Hii habari hapa chini toka Raiamwema ni uwongo mtupu. Mwandishi ameshindwa hata kutambua jambo rahisi la kujua kwamba Dr. Mwakyembe sio mjumbe wa NEC ya CCM.
Acheni kuutumia mkoa wa Mbeya kuendeleza vita ambavyo havipo.
Sources zangu zote za huko Mbeya zinaonyesha hakuna kitu kama hicho. Baadhi ya waandishi wa habari wana sababu zao za kutaka kuona ugomvi huu unaendelea kwa cost ya wananchi wa Mbeya.
Hakuna kikao cha kuwajadili Mwandosya na Mwakyembe na wala Prof. hana mpango wa kugombea urais mwaka 2010.
Inaelekea kuna watu wanakuza hayo maneno kwa faida zao binafsi.
Mwandosya, Mwakyembe waundiwa mzengwe
Mwandishi Wetu Aprili 23, 2008
HASIRA za wanamtandao waliojeruhiwa na sakata la Richmond sasa zimeelekezwa mkoani Mbeya kuhakikisha viongozi wawili maarufu mkoani humo, Profesa Mark Mwandosya na Dk. Harrison Mwakyembe wanamalizwa kisiasa, Raia Mwema imeambiwa.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili lilizipata mjini Mbeya, hivi karibuni, hasira dhidi ya Mwandosya na Mwakyembe ambao wote ni wajumbe wa NEC ya CCM, zimejengeka baada ya Edward Lowassa kulazimika kujiuzulu uwaziri mkuu kutokana na taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kumhusisha na kashfa ya Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na Dk. Mwakyembe.
Aidha, ushindi wa Profesa Mwandosya katika kinyanganyiro cha kuwania ujumbe wa NEC (Mbeya) dhidi ya Tom Mwangonda, mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Cornel Apson, umeacha majeraha mabichi CCM mkoani Mbeya.
Taarifa za uhakika ndani ya chama hicho mkoani Mbeya zinasema kwamba maandalizi ya tuhuma nzito dhidi ya wanasiasa hao wawili ambao pia wana mahusiano ya karibu, yamekwisha kukamilika na kwamba kilichobakia ni kuwaandikia barua za kuwaita kujitetea katika kikao cha Chama kinachotarajiwa kuitishwa hivi karibuni.
Maandalizi ya mkakati huu yalianza siku nyingi wakati wa uhai wa Katibu wa CCM mkoani Mbeya, Silvester Kikungwe (marehemu) na sasa inadaiwa kuwa yamekamilishwa na Mwenyekiti mpya wa CCM wa mkoa, Nawab Mulla, alisema ofisa mmoja wa CCM mkoani humo ambaye kwa sababu za wazi hakutaka jina lake litajwe.
Ofisa huyo alitoa mfano wa kikao cha Wazee wa Mkoa kilichoitishwa na Mulla kwa lengo la kutoa tamko la kuwatuhumu Mwandosya na Mwakyembe kuwa wanadhoofisha chama, lakini ikashindikana baada ya viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho kupinga utoaji wa tamko hilo bila kwanza wahusika kuitwa kujitetea. Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe hawakuitwa katika kikao hicho kilichofanyika Februari mwaka huu mjini Mbeya.
Raia Mwema ilipomtafuta Mulla kueleza kwa undani suala hilo, iliambiwa kuwa alikuwa Dubai, lakini Katibu wake msaidizi, Zongo Lobe Zongo, alithibitisha kwamba kutakuwa na kikao cha CCM Mkoa wa Mbeya hivi karibuni, ingawa alisema hajui ajenda zake.
Kwa sasa Mwenyekiti yuko Dubai, lakini ninajua kuwa kutakuwa na kikao siku za karibuni. Ajenda sizijui, kwa sababu sekretarieti ndiyo inayopanga Wao ndio wanaweza kujua na inawezekana wao wamejadili wakati Mwenyekiti hayupo, alisema Zongo.
Hata hivyo, alipodokezwa kuhusu kuwajadili wanachama, ambao CCM Mkoa wa Mbeya inadai wanakigawa chama, Zongo alidai kwamba Mwenyekiti wake hawezi kuruhusu ajenda kama hiyo kujadiliwa kwenye kikao.
Lakini Raia Mwema imethibitishiwa na vyanzo vingine vya habari kwamba kesi inayotungwa dhidi ya Profesa Mwandosya, Mbunge wa Rungwe Mashariki na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, ni ya tuhuma kwamba ameanza mapema maandalizi ya kugombea urais mwaka 2010 kinyume cha taratibu za Chama, na kwamba akipita mitaani mkoani Mbeya baadhi ya watu humwita Rais , Rais. Tuhuma hizo pia zilipata kuandikwa na gazeti moja la wiki lililo karibu na wanamtandao hao.
Kuhusu Dk. Mwakyembe, taarifa zinasema kwamba tuhuma zake zimebadilishwa. Awali alikuwa anatuhumiwa kwa kumuunga mkono Profesa Mwandosya katika hicho kinachodaiwa kuwa ni maandalizi ya mapema ya kuwania urais mwaka 2010, lakini sasa anatuhumiwa kwa ukosefu wa utiifu kwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa (Mulla).
Kinachodaiwa kuwa ni ukosefu wa utiifu kwa Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa ni hatua ya Dk. Mwakyembe kukubali kupokewa na umati mkubwa wa watu siku aliporejea Kyela baada ya kuwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond ambayo hatimaye ilisababisha kujiuzulu kwa Lowassa, mawaziri Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.
Inadaiwa kwamba Mulla alimkataza asishiriki katika mapokezi hayo kwa kuwa hayakubarikiwa na Chama, na kwamba alikasirika zaidi baada ya Dk. Mwakyembe kueleza wakati akihutubia umati huo kwamba alikuwa amezuiwa na yeye (Mulla) kushiriki katika mapokezi hayo.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa CCM Mkoa, barua zenye tuhuma dhidi ya wanasiasa hao wawili tayari zimekwisha kutawanywa kwa baadhi ya wabunge wa CCM wa mkoa huo na kwamba njama hizo za kuwamaliza kisiasa Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe zinaeleweka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa kitaifa wa CCM walio kwenye mtandao na inadaiwa wameubariki mpango huo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini wanaamini kwamba kama kutokuelewana huko kwa CCM mkoa wa Mbeya hakutashughulikiwa, chama hicho kitaupoteza kabisa mkoa huo kwa wapinzani katika uchaguzi wa mwaka 2010.
Kampeni hii ya kuwamaliza kisiasa kama itafanikiwa itaiumiza sana CCM mwaka 2010. Kwanza Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe wana ushawishi mkubwa si tu kwenye majimbo yao bali vilevile mkoa mzima na pia miongoni mwa wabunge wenzao, alisema.
Profesa Mwandosya hakupatikana jana kwa simu kuzungumzia suala hilo, lakini Dk. Mwakyembe yeye alipopatikana hakupenda kulizungumzia suala hilo mbali ya kukiri kusikia kuwepo kwa tuhuma hizo dhidi yake.