Changamoto uchumi wa viwanda: Somo kutoka ufisadi wa China kwenye vita ya kibiashara na Marekani

Volatility

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,920
7,469
Baada ya kuona mategemeo yao ya kuziwekea vikwazo vya kikodi (Tariffs) bidhaa zinazoingizwa nchini Marekani kutokea china hayafikii malengo, Serikali ya Marekani imegundua wizi wa kukwepa vikwazo unaofanywa na Uchina.

Mategemeo ya Wamarekani ilikuwa ni kuona udhalishaji nchini China kushuka kwa kukosa soko la Marekani sababu ya bei za bidhaa zao kupanda na kuyapa mataifa mengine fursa ya kuzalisha na kuuza bidhaa zao kwa bei nafuu nchini marekani sababu hazina matariffs.

Hii imekuwa ni kinyume, sababu uchumi wa China umeonekana kuendelea kukua japo kwa mdororo kidogo sana, huku China ikiendelea kuonyesha uwezo wa kuhimili vikwazo hivyo kwa muda mrefu.

Sasa imebainika hata kwenye hili wachina wanaiba, taarifa za kibiashara zinaonyesha wakati huko marekani manunuzi ya bidhaa zikizowekewa vikwazo kutoka nchini china yameshuka.

Mauzo ya bidhaa hizo hizo kutoka China kwenda nchini Taiwani yameongezeka,

wakati huo huo manunuzi ya bidhaa hizo hizo huko nchini marekani kutokana nchini Taiwani yameongezeka.

Maana yake, wachina wanapeleka bidhaa zao nchini Taiwani, zikifika huko zinabadirishwa documentations na kuonekana zimezarishwa nchini humo (Taiwani) alafu zinauzwa kwenda marekani huku Taiwani ikionekana kana Country of Origin. Marekani anakuwa looser kwenye matariffs yake.

Sasa wao acha waendelee na Mapambano.

Hoja yangu ni kwamba wizi wa namna hii uko hata hapa hapa nchini kwetu na ndio kilikuwa chanzo cha Mpango wa Marekani kusaidia nchi zinazoendelea kupiga hatua ya maendeleo kwa kuwa nchi za viwanda katika mpango wake wa AGOA kutozaa matunda.

Hapa nyumbani vipo viwanda vya wachina ambavyo viko katika export processing zones, malengo ya viwanda hivi ni kuongeza ajira pamoja na kusaidia ukuzaji wa thamani wa marighafi zinazopatikana nchini.

sasa wachina hawa, well pamoja na wahindi, kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo serikali wanatumia mwanya wa uzembe na ujinga katika uendeshaji wa bandari zetu hasa ya Zanzibar wanaagiza bidhaa zilizotengezwa nje ya nchi, hasa india na uchina, wanazileta hapa alafu wanabadirisha makaratasi alafu zinaondoka kuelekea marekani n.k kisha tunareport export growths huku sisi wapinzani wa serikali za CCM tukisema data ni fake sababu ukuaji huo wa exports hauendani na ukuaji wa ajira wa nafuu ya kiuchumi wa wazalishaji wa marighafi.

Serikali itupie macho swala hili, ama sivyo Tanzania ya viwanda itakuwa Tanzania ya vi wonder.
 
Ujasusi wa kiuchumi

Uchumi wa viwanda kwa Tanzania must be a process. Lazima uandae mambo yafuatayo kwanza kabla ya kuingia kwenye uchumi wa viwanda (Prelude to Industrialization)

1. Mapinduzi ya Kilimo ili kuwa na uhakika wa malighafi za viwanga. Lazima kuwe na mapinduzi katika kilimo kuwe na kilimo cha mashine chenye tija. Agrarian revolution
2. Miundo mbinu kama umeme mwingi sana wa uhakika hadi maporini, reli kila mkoa, meli na pantoni nyingi, barabara pana na nzuri kila mahali, maji safi hadi maporini, huduma za uhakika za afya na usalama kama polisi na firefighters wa uhakika na ufanisi,
3. Serikali na taasisi zenye nidhamu na misimamo kwaajili ya kuwa regulators and enablers. Serikali inayowapenda nakuwa support wafanya biashara na wawekezaji. Sasa hivi ukidhulumiwa hapa tanzania ni ngumu kupata haki kwa haraka. Hata fair competition commission ni maigizo tu
4. Sheria madhubhuti za kuimarisha na kulinda biashara, viwanda. Sasa hivi ukipeleka idea yako Tume ya Sayansi wanakuambia hii mbona kuna mtu alishaleta - kumbe uongo ukiondoka wanaichuku wao
5. Masoko ya uhakika
6. Watu wenye uwezo na uchumi wa kati amabo ndio buyers - purchasing power

Ukishakua na mambo ya msingi kama hayo ndio unaweza kuingia uchumi wa viwanda
 
Baada ya kuona mategemeo yao ya kuziwekea vikwazo vya kikodi (Tariffs) bidhaa zinazoingizwa nchini Marekani kutokea china hayafikii malengo, Serikali ya Marekani imegundua wizi wa kukwepa vikwazo unaofanywa na Uchina.

Mategemeo ya Wamarekani ilikuwa ni kuona udhalishaji nchini China kushuka kwa kukosa soko la Marekani sababu ya bei za bidhaa zao kupanda na kuyapa mataifa mengine fursa ya kuzalisha na kuuza bidhaa zao kwa bei nafuu nchini marekani sababu hazina matariffs.

Hii imekuwa ni kinyume, sababu uchumi wa China umeonekana kuendelea kukua japo kwa mdororo kidogo sana, huku China ikiendelea kuonyesha uwezo wa kuhimili vikwazo hivyo kwa muda mrefu.

Sasa imebainika hata kwenye hili wachina wanaiba, taarifa za kibiashara zinaonyesha wakati huko marekani manunuzi ya bidhaa zikizowekewa vikwazo kutoka nchini china yameshuka.

Mauzo ya bidhaa hizo hizo kutoka China kwenda nchini Taiwani yameongezeka,

wakati huo huo manunuzi ya bidhaa hizo hizo huko nchini marekani kutokana nchini Taiwani yameongezeka.

Maana yake, wachina wanapeleka bidhaa zao nchini Taiwani, zikifika huko zinabadirishwa documentations na kuonekana zimezarishwa nchini humo (Taiwani) alafu zinauzwa kwenda marekani huku Taiwani ikionekana kana Country of Origin. Marekani anakuwa looser kwenye matariffs yake.

Sasa wao acha waendelee na Mapambano.

Hoja yangu ni kwamba wizi wa namna hii uko hata hapa hapa nchini kwetu na ndio kilikuwa chanzo cha Mpango wa Marekani kusaidia nchi zinazoendelea kupiga hatua ya maendeleo kwa kuwa nchi za viwanda katika mpango wake wa AGOA kutozaa matunda.

Hapa nyumbani vipo viwanda vya wachina ambavyo viko katika export processing zones, malengo ya viwanda hivi ni kuongeza ajira pamoja na kusaidia ukuzaji wa thamani wa marighafi zinazopatikana nchini.

sasa wachina hawa, well pamoja na wahindi, kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo serikali wanatumia mwanya wa uzembe na ujinga katika uendeshaji wa bandari zetu hasa ya Zanzibar wanaagiza bidhaa zilizotengezwa nje ya nchi, hasa india na uchina, wanazileta hapa alafu wanabadirisha makaratasi alafu zinaondoka kuelekea marekani n.k kisha tunareport export growths huku sisi wapinzani wa serikali za CCM tukisema data ni fake sababu ukuaji huo wa exports hauendani na ukuaji wa ajira wa nafuu ya kiuchumi wa wazalishaji wa marighafi.

Serikali itupie macho swala hili, ama sivyo Tanzania ya viwanda itakuwa Tanzania ya vi wonder.

Nakala imfikie Waziri wa Viwanda Mh. Innocent Bashungwa
 
Back
Top Bottom