Fursakibao
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 6,676
- 11,109
Habari za mida wadau wenzangu wa kilimo.
Niende moja kwa moja ni share safari yangu kwenye hii fani ya kilimo ili wale wanaotegemea kujiunga wapate ka uzeofu kadogo japo wapate pa kuanzia.
Nimekuwa nikifanya shuguli za kilimo toka mwaka 2014 toka hapo nimekuwa nikipata na kukosa pia.
Nilianza kulima tumbakuku mwaka 2014 huko wilaya ya Serengeti; katika hichi kilimo cha tumbaku tulifanikiwa kupata milioni 20 ambazo tuligawana kwani tulilima kifamilia.
Mwaka 2015 nikalima Mahindi na Alizeti wilaya ya kiteto; ambapo nilifanikiwa kuvuna tani 15 za mahindi na tani 6 za alizeti.
Mwaka 2016 nililima heka 50 za mahindi, mbaazi pamoja na alizeti wilaya ya Kiteto. Huu mwaka sikupata hata shilingi kumi, hivyo nikaishia kupata hasara ya milioni 10.
Mwaka 2017 /18 nililima matikiti maji pamoja na pilipiili hoho. Hichi kilimo kilikuwa tofauti na vingine kwani nilijikita zaidi katika kilimo cha umwagiliaji licha ya kufanya kilimo cha umwagiliaji niliishia kupata hasara ya Milioni 8.
Kulingana na hasara nilizo zipata mwaka 2016 – 2018 nilighafirika sana na kuamua kupumzika kwa muda huku nikitafuta njia ya kukabiliana na changemoto zilizosababisha nipate hasara.
Mimi sio mwandishi mzuri na ni mvivu pale linapokuja suala la kuandika makala ila nitajitahidi kuandika ili wale wanaotarajia kuingia kwenye kilimo wajifunze kitu.
Hivyo basi nitajitahidi kuchambua hizi changamoto kwa kila msimu niliolima.
2015
Huu mwaka kama nilivyoeleza hapo juu sikupata hasara japokuwa nilichokipata kilikuwa chini ya matarajio kwa sababu ya changamoto zifuatazo:
1. Kukosa muda wa kusimamia shamba kwa 100%
Hii ni moja ya changamoto inayotukabili wakulima wengi ambao tunajihusisha na kilimo wakati huo huo tukiwa tumeajiliwa hivyo; kukosa muda wa kulisimamia shamba kwa 100% kulipelekea kazi kufanyika chini ya kiwango kinachotakiwa hivyo kupelekea mimi kupata mavuno kidogo.
Mambo vitu vilivyosababisha nipate mazao chini ya mategemeo vilikuwa:
i. Eneo lililolimwa lilikuwa chini ya lile liliotakiwa kulimwa. Nilipanga nilime heka 45 matokeo yake nilikuta heka 35 tu.
ii. Palizi kutofanyika kwa wakati. Kati ya hizo heka 35 nilikuta heka 10 hazijapaliliwa kabisa licha ya kwamba nilipokuwa napiga simu kuulizia naambiwa shamba liko vizuri. Siku nilipofika shambani nilitaka kulia kwani hali niliikuta kama muonavyo hapo chini.
iii. Kuibiwa mazao wakati wa mavuno. Hapa niliibiwa kiasi ambacho siwezi kujua kilikuwa ni kiasi gani kwani tulikuwa tunavuna alafu tunaacha mazao shambani mpaka siku inayofuata. Picha hapo chini
Itaendelea.