Changamoto ya maji itatuliwe ili kuboresha shughuli za maendeleo kijamii.

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Tunajua kwamba maji ni uhai mia ni hitaji la muhimu kwa kila mmoja wetu, lakini kumekuwa na baadhi ya maeneo ambayo yanasumbuliwa na upungufu wa vyanzo vya maji ikiwemo visima mabwawa na hata mito hali inayosababishwa na asili ya eneo hilo la kijographia au hata mabadiliko ya tabia ya nchi.

Katika maisha yetu maji yana kazi nyingi sana katika jamii ikiwa ni pamoja na kunywa, kupikia, Kufuria, kuoshea, kuogea na pamoja na shughuli zingine zisizokuwa na ulazima sana kama zile zinazolenga kilimo bora cha umwagiliaji, Na pia katika uzalishaji wa nishati mbalimbali ikihusisha ufuaji wa umeme kwa kutumia maji.

Lakini kama wewe ni mfuatiliaji mzuri utaona kuwa kuna kipindi kirefu sana bado kuna baadhi ya maeneo mengi ya vijijini wakina mama wengi wamekuwa wakijitwisha ndoo za maji vichwani huku wakitembea umbali mrefu kwenda kuyatafuta maji hayo. Ambapo labda maji yangelikuwa karibu mama huyo angelipata wasaa wa kufanya majukumu mengine ya kijamii katika kujipatia kipato lakini imekuwa ndivyo sivyo wengi wao wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhangaikia kwa kuyapata maji hayo, swala ambalo ni kisababishi mojawapo cha kurudisha nyuma maendeleo ya raia na wanachi kwa ujumla.

Na hili linatokea maeneo mengi hasa katika mikoa mbalimbali tanzania nimeliona hili katika baadhi ya maeneo ikiwemo mtwara, songea pamoja na mbeya. Ambapo kwa maeneo mengi maji ndilo limekuwa kama hitaji Lao peekee na sio kingine chochote

Kwa sababu wanaamini viongozi waliowachagua kwa kuwapigia kura watakwenda kufanya utekelezaji wa yale yote waliyopanga walipokuwa pamoja katika kuzijadili changamoto zinazowakabili wananchi kipindi cha kampeni.
Tuchukue nafasi hii kuiomba serikali na viongozi wake wa idara za maji na wadau wake wote ili kuweza kuchukua hatua ya kuwatua ndoo wakina mama kwa kuwafungia mabomba ya maji ili kwamba ifike muda na wao wapate nafasi ya kufanya shughuli zingine za kimaendeleo. Ili kuendeleza kusogeza gurudumu la maendeleo kwa taifa letu.
Asante.
 
Back
Top Bottom