Changamoto za kimaisha zinataka kunifanya nichukue maamuzi magumu na ya kishetani

Mkuu wewe siyo mtu mzuri aisee...

Umenipa hiyo namba hapo nimejaribu tu kui save kwenye simu, kui-check WhatsApp nikakutana na profile picture ya Machatu mawili hapo hapo nikaifuta na namba maana inaonekana ni uchawi mtupu
si unataka hela acha uoga si unatamani kulala kwenye gorofa na ku drive v8 mkuu haya magorofa usitamani yana siri nyingi
 
Mtoto wa kiume unatafuta sympathy, unataka watu wakuonee huruma , katika watu wenye maisha magumu wewe hauna maisha magumu unapata mpaka bundle la ku-post JF , kuna watu hata darasa la saba hawajafika kipato hakuna tena wana uremavu na magonjwa makubwa kama kansa wanaoza wanajiona alafu wewe unasema unamaisha magumu acha ujinga wewe
Hivi Umaskini ni nini
 
Tuachane na yote Mimi nimependa tu hapo kwenye $150k kwa mwezi kwa jinsia ke
Na sikutaka kumuuliza kwanini KE apewe USD 150k alafu ME apewe USD 100k

Labda wanawake kila mahali ni kipaumbele kama kwenye taasisi zingine tunavyowaonaga...kuwa empowered
 
-The law of attraction says that you can attract positive things into your life by thinking positive thoughts and vice versa

-There is the price to pay to make the changes you want in life

ukielewa hapo hupati hata shida
Nimeelewa kwenye ya pili "There is the price to pay to make changes in your life "

Even an act of selling your soul to the devil is the price, don't you know that ?
 
Namba zinanunuliwa tu dollar 3 kwa mwezi unapta namba ya nchi yoyote, na unaweza piga na kupigiwa na kutumiwa sms za kawaida kama uko nchi husika kweli.

Kwenye hili la kununua code number ya nchi sikuwa najua
 
“Ukiangalia maisha ya baba, mama na wadogo zako roho inakuuma... ni umaskini unaofedhehesha”!

Wao hawaumii na wameridhika, wewe kivipi unateseka?

Utakuwa umeiga maisha ya wengine huku ukilinganisha na ya familia yako, ni kujipa msongo wa mawazo na haitokuacha salama.
Kauli yako inaweza kumfanya mtu aridhike na umaskini wake na kukubali kuwa yeye atakufa masikini hata kama ana uwezo wa kupambana kuyabadilisha maisha yake
 
“Kifo huja pale mwanachama anapotoa siri kwa wasiohusika”!

Wakati huo yeye anakupa siri hizo ungali si mwanachama!
Hakuna siri nilizopewa za maana hapa, wanachojua nini illuminati wanafanya na mission yao nini, ni wanachama pekee ndiyo wanaojua
 
si unataka hela acha uoga si unatamani kulala kwenye gorofa na ku drive v8 mkuu haya magorofa usitamani yana siri nyingi
Hakuna mahali nimekuambia mimi nataka maghorofa aua mgari ya kifahari.

Wala siitaji mali za ziada mimi

Mimi ninachotaka ni kuwa na maisha ambayo naweza kumudu mahitaji yangu ya msingi kimaisha pamoja na na familia yangu.

Nikiwa na nyumba yangu ya kuishi,mke wangu na watoto.wangu wanakula vzuri wanavaa vizuri wanapata elimu bora basj mm hayo yanatosha.

Maghorofa sijui malambogirn sijui Burgatti siyo matamanio yangu mimi.
 
Huyu ni graduate wa university of Dar elimu yetu ina kasoro mahara mind set yako ni ya witchcraft duh....
Elimu ya chuo kikuu haijawahi kuwa chanzo cha utajiri

Utajiri wa mlata mada uko kwenye akili ya sema amechagua kuwa mjinga kwahio lazima awe masikini tu unless abadilike

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu wakuu.

Bila kuwachosha nina maada ya ku-share na ninyi ingawa sijui kama hili jukwaa ni sahihi ama laa mtanisamehe bure.

Kiufupi mimi ni kijana wa 26 years na sijaoa bado ila kuna changamoto kadhaa za maisha zinanitia wazimu sana kiasi cha kunifanya nianze kufikiri nje box tena kwenye mambo yanayohusiana na ushetani kabisa (Freemasons & Illuminati societies).

Nilibahatika kusoma (Level ya degree moja) na nilihitimu mwaka 2018 lakini mpaka sasa ajira ya uhakika sijaipata,

Kuna mahali tu nimejiegesha napata Tsh 380,000/= per month.

Tatizo ni kwamba matumizi ni mengi kuliko kipato changu natakiwa nilipie chumba, nilipie umeme, nilipie maji, ninunue vitu vya kula ndani na kinachonigharimu zaidi ni kuwa na wategemezi wengi hasa wazazi na wadogo zangu.

Kwa hiyo huwa najikuta kipato changu cha mwezi siyo kitu (hakitoshi hata robo ya matatizo yangu) na kibaya zaidi kinachonitia stress ni kwamba kila mwisho wa mwezi unapofika matatizo huanza kujizalisha kwa fujo kama mvua.

Sasa nimekuja kujitafakari na kuona kwamba nitaishi kwenye maisha ya umaskini na fedheha hadi lini?

Ni lini mimi nitafanikiwa na kuwa na maisha yangu na kuonekana kwamba niliishi duniani? Nikiangalia familia yangu Baba, Mama na wadogo zangu maisha wanayoishi inaniuma sana kwa sababu ni umaskini unaofedhehesha.

Kutokana na kulemewa na mawazo ya umaskini na katika kufikiri namna ya kuanza kujikomboa kwenye umaskini, ndipo nilipokutana na jamaa mmoja Mmarekani wa huko Los Angeles.

Huyu jamaa ni mzungu na alinitumia Email akisema yeye ni Agent wa Illuminat (Devil worshiper Master) na akasema huko kuna Utajiri, umaaarufu, Nguvu n.k

Akanipa namba ya WhatsApp tukaanza kuchati.

Nikachati nae mambo mengi sana kuhusu jamii ya Illuminati ila key point niliyomuuliza ni kwamba "Is there any blood or human sacrifices in this society ?"

Yeye akanijibu "NO" na nikaona kama hakuna kafara ya damu wacha nijaribu nimechoka kufedheheshwa na Umaskini.

Tukaanza process zote za kujiunga akanipa form ya kujaza nikajaza na masharti kama 15 hivi nikayasoma ila sharti nililoliona gumu lilisema "Nisioe Wala kufanya mapenzi mpaka pale nitakapopata ruhusa kutoka kwa Master wao".

Lakini bado sikukata tamaa kutokana na hilo sharti maana katika masharti yote 15 ilikuwa hakuna hata sharti moja linalosema kuwa nitatakiwa kutoa kafara ya damu.

Nikamwambia tuendelee mbele kwa ajili ya initiation process.

Nilikuja kushindwana nae aliponiomba USA dollar 200, nikamuuliza kama nyie ni matajiri na mnatoa pesa Je dollar 200 kwangu unaitaka ya nini?

Akanijibu kuwa "It is a sacrifice for Lucifer to help you "

Nikaona huyu jamaa nitapeli nikam-block muda huo huo.

Sasa picha lingine limekuja juzi, kuna jamaa mmoja hivi kani follow Instagram anaitwa Illuminati 666, baada ya kuni- folllow nili agree request alafu baadae akanitumia ujumbe mrefu sana DM.

Akasema yeye ni Devil Worshiper na anawaleta watu kwenye ulimwengu wa mafanikio na pia akasema watu wanaotozwa pesa kama ada ya kujiunga ni uwongo kwani kujiunga na Illuminati ni free ili mradi tu uwe umekidhi vigezo.

Huyu jamaa nilimuuliza maswali mengi sana lakini badae nilijiridhisha kuwa siyo tapeli wa kuomba hela kama yule wa kwanza.
Na akanambia in Iluminatti - no bloodshed

- no registration fee

- no human sacrifice

Nikaona imekaa poa.tukaanza process zote ila tu alinipa angalizo kwamba kifo huja pale mwanachama anapotoa siri kwa watu wasiohusika (ambao si wanachama)

Aisee niwe mkweli kwamba nimeshafanya process zote hadi kitambulisho cha NIDA nishamtumia na picha yangu moja kwa ajili ya kunitengenezea Identity card ya Illuminati.

Sasa process iliyopo kwa sasa ameniambia nimtumie video ya dakika 2 ya kuomba kwamba nataka Mungu wao (wao wanamwita BAPHOMET) anifanyie nini.

Na kilichonipa wakati mgumu niandike hapa ni kwamba kuna maneno ambayo amenipa nianze nayo na kumalizia nayo na ni kama kiapo hivi ila na maneno makali sana hadi nafsi inatetemeka ninapoyataja tu.

Yanasema hivi "Hail the Lucifer, The leader of this world who created Men and women, Hail the light and open the gate of Hell to come and hug me your brother, Hail our Lord BAPHOMET"

Mengine sijayataja maana ni sala ndefu kidogo amenambia kuwa hayo maneno hapo juu ni very spiritual kuwa nitakachokisema ndicho kitakachokuwa.

Sasa wakuu mimi kichonipa wakati mgumu ni kurekodi video nikiyasema hayo maneno hapo maana ni makali mno mpaka natetemeka mwenyewe ingawa umaskini nauchukia pia.

Na lengo mimi la kuingia huko ni niwe tu maisha mazuri na kusaidia wengine wenye uhitaji na wasiojiweza wala mengine sina mda nayo.

Ahadi alizoniahidi ni kwamba iwapo nitakidhi vigezo vya kukubaliwa basi nitapewa USA dollar elfu 60 kama zawadi ya kuanza maisha mapya.

Alafu baada ya hapo siku ya kwenda kula kiapo nitakutana na illuminati wa nchini kwetu ambao watanifanyia ceremony na kunipa zawadi kama nyumba, magari ama kunipa job offer kwenye kampuni zao ama kunifanyia promosheni yeyote ile.

Na pia kabla ya kuwa full member watakuwa wanatoa mshahara wa dollar laki moja kwa mwezi kwa mwanaume na dolla laki moja na nusu kwa mwezi kwa mwanamke kama njia ya kuwa full membership ambao hapo inaweza kuchukua miaka kadhaa pia.

Mimi nimeona kwamba haya ndiyo maisha nnayoyataka maana umaskini ushanifedhehesha sana.

NB: You will not success by any means if you will not sell your soul to the Lucifer, and money is something to some people but is nothing to those who made it"

Haya ndiyo maneno aliyoniachia.

Marko : Mlango 8​

36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Mark 8:36
[36]For what does it profit a man to gain the whole world, and forfeit his life [in the eternal kingdom of God]?
 
Almost every human Being now is under "New world order system "
 
Hayo maden si umeyavuta mwenyew unalipwa pesa ndogo cut down matumiz ya kishenz .
Unasema unafedheheshwa na nani ? Huna kitu ww fedhea kawaida yaan unaongea utafikiri Ulikuwa Milionea sasa umefulia ndio una fedheheshwa achaa bangi 380,000 pesa nzuri sana bado huna mambo mengi ila kichwa chako kimejaa mambo ya kuiga maisha ya watu.
Kwa matatizo yanayoniangalia hii pesa si chochote ...na pia najikuta nna madeni kuliko hata kipindi sina kazi
 
Huge price
Nimeelewa kwenye ya pili "There is the price to pay to make changes in your life "

Even an act of selling your soul to the devil is the price, don't you know that ?
You will serve. and you will be of service...Under the High table
Anytime /Anywhere
 
Usijisifu upo makin na hela na ID zako umetumaa (private info)
Kwenye suala la pesa niko makini sana siwezi kutapeliwa ila nashukuru umenifumbua kitu maana kweli naweza aaambiwa nimefuzu kila kitu alafu kwenye kupewa dola ndo niambiwe nitume dola 200 alafu ndiyo nigundue kuwa mlolongo wote ilikuwa tu njia ya kutapeliwa
 
vijana tupo kasi sana na maisha mi namiliki Sabufa tu hapa geto na degree yangu mshahara 350k kijana anapiga kelele anafedheheshwa daaah
Ukishakolea vizuri Kuna siku watakwambia tuma video ukiwa Uchi hapo ndo utafurahi show, maana watakublackmail wakupige pesa mingi.
Watakutishia kusambaza video yako, mwishowe utakuwa frustrated unajinyonga bure. Duniani hakuna pesa ya bure .
Wenzako wana miaka 5 bila ajira bado wapo nyumbani wewe miaka 2 tu unaanza kulialia FUCKOFF
 
Habari zenu wakuu.

Bila kuwachosha nina maada ya ku-share na ninyi ingawa sijui kama hili jukwaa ni sahihi ama laa mtanisamehe bure.

Kiufupi mimi ni kijana wa 26 years na sijaoa bado ila kuna changamoto kadhaa za maisha zinanitia wazimu sana kiasi cha kunifanya nianze kufikiri nje box tena kwenye mambo yanayohusiana na ushetani kabisa (Freemasons & Illuminati societies).

Nilibahatika kusoma (Level ya degree moja) na nilihitimu mwaka 2018 lakini mpaka sasa ajira ya uhakika sijaipata,

Kuna mahali tu nimejiegesha napata Tsh 380,000/= per month.

Tatizo ni kwamba matumizi ni mengi kuliko kipato changu natakiwa nilipie chumba, nilipie umeme, nilipie maji, ninunue vitu vya kula ndani na kinachonigharimu zaidi ni kuwa na wategemezi wengi hasa wazazi na wadogo zangu.

Kwa hiyo huwa najikuta kipato changu cha mwezi siyo kitu (hakitoshi hata robo ya matatizo yangu) na kibaya zaidi kinachonitia stress ni kwamba kila mwisho wa mwezi unapofika matatizo huanza kujizalisha kwa fujo kama mvua.

Sasa nimekuja kujitafakari na kuona kwamba nitaishi kwenye maisha ya umaskini na fedheha hadi lini?

Ni lini mimi nitafanikiwa na kuwa na maisha yangu na kuonekana kwamba niliishi duniani? Nikiangalia familia yangu Baba, Mama na wadogo zangu maisha wanayoishi inaniuma sana kwa sababu ni umaskini unaofedhehesha.

Kutokana na kulemewa na mawazo ya umaskini na katika kufikiri namna ya kuanza kujikomboa kwenye umaskini, ndipo nilipokutana na jamaa mmoja Mmarekani wa huko Los Angeles.

Huyu jamaa ni mzungu na alinitumia Email akisema yeye ni Agent wa Illuminat (Devil worshiper Master) na akasema huko kuna Utajiri, umaaarufu, Nguvu n.k

Akanipa namba ya WhatsApp tukaanza kuchati.

Nikachati nae mambo mengi sana kuhusu jamii ya Illuminati ila key point niliyomuuliza ni kwamba "Is there any blood or human sacrifices in this society ?"

Yeye akanijibu "NO" na nikaona kama hakuna kafara ya damu wacha nijaribu nimechoka kufedheheshwa na Umaskini.

Tukaanza process zote za kujiunga akanipa form ya kujaza nikajaza na masharti kama 15 hivi nikayasoma ila sharti nililoliona gumu lilisema "Nisioe Wala kufanya mapenzi mpaka pale nitakapopata ruhusa kutoka kwa Master wao".

Lakini bado sikukata tamaa kutokana na hilo sharti maana katika masharti yote 15 ilikuwa hakuna hata sharti moja linalosema kuwa nitatakiwa kutoa kafara ya damu.

Nikamwambia tuendelee mbele kwa ajili ya initiation process.

Nilikuja kushindwana nae aliponiomba USA dollar 200, nikamuuliza kama nyie ni matajiri na mnatoa pesa Je dollar 200 kwangu unaitaka ya nini?

Akanijibu kuwa "It is a sacrifice for Lucifer to help you "

Nikaona huyu jamaa nitapeli nikam-block muda huo huo.

Sasa picha lingine limekuja juzi, kuna jamaa mmoja hivi kani follow Instagram anaitwa Illuminati 666, baada ya kuni- folllow nili agree request alafu baadae akanitumia ujumbe mrefu sana DM.

Akasema yeye ni Devil Worshiper na anawaleta watu kwenye ulimwengu wa mafanikio na pia akasema watu wanaotozwa pesa kama ada ya kujiunga ni uwongo kwani kujiunga na Illuminati ni free ili mradi tu uwe umekidhi vigezo.

Huyu jamaa nilimuuliza maswali mengi sana lakini badae nilijiridhisha kuwa siyo tapeli wa kuomba hela kama yule wa kwanza.
Na akanambia in Iluminatti - no bloodshed

- no registration fee

- no human sacrifice

Nikaona imekaa poa.tukaanza process zote ila tu alinipa angalizo kwamba kifo huja pale mwanachama anapotoa siri kwa watu wasiohusika (ambao si wanachama)

Aisee niwe mkweli kwamba nimeshafanya process zote hadi kitambulisho cha NIDA nishamtumia na picha yangu moja kwa ajili ya kunitengenezea Identity card ya Illuminati.

Sasa process iliyopo kwa sasa ameniambia nimtumie video ya dakika 2 ya kuomba kwamba nataka Mungu wao (wao wanamwita BAPHOMET) anifanyie nini.

Na kilichonipa wakati mgumu niandike hapa ni kwamba kuna maneno ambayo amenipa nianze nayo na kumalizia nayo na ni kama kiapo hivi ila na maneno makali sana hadi nafsi inatetemeka ninapoyataja tu.

Yanasema hivi "Hail the Lucifer, The leader of this world who created Men and women, Hail the light and open the gate of Hell to come and hug me your brother, Hail our Lord BAPHOMET"

Mengine sijayataja maana ni sala ndefu kidogo amenambia kuwa hayo maneno hapo juu ni very spiritual kuwa nitakachokisema ndicho kitakachokuwa.

Sasa wakuu mimi kichonipa wakati mgumu ni kurekodi video nikiyasema hayo maneno hapo maana ni makali mno mpaka natetemeka mwenyewe ingawa umaskini nauchukia pia.

Na lengo mimi la kuingia huko ni niwe tu maisha mazuri na kusaidia wengine wenye uhitaji na wasiojiweza wala mengine sina mda nayo.

Ahadi alizoniahidi ni kwamba iwapo nitakidhi vigezo vya kukubaliwa basi nitapewa USA dollar elfu 60 kama zawadi ya kuanza maisha mapya.

Alafu baada ya hapo siku ya kwenda kula kiapo nitakutana na illuminati wa nchini kwetu ambao watanifanyia ceremony na kunipa zawadi kama nyumba, magari ama kunipa job offer kwenye kampuni zao ama kunifanyia promosheni yeyote ile.

Na pia kabla ya kuwa full member watakuwa wanatoa mshahara wa dollar laki moja kwa mwezi kwa mwanaume na dolla laki moja na nusu kwa mwezi kwa mwanamke kama njia ya kuwa full membership ambao hapo inaweza kuchukua miaka kadhaa pia.

Mimi nimeona kwamba haya ndiyo maisha nnayoyataka maana umaskini ushanifedhehesha sana.

NB: You will not success by any means if you will not sell your soul to the Lucifer, and money is something to some people but is nothing to those who made it"

Haya ndiyo maneno aliyoniachia.
There is a lot of treachery in the promises you have been given. The truth of the matter just to be brief is that, your life will be very miserably once you join that camp to the extent you would wish to undo what you have done but it will be impossible. Trust me the devil is a liar and works in lies. Money, like they promised you, is nothing to them. What they want is your soul.
Be not deceived. If you get into that trap its done for you my friend.
Chukua hii warning mapema sana.
Only God the Father is the one true God who made heaven and earth and human being and everything in this world.
That we read in Bible, shetani huyo Lucifer has never contributed a single thing in creation rather than destroying what God created.
Dont sell yourself cheap. You will get the money but you will NEVER enjoy nor use it to help anyone as you desire to do so.
Nimemaliza
 
Back
Top Bottom