serikali wanavyodumaza na kuviua vipaji vya Watanzania ambao wana uwezo wa kuondosha umasikini, ujinga na maradhi nchini hapa kwa sababu tu za uchoyo,wivu, ubinafsi na kupapatikia wazungu.

Yarabi alaani kizazi cha wale wote wanaodumaza uwezo na vipaji vya watoto wa wengine eti tu kwa sababu sio jamaa zao kwa kuhakikisha kile kizazi chao kinachoshika kinageuka mawe; kile wanachokula kinakuwa najisi; na hewa wanayovuta inageuka sumu!


Dear waziri kalala,
Dear waziri kalala,
 
OTHMAN OMARI MSEKENI

BWANA huyu kama sikosei ndiye yule mgunduzi wa Kifaa cha kuzalishia umeme kinachotumia upepo.

Kufikia hadi hapo alipowezesha chombo hicho kufanya kazi hajapata msaada wowote wa maana toka serikalini.


Kumbukeni hii ni nchi isiyokuwa na utamaduni wa research and development.

Na sababu kubwa ni kuwa viongozi wakishachaguliwa wao huwa wanahesabu wamekwishafika kwa miaka mitano kama sio kumi. Kwa maneno mwingine kila uchaguzi Tanzania ni kitendo cha kudumaza maendeleo yetu na uwezo wa kutatua matatizo yetu kwa miaka sio chini ya mitano kila baada ya miaka mitano mingine iliyopotea bure.

Watu wanaelekea kuliogopa hili lakini wakati umefika wa kuwaambia viongozi wetu wako uchi. Tutaendelea hadi lini kutegemea sindano hadi magari kama sio meli na ndege kutoka Ulaya. Hivi wahandisi wote tuliwafundisha elimu yao haifikii hata robo ya elimu ya kutafuta mwenyewe ya Mzee Othman Omari Msekeni na wanajihesabu ni wasomi au wakoma?

Tunamuomba Rais wetu mpendwa aliingilie jambo hili kati na kuhakikisha Mzee Othman Omari Msekeni anaanzishiwa chuo maalum cha ufundi kwa lugha ya Kiswahili na kuwaonesha watu uwezo wa mambo haya bwana auhitaji Kiingereza bali kuelewa jambo na majaliwa ya kuwa na kipaji mukaramah.

Hivi Wizara ya Sayansi na Teknolojia ipo? Na toka ilipoanzishwa imewahi kufanya nini cha kubadili maisha ya Mtanzania au ni tafiti za wasomi wa kubabaisha zinazoishia kula vumbi na matandu ya buibui maofisini kusikojulikana?
 
Back
Top Bottom