Changamoto ya usafiri; Bora mabasi yote yapakie na kushusha abiria Stendi ya Magufuli

mgungani

Member
May 13, 2022
38
60
Changamoto nilizokutana nazo leo bora magari yote yapakie stendi ya Magufuli iliyopo Mbezi. Nimepanda gari ya Ester Kitunda saa 10.20 nikashushwa River Side.

Nikapandishwa basi jingine kutoka Buza nikashushwa magari saba usiku. Hapo magari saba hakuna choo wala kiti.

Nikasubiri hapo mpaka saa moja kasoro ndio basi likaja. Hapo magari saba hakuna stendi wala nini ni porini, kondakt, ajenti, dereva kila mtu anasema lake.

Watu wanaachwa vituoni na hakuna mwongozo wowote. Customer care ni sifuri, bora magari yote yaingie stendi ya Magufuli kuliko kusubirishwa porini bila utaratibu sahihi.
 
Ulikua unaenda wapi Mkuu?

Next time tuulize magari mazuri yenye customer service A plus.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom