Changamoto ya aviation industry: Baada ya ndege kupata hitilafu na kusitisha safari, Fastjet kulipa kila abiria shilingi 30,000 ya chai na nauli

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kampuni ya ndege ya Fastjet jijini Mwanza leo Jumapili Oktoba 28, 2018 imeeleza kusitisha safari zake kuanzia asubuhi hadi mchana kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam kutokana na ndege kupata hitilafu.

Abiria waliopaswa kusafiri saa 2:00 asubuhi sasa watasafiri saa 1:30 usiku wakati waliotakiwa kusafiri leo jioni, wataondoka Mwanza saa 5:00 usiku.

Uamuzi huo umetangazwa kwa mamia ya abiria waliojazana nje ya ofisi ndogo ya kampuni huyo katika uwanja wa ndege Mwanza.

“Kampuni itatoa Sh30,000 kwa kila abiria kwa ajili ya kunywa chai asubuhi na usafiri wa kurejea mjini wakati wa kusubiri muda wa safari," amesema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo

Mwanza kwa sharti la kutotajwa.
Kutokana na wingi wa abiria, muda wa abiria kuingia uwanja wa ndege itakuwa kuanzia saa 11:00 jioni."

Mfanyakazi huyo amewahakikishia abiria hao uhakika wa kusafiri jioni na usiku kutokana na hitilafu katika ndege kurekebishwa.


     
 
Hivi na atcl huwa wanatoa chochote baada ya safari kuhailishwa!??
 
Hivi na atcl huwa wanatoa chochote baada ya safari kuhailishwa!??
Abiria wa ndege huwa hawatelekezwi kama wa mabasi na kuna wakati hoteli unawakodia kama ikibidi.

Kwa mfano, Precision au ATCL nakumbuka waliwahi kuwalaza abiria wao Tabora Hoteli mwaka 2010 kama sikosei baada ya ndege kupata hitilafu.
 
Back
Top Bottom