Acceptable
Senior Member
- Oct 7, 2020
- 153
- 302
Habari wakuu.
Kuna changamoto ambayo mawakala wa huduma za kifedha kama vile M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na T-Pesa wanazopitia hasa katika upande wa kufanya miamala. Lakini tatizo lipo sana upande wa M-pesa.
Nikiri kwamba kufanya miamala ni biashara kama biashara zingine duniani ambazo zinahitaji mtu apate faida ili aendelee kufanya biashara hiyo. Inapotokea mtu hapati faida basi biashara yake itakufa.
Kumekuwa na tahadhari kutoka mitandao ya simu hasa Vodacom (M-Pesa) kwamba wakala ukimuwekea pesa mtu ambae yupo mbali hautalipwa kamisheni yako ya muamala huo. Hii inaweza kuwa sawa kwasababu za kibiashara lakini kwa mawakala hili ni tatizo kwasababu mtu anaweza kudanganya kuwa anaweka pesa kwenye simu yake kumbe anamtumia mtu wa mkoa mwingine tofauti na alipo (Kumbuka huwezi kumwambia mteja lete simu yako hapa nione kama SMS ya muamala unaingia kwako). Mwisho wa siku hii inakuwa imekula kwako wewe wakala kwa kukosa kamisheni yako.
Nini kifanyike?
Makampuni haya ya simu yatengeneze mfumo (Automatic Location Detection) ambao utawawezesha mawakala kupewa WARNING wakati wanaweka pesa kwa mteja kama yuko mbali simu ikutahadhalishe kwamba "mtu unaemuwekea hela yupo mbali na eneo lako hivyo hautalipwa kamisheni yako, kuendelea bonyeza labda "1" kusitisha muamala bonyeza "2".
Hii itasaidia kuwapatia kamisheni zinazostahili mawakala wanaowasaidia kuwafikishia huduma karibu na wananchi.
NAOMBA TUSAIDIE KUFIKISHA UJUMBE HUU SEHEMU HUSIKA.
ASANTE